Taaluma ya ualimu imepoteza hadhi katika jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taaluma ya ualimu imepoteza hadhi katika jamii

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kilimasera, Apr 26, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SIO siri kuwa hivi sasa, taaluma ya ualimu imepoteza hadhi katika jamii. Ile fahari ya kujiita ama kuitwa mwalimu kama ilivyokuwa zamani, sasa imepotea.

  Vijana wengi wanaukimbia ualimu kwa kile wanachodai kuwa haulipi kimaisha.Hata wazazi nyumbani, wanashtadi kuwaeleza watoto wao uzuri wa fani kama udaktari, uhasibu na nyinginezo, huku wakiusema vibaya ualimu.

  Ilivyo sasa, ualimu unaonekana kuwa taaluma kimbilio la watu waliopoteza matumaini ya kufanikiwa katika taaluma nyingine au wale wanaofeli katika mitihani. Hata fikra za wanajamii zimejengwa katika kuamini hili.

  Haya yananikumbusha kauli ya Ofisa Mchechemuaji wa sera katika asasi ya mtandao wa elimu Tanzania(TenMet), Florence Katabazi aliyewahi kusema kuwa katika hali hii si ajabu kuona kati ya walimu 10,000 ni 400 tu wenye sifa na haiba ya ualimu.

  Lakini kwa nini tumefika hapa? Wafuatiliaji wa masuala ya elimu wanaweza kuorodhesha lundo la sababu ikiwemo maslahi madogo wanayopata walimu.

  Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) ya mwaka 2009 inasema mwaka 1975, Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa kuwalipa mishahara mizuri walimu wake kuliko nchi kadhaa za Afrika Mashariki na Kusini ikifuatiwa na Burundi.

  Mwaka 2004, hali ikabadilika, mishahara ya walimu Tanzania ni midogo zaidi ikilinganishwa na mishahara ya walimu katika nchi kama Kenya, Msumbiji, Malawi na Rwanda.

  Kama haitoshi, walimu Tanzania wanalia kwa kufanya kazi katika mazingira duni, hawana vifaa stahiki huku mwajiri wao akishindwa kuwaendeleza kitaaluma. Haya yote yanachangia kupungua kwa hamasa ya watu kujiunga na taaluma ya ualimu, hivyo kukuza tatizo la uhaba wa walimu shuleni.

  Utafiti kuhusu walimu wanafunzi uliofanywa na Towse na wenzake mwaka 2007, unaonyesha asilimia 10 ya walimu wa kiume na asilimia 15 ya walimu wa kike walisema ualimu ndio uliokuwa chaguo lao la kwanza huku asilimia 37 wakisema waliamua kuwa walimu baada ya kupata alama za chini katika matokeo ya mitihani yao.

  Hivi ndivyo hali ya ualimu ilivyo nchini. Kumbe kuna watu walioingia katika kazi hii adhimu bila ya ridhaa ya nafsi zao. Kwa sura hii, si ajabu kuona ama kusikia madudu yanayofanywa na walimu wetu ambao kumbe moyoni hawautaki ualimu!

  Hata hivyo, tufanye nini kuleta nafuu katika taaluma hii? Kwanza serikali iimarishe Mkakati wa Maendeleo na Menejimentti ya ualimu(TDMS)ambao pamoja na mambo mengine unalenga kuondoa changamoto zinazowakabili walimu.

  Mdau wa Elimu Mbaraka Madenge, mkazi wa Mbezi Samaki jijini Dar es Salaam, anasema walimu pia wanatakiwa wapewe mafunzo kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia…… “Walimu wanatakiwa kupewa kipaumbele kwa kuwekewa kompyuta shuleni ili waweze kujifunza vitu vingi vya dunia ya leo.”

  Kwa upande wake, ripoti ya Unesco inashauri kuwa kuwepo kwa motisha maalumu kwa walimu wanaopangiwa kazi katika maeneo ya pembezoni.

  Mapendekezo mengine ni kupandishwa madaraja haraka, kupandishwa mishahara, kupewa posho ya usafiri na nyumba, kupewa nyumba, likizo maalumu ya masomo au fursa ya kupata mafunzo.

  Jambo jingine linaloweza kurejesha hadhi ya walimu ni pamoja na kupewa fursa ya kujiendeleza kitaaluma kama ilivyoelezwa katika ripoti. Hili litasaidia kupunguza utoro hasa baada ya walimu kunyimwa nafasi ya kusoma.

  Aidha, semina na mafunzo mbalimbali yaandaliwe ili kuwawezesha walimu kujua haki zao za msingi na kuzipigania pale inapotakiwa.

  Inatia moyo kusikia serikali imeridhia uanzishwaji wa Bodi ya Kitaaluma ya Walimu ambayo pamoja na mambo mengine itasimamia maadili ya ualimu.

  Nashauri chombo hiki kisiishie tu katika kudhibiti walimu, lakini kiwe chombo kitakachobadili taaluma ya ualimu kwa jumla na kutetea maslahi ya walimu ili ualimu nao ugeuke kuwa taaluma yenye hadhi katika jamii kama zilivyo taaluma nyingine.
  Furaha Maugo ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi 0765434357
   
 2. m

  mohamed ally Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakin mimi nadhan unajua kuwa wanaopelekwa kujifunza ualimu ni four wenye credit 2 au hata moja, Hi inamaanisha walimu hawajapewa nafasi nzuri kwanini wasichukuliwe wenye credit 3 na kuendelea?
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wenye credit 3 hawautaki ualimu na nchi ina tatizo kubwa la waalimu
   
 4. F

  Freeman Babu. New Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali ya sasa ya ualimu TZ+ Elimu ya kata Ni bomu linalosubiri kulipuka.
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  sio wote waliofeli ni walimu pia wengine tulisoma ualimu coz tuliupenda na tulichagua wenyewe BeD ila matatizo yaliyopo huku yamenifanya masters nafkiria kusoma kitu kingine kabisa mazingira ya kazi ni magumu hamna motisha mishahara midogo vitabu mzozo, madarasa mabovu vifaa vya maabara na maabara zenyewe hazipo syllabus haziendani na uhalisia wa ufundishaji wa somo yaani tabu tu. Tena sisi tuliotoka vyuoni hivi karibuni tunashindwa kudeliver what we were taught, tumejifunza kufundisha kwa njia ya participatory (modern teaching) ila sasa coz ya wingi wa watoto darasani hamna vifaa kazi inakua ngumu ndo maana samtym tunakaa ofsini kupiga story au wengne wanaenda ktk mishe zao
  serikali ingechukulia hili suala serious na kupandisha status ya ualimu means uwe ni profesion bila kuqualify hufundishi na tuwe na board yetu ka wahasibu, lawyers na engineers na mishahara iboreshwe things will change greatly na biashara ya private school itaisha since shule za kata zitweza kudeliver as expected
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kazi ipo yaani sekta hii matatizo lukuki na nadhani ndio sekta inayoongoza kwa kua na wafanyakazi wengi!
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  Point of correction ...Unaposema waliofeli unawalenga walimu wa ngazi ipi? hebu jaribu kuwa bayana kidogo,mie nakumbuka kuna watu wako vyuo vikuu wana div1/11 wengi sana,tena wamefaulu kuliko wanaosoma kozi zingine katika vyuo bnafsi, mfano mzuri hata sahvi fuatilia wale wanaosoma sheria,masscom,n.k pale Tumaini,Sauti,Mor U n.k alafu ulinganishe na wanaosoma Edctn pale Udsm

  mie nadhani kweli kabisa elimu ni ndogo kwa wale wenye ngazi ya vyeti na dipl lakini siyo wenye shahada,hii ni fallacy of generalisation

  tatizo la kushuka thamani ya ualimu inategemeana na uongozi wa juu wa nchi uliopo(rais) Nyerere alijua umuhimu wao tofauti na hawa marais wa leo,kwahyo hata leo akitokea rais fulani (Dr.Slaa) 'labda'anaweza kuregrade taaluma hiyo na zingne znazoendelea kupwaya kama eng,law,sociology etc

  tatizo jingne ni kuendelea kuiita taaluma hii eti ni kazi ya wito,this is an illusion,maana yake ni kwamba kijana wa leo in a capitalist world ambapo service out there demands capital (money),mfano kijana wa sahv analea familia baada ya mzazi kufa,anahitaji kuoa,anahitaji kula,kusomesha wadogo zake na wanae,anahitaji kujenga nyumba,kumiliki gari na mambo mengne,sasa kwa hali hii unawezaje eti unamwambia kijana afanye kwa wito ilohali hakuna wa kuja kumpa mahitaji yake bure

  hii dhana iliwezekana kipindi cha ujamaa maana bidhaa zilipatikana communally na pesa haikuwa na nafasi sana ila sahv huna hela huna maisha,serikali haitoi mishahara minono haina walimu...ama sivyo pimeni wenyewe
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  Unaposema waliofeli unawalenga walimu wa ngazi ipi? hebu jaribu kuwa bayana kidogo,mie nakumbuka kuna watu wako vyuo vikuu wana 1/11 wengi sana,tena wamefaulu kuliko wanaosoma kozi zingine katika vyuo bnafsi,mfano fuatilia wanaosoma sheria,masscom,n.k pale Tumaini,Sauti,Mor U n.k alafu ulinganishe na waliokwenda Ed pale Udsm

  mie nadhani elimu ni ndogo kwa wale wenye ngazi ya vyeti na dipl lakini siyo shahada,tatizo la kushuka thamani ya ualimu inategemeana na uongozi wa juu wa nchi uliopo(rais) Nyerere alijua umuhimu wao tofauti na hawa marais wa leo,kwahyo hata leo akitokea rais fulani (Dr.Slaa) 'labda'anaweza kuregrade taaluma hiyo na zingne znazoendelea kupwaya kama eng,law,sociology etc
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nashukuru sana kwa uchambuz wako,mim ni mwalim nimemaliza shahda yangu mwaka jana@udsm,na sidhan kama kujiunga na education eti ni kwa sababu ya low pass,nilipata daraja la kwanza,na nikapata B.A WITH EDUCATION,si kila anaekwenda ualim ni faikure,
  nikija suala la ajira,ni kweli mazingira ya kaz ni magumu na pia mishahara duni si serikalin si pruvate,lakin pia ni kweli jamii inauchukulia tofaut ualim kutokana na sera mbovu za serikali,nilikataa kwenda kufundsha kigoma nikaamua nibak mjin ili nijiendeleze kielim maana najua ualim hauna maslah unless uwe na mikakat mizur,
  jamii na serikal isiidharau hii taaluma,maana tutaishia pabaya sana,ila muimu ni kuiboresha ipasavyo,Ualim unaonekana ni vioja leo maana serikal imeona ni jalala la failures,ala!
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  labda wewe haupo katika sekta ya elim,BOMU LISHALIPUKA,lilipuke mara ngap?
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  asante sana mdau kwa kulifafanua hilo,mim nimesoma B.A ED,@UDSM,na walinidahili kwa kufaulu advance so mtoa mada aweke bayana hilo
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  asante mdau yanni,namkumbuka mhadhir wangu prof Njabir alikua akisistza kwel partipatory method,darasa langu lina wanafunz 120 ,sasa ntawamanage vipi?now selabasi mpya ya advance imetoka lakin vitabu hakuna na havijatungwa kabisaaa,mimi natumia google kuandaa notes,je huko kijijn ningeandaa vp?
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaa google kweli mkombozi wa waalimu!!!life imekua tight sana
   
 14. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Inauma sana, kuona hakuna anaejali. Walimu wakiomba kupandishwa mshahara wanatishiwa. CWT haina maana, kwa sababu haiwasaidii lolote!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  aaaah,halina siri hilo mdau google inanisadia sana nkinunu kifurush cha tigo nadeeeeessaaaa,nondo za kutosha nazmwaga darasan,maana hakuna bboooks
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli mkuu ila ungeweza kuna baadhi ya sites unaweza kudownload books ngoja nitakupa hizo adress ni pm e mail adress yako
   
 17. S

  Sebali Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ualimu ni taakuma nzuri tu kama taaluma nyingine. Ila kuna mangufu baadhi ambayo yanaifanya hii taaluma iangaliwe kwa mtazamo potofu.
   
Loading...