Kitia
JF-Expert Member
- Dec 2, 2006
- 418
- 74
Kuna hii ya Solar ambayo nimeifanyia utafiti kwa muda wa mwaka mmoja na nimethibitisha kuwa hii taa ni madhubuti na inakidhi sifa ambazo watengenezaji wake wamezipa.
Hii taa ni taa ndogo, mbadala wa kibatari. Ukichaji siku moja unaweza kutumia kwa siku 5 ndipo inafifia na kuzima kabisa. Kwa maeneo yetu ya Tanzania yenye mwanga wa jua mkali ni dhahiri kwamba utakuwa na taa ya uhakikamuda wote.
Taa yenyewe inatumia mwanga wa jua kuchaji betri tatu za AA za kuchaji, ambazo uhai wake ni miaka mitatu ndipo utabidi uzibadilishe uziweke mpya.
Kwa hesabu za haraka haraka taa hii inaleta unafuu wa gharama ukilinganisha na bei ya mafuta ya taa utakayonunua kwa miaka mitatu. Kama nilivyosema taa hizi ni mbadala wa kibatari, na hata pale umeme unapokatika, kuwa nayo kwenye gari au hata ukisafiri.
Taa hizo na bei yake moja ni Tshs. 30,000. Nipo katika matayarisho ya kufungua sehemu ya mauzo Dar es salaam kwa hiyo atakayetaka habari zaidi anitumie PM na pia soma habari zaidi hapa: