T.I.D Kumburuza Steve Nyerere mahakamani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
tid2.jpg

Msanii wa bongo fleva Khalid Mohamed 'T.I.D' ameahidi kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaosambaza taarifa kuwa amepewa pesa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kama kivuli katika sekeseke la kutaja majina ya wanaohusika na dawa za kulevya.

Akizungumzia ishu hiyo, TID amesema, yeye alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na serikali ilimkamata kwa kosa la kutumia lakini ikaamua kumsaidia kwa kumfanya aachane na dawa hizo pamoja na kumpa nafasi ya kuelimisha vijana wenzake ambao bado wapo katika janga hilo.

TID ameonesha kushangazwa na kuumizwa na taarifa zinazoenea kuwa amepewa pesa ili ataje watu au ajitangaze, jambo ambalo amesema ni wivu wa baadhi ya watu wasiomtakia mema, na wanaotaka kumuona akiendela kutaabika kwenye matumizi ya dawa hizo.

"Watu wana ushahidi gani kama mimi Mh. Makonda kanipa mimi pesa au wanazungumza tu? mimi nataka huyo sijui Steve nani nani.....aseme kwamba aliniona nikipatiwa hizo pesa bila hivyo mimi nitamshtaki, unaituhumu serikali, bila ushahidi, hili ni kosa ambalo naweza nikampeleka mtu mahakamani" Amesema TID

Alipoulizwa kama sasa atakwenda mahakani, TID alijibu

"Ndiyo nitakwenda Mahakamani..."

Msanii anayedaiwa kutoa kauli hiyo ya TID kupewa pesa ni Steve Nyerere, kupitia sauti za simu zilizosambazwa tangu juzi, zikionesha mtu anayedhaniwa kuwa ni Steve Nyerere akiongea na mtu anayedhaniwa kuwa ni Mama wa Msanii Wema Sepetu.

Pia aliwajibu wanaodai kuwa amewageka "Unasema mimi nimekusnitch wakati wote tulikuwa ndani, nilipokuwa chini mbona ulikuwa unafurahi saivi nimetoka unasema nakusnitch?". Amehoji TID

Pamoja na hayo TID ameongeza kuwa yeye kutajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kufikishwa kituo cha polisi kumemuongezea mashabiki zaidi na kumfanya awe maarufu zaidi kutokana na simu za pole kutoka kwa mashabiki na wanahabari kuwa nyingi, pia kuandikwa na kuzungumzwa kwenye vyombo vyote vya habari.

Source: Eatv
 
T.I.D njaa imekuponza na ndiyo maana sasa unaishi kwa Kujipendekeza huku ukitumika kama Condom vile. Kwa nimjuavyo Steve Nyerere wala hajaongopa na kanyoosha vizuri mno maneno / maelezo yake. Halafu unajiita Mnyama wakati Mimi nakuona Bata tu!
 
Mteja kadata na alosto...anadhan kwenda mahakamannni kama kwenda kwa pusha sio!,dogo alitamba sana enzi hizo akiwa zeze lake sasa hivi hamna kitu kawa mtu wa ku panick sana ndio maana billnas alimwona chenga akamkimbia!
 
Back
Top Bottom