Taarifa Kidogo Kuhusu Cloud Computing | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa Kidogo Kuhusu Cloud Computing

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jun 27, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Umewahi kujiuliza Serikali yetu inatumia Pesa kiasi gani kwa mwaka kwa ajili ya Kununua vifaa , programu , kuajiri na Elimu kwa wafanyakazi wake kwenye masuala ya Teknohama ? Sio serikali tu mfano wewe una kampuni yenye miradi 6 mikao tofauti nchini unatumia shilingi ngapi kwa mwaka kwa ajili ya kuhudumia vifaa hivyo , watu wanaosafiri kati ya sehemu kwa ajili ya kwenda kuchukuwa taarifa ambayo ingeweza kuwekwa kwenye mtandao .

  Kama hayo ni madogo unajua ni watu wangapi wanasafiri kila kukicha kwenda sehemu zingine za dunia kwenda kufanya kazi au mikutano ambayo ingeweza kufanywa kwa njia ya mtandao tu kwa gharama nafuu - Wenzetu kukutana ni nadra sana au kumwona amesafiri na lundo na makabrasha pia ni nadra kwa sababu popote anapoenda nyaraka zake na kazi zake anaweza kuzipata kwa njia ya mtandao Mfumo huu ni Cloud Computing

  Cloud Computing ni Huduma , Programu , na uhifadhi Taarifa unaowezeshwa kwa njia ya mtandao kupitia Komputa Zingine zilizo sehemu mbalimbali duniani ( Server ) , Njia hii inamtoa mtumiaji wa kompyuta wa kawaida kwenye utendaji wake wa kazi wa kila siku Bila kuangalia eneo alipo , Njia hii inafanya mapinduzi ya haja ya jinsi Watu wanavyofanya biashara , wafanyakazi wanavyofanya kazi zao , watafiti wanavyobadilishana taarifa na kufanya kazi pamoja .

  Miaka michache iliyopita tumeona ulimwengu wa teknohama ukibadilika kwa kiasi kikubwa haswa kwenye masuala ya kuhifadhi vitu kwa kutumia njia na vifaa mbalimbali ili visiharibiwe na mtu huyo aweze kutumia au kuhama navyo kwenda popote anapotaka yeye ulimwenguni .

  Mabadiliko ya kuhifadhi vitu yalihusiha matumizi ya floppy disk za ukubwa tofauti mpaka cd na DVD , kutoka Zip Drives ambazo hazikukaa sana kwenye soko mpaka kwenye External Hardrive, flash disk za aina mbalimbali , mfano zilipokuja hizi portable Hardrive watu watu walizinunua sana mpaka sasa hivi wanazidi kununua hata flashdisk .

  Teknologia za kuhifadhi vitu imebadilika sana siku hizi kuna watu na kampuni ambazo hazitegemei tena kuwa na Nafasi kubwa kwenye Komputa yake ili aweze kuhifadhi vitu vyake na endapo laptop au komputa hiyo ikipotea au kuibiwa ina maana anakuwa amepoteza vyote wengi wao wanahamia kwenye mfumo wa mtandao katika kuhifadhi vitu na ufanyaji kazi zao .

  Mimi ni mmoja wa watu hao sitembei na vitu vyangu ninavyofanyia kazi nimepoingia kwenye sehemu inayotoa huduma ya mawasiliano ya mtandao Internet Café basi natembelea tovuti ambayo nimehifadhi vitu vyangu na kuanza kufanyia kazi toka huko huko na nikitaka kazi hizo wengi waweze kuziona nawaalika wanaweza kuangalia bila kufanya hujuma yoyote .

  Kwa miaka michache iliyopita tumekuwa kwenye mradi ambao unahusisha nchi 3 za afrika mashariki safari za kwenda kwenye baadhi ya maeneo ni ndefu na gharama sana mfumo huu wa mawasiliano umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kurahisisha mradi huu kuna watu ninafanya nao kazi sina haja ya kujuana nao wale kukutana nao ni wao kutembelea mtandao wetu na kufanya shuguli zao tu zinazowahusu .

  Ukija kwenye Serikali zetu na Taasisi zingine zinazohudumia idadi kubwa ya watu au zilizokuwa na wafanyakazi wanaosafiri mara kwa mara sasa hawana haja ya kusafiri na rudi na vitu na vifaa vya kufanyia kazi mfumo huu utamwezesha kufanya kazi akiwa popote pale ambapo kuna huduma ya mtandao .

  Kuna baadhi ya serikali Duniani zimetumia mfumo huu kwa kipindi kidogo na zingine kidogo kidogo zinaendelea lakini hizo serikali zilizoamua kungia kwenye mfumo huu zinapata upinzani wa baadhi ya vitu kwa mfano masuala ya leseni ya programu wanazotumia wafanyakazi wao na sheria zingine za hati miliki ya programu na mali zingine zinazotumika kwenye mfumo huu na pia baadhi ya wafanyazi na wadau wengine wanahofia siri na taarifa zao zingine kuvuja kwa urahisi kutokana na mfumo wake wa ulinzi .

  Mfano kuna watu Wanaosema kwamba Taarifa zingine zinafaa zaidi kuhifadhiwa sehemu moja tu bila kuunganishwa na sehemu zingine mfano taarifa za wateja , wagonjwa na nyingine nyingi zinazohusu watu hata hivyo kuna mkakati unaofanywa kwa pamoja kati ya kampuni za Google, Microsoft, AT&T, Salesforce.com na taasisi zingine za kiraia ili kuja na sera nzuri na bora za usalama wa masuala ya kiteknohama hii ni kwa marekani hata hivyo nchi nyingi zina masuala yake ya utamaduni na mengine ya ndani ambapo sheria hizo zinaweza kuwa ngumu kwao .

  Hapa nchini kwetu pia mwaka huu tumekuwa na sheria ndogo za masuala ya kielektroniki sina uhakika kama sheria hii imegusia masuala ya mfumo huu indepo moja ya shirika au taasisi za serikali ukaamua kuutumia kikamilifu zaidi .

  Pamoja na vikwazo vidogo ambavyo vinatokea hapa na pale mfumo huu wa mawasiliano kwa njia ya mtandao naamini unaweza sana kuzifaa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kupanua shuguli zao mbalimbali kwenye jamii zao na kupunguza kwa asilimia kubwa gharama mbalimbali ambazo jamii zinatumia kwa ajili ya usafiri , ununuzi na masuala mengine yanayohusiana na teknohama .

  Na ule utamaduni wetu wa kuiba leseni na kudanganya baadhi ya takwimu kwenye masuala ya teknohama nadhani unaweza kuwa historia mfumo huu ukiweza kukubalika na kufanyiwa kazi ipasavyo kwa kutumia sheria tulizonazo au za kimataifa .

  Unaweza kusoma makala zifuatazo kwa ajili ya kujifunza zaidi na kuna vyuo vingine na taasisi ambazo zimeamua kufanya utafiti zaidi kuhusu suala hili

  [FONT=&quot]Hart, Kim, “Google Goes to Washington, Gearing Up to put Its Stamp on Government”, Washington Post, September 29, 2008. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  Helft, Miguel, “Technology Coalition Seeks Stronger Privacy Laws”, New York Times, March 30, 2010.

  [FONT=&quot]Lewin, Katie, “Federal Cloud Computing Initiative Overview”, June 18, 2009. [/FONT]
  Lohr, Steve, “When Cloud Computing Doesn’t Make Sense”, New York Times, April 15, 2009.

  Distinguishing Cloud Computing from Utility Computing - SaaS Week
  Cloud computing: Clash of the clouds | The Economist
  The Technium: A Cloudbook for the Cloud
  www.Apps.gov
   
Loading...