Princemwalejr
JF-Expert Member
- Nov 9, 2017
- 496
- 492
Miji ya nchi zilizoendelea ina polisi wa patrol za magari usiku. Mitaa ina kamera. Mitaa yao imepangika haina vichochoro na maficho. Watu wanafanya kazi usiku na kuchangamsha miji wakati wa usiku. Kukitokea tukio kuita polisi, zimamoto au ambulensi ni dakika sifuri. Wakazi wanajilinda kwa silaha za moto majumbani mwao.
Pamoja na hayo yote wenzetu mitaa yao ina taa za barabarani na mitaani zinazotoa mwanga unaofanya usiku uwe mweupe karibu na mchana.
Kufupisha habari hali ya kwetu ni kinyume cha hivyo. Usiku ni giza totoro!
Taa za barazani husaidia lakini kwenye maeneo mengine inabidi uzifungie ndani ya waya za chuma na magrili kuepuka vibaka wa balbu au jirani wanaopenda giza mitaani.
Napendekeza madiwani, halmashauri, serikali za mitaa mpaka mikoani wapitishe kampeni ya kupambana na giza mitaani usiku.
Kila mtaa uwe na taa angalau mbili ndefu kama za uwanja wa taifa. Hii ikimaanisha ni vibaka wenye uzoefu wa kukwea minazi tu ndio wataoweza kuiba taa hizo.
Na balbu zake ziwe na mwanga mkali kama zile za Namanga mpakani.
Hapo ukabaji wa usiku na hofu ya kutembea usiku mitaani itapungua kwa asilimia hamsini.