Kuhusu skills kulipa inahitaji uwe na uwezo wa kuitumia skils husika practically siyo chupri chupri, ukiwa smart itakulipa tu.
Binafsi Namshauri ajifunze Programming.
Aanze kujifunza Basic building blocks of website (HTML, CSS & JAVASCRIPT).
Akipata basic knowledge then anaweza kwenda deep zaidi na kujifunza Advanced JavaScript au kuchagua backend language Moja Python or Java akaongeza ujuzi.
Au anaweza kufocus na JavaScript tu zaidi na kujifunza jinsi ya kutumia NODE, then akawa JavaScript Fullstack Developer.
Akiweza kumaster hizo skills anauwezo wa kujiajiri kama Freelancer Software Developer au kuajiriwa kwenye makampumi kama Software Developer.
N:B
Inabidi awe mvumilivu na mtu mwenye kupenda kujifunza kila siku kwa kuwa Technology inabadilika na inakua kwa Kasi. Safari siyo nyepesi, inahitaji passion, but if you believe it , you can achieve it.