ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Taarifa Juu ya Hoja za Ukaguzi kuhusu Hesabu za Fedha za ACT Wazalendo Kutokana na Taarifa ya CAG ya mwaka unaoishia June 2016
Tumesoma Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu hoja za ukaguzi wa Chama cha ACT Wazalendo za mwaka 2014/15. Tunapenda kuwajulisha wanachama wetu kuwa hoja hizi za CAG ni za hesabu za mwaka 2014/15 na sio hoja za Sasa za 2015/16. Ukaguzi wa mwaka 2015/16 bado.
Hoja hizi zote zilizoibuliwa na CAG tulizijibu pamoja na kuwasilisha hesabu za mwaka 2015/16 kwaajili ya Ukaguzi. Kama kawaida yetu, tutaweka Taarifa hii ya 2014/15 ya ukaguzi pamoja na majibu yetu wazi kwenye tovuti ya Chama siku ya Jumatano tarehe 19 Aprili, 2017, ambao pia Kamati ya Fedha itatoa maelezo kwa wanachama wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa ujumla juu ya Masuala kadhaa yaliyoibuliwa katika ripoti ya CAG kwa hesabu za mwaka 2014/15.
Venance Msebo
Mwenyekiti Kamati ya Fedha - ACT Wazalendo
April 15, 2017