Wakuu muziki wa taarabu umeanza kuelekea pabaya zaidi tofauti na mwanzo ilianza taarab asilia ikaja #modern#taarab na sasa ni #modern#taradance.
Muziki umegeuka vijembe,matusi ya live yaso na mfano angalau hata mwanzo walikuwa wakitumia lugha ya mafumbo, kiduku, kuvaa mavazi ya ajabu nayo yameikumba taarab imekuwa ni vurugu tosha muziki huu umegeuzwa dance na rhumba utunzi mbovu wa mashair usiozingatia mizani wala vina kibaya zaidi juzi kati wakati wa tuzo za KTMA/Kill Music Award walishangaza Tanzania kwa kitendo cha kusikitisha cha kuutaja wimbo wa rhumba alioimba isha mashauz kuwa eti ndo wimbo bora wa taarab.
Wimbo huo unaitwa #mapenzi#hayana#dhamana ni wimbo wa rhumba ulioingza kwenye taarab kuwa eti ndo wimbo bora, hii imeleta manung'uniko makubwa kuuweka wimbo ambao una mashair mabovu kuwa ndo wimbo bora.
Hizi #modern#taradance zitatupeleka pabaya, nini kifanyike kuikoa taarab?
Taarab ilikuwa enzi za JKT ya kina marehemu Issa Matona (Kimasomaso), Patricia Hillary (njiwa), bila kuwasahau kina Shakila (macho yanacheka moyo unalia)... Siku hizi ni vurugu mechi tupu!
Huo wimbo aloimba isha unaoitwa wimbo bora wa taarab ukiusklza utabak ukicheka ktk taarab haujawah kushuhudiwa wimbo wa ajab hvyo ingia Tubidy Mobile Video Search Engine then kwenye search andika isha mapenzi hayana dhamana au angalia youtube kiukwel utabak kinywa wazi