System of US Presidential Elections | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

System of US Presidential Elections

Discussion in 'International Forum' started by Teye, Oct 28, 2012.

 1. T

  Teye Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanajamii ,naomba shule ya system ya uchaguzi wa US Presidential Elections.specifically kuhusu swing states,early voting,Electoral college.

  Nawasilisha!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nitakumegea kiduchu tu. Marekani ni nchi iliyogawanyika kiitikadi, kiutamaduni na kisiasa vile vile. Kuna majimbo ambayo daima yanapiga kura Republican, kama vile Kansas, Missouri, Nebraska, na kuna majimbo ambayo daima yanapiga kura Democratic, kama vile New York, California, Connecticutt, etc. Sasa swing states ni majmbo ambayo yanapiga kura kufuatana na ushabiki wa mgombea, anaweza kuwa Republican au Democrat, lakini amewakonga nyoyo wapiga kura katika majimbo hayo. Kwa mwaka huu hayo ni pamoja na Colorado, Ohio, Virginia, ambalo kwa muda mrefu lilikuwa Republican, Florida, Wisconsin, Minnesota na New Hampshire. Huko ndiko kura zinapogombaniwa hivi sasa kuelekea uchaguzi wa wiki ijayo na ndio maana unaona Romney na timu yake na Obama na timu yake wanazungukia hayo majimbo kwa sababu wanajua katika yale majimbo mengine wanaongoza kwenye kura ya maoni.
  Early voting ni ruhusa ya kupiga kura mapema kabla ya siku ya uchaguzi, ambayo kwa mujibu wa katiba ni lazima iwe jumanne ya kwanza ya mwezi Novemba. Majimbo kadha wa kadhaa huruhusu early voting ili kupunguza msongamano siku ya upigaji kura. Kuhusu electoral college ni idadi ya kura alizopata mgombea kutokana na ushindi wa jimbo kwa jimbo. Kila jimbo lina idadi yake ya electoral votes kutokana na idadi ya watu. Kwa kifupi ni hivyo.
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hili la early voting likija TZ ndo kwisha habari yake, tutapewa matokeo yaliyochakachuliwa mpaka yakachacha maana nani mwenye uwezo wa kulinda kura zake muda wa let say two weeks.Mafisadi wote watashinda
   
 4. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  Electoral coolege ni mfumo wa upigaji kura ambao umebuniwa ili kuleta usawa katika kila jimbo kutokana na idadi ya watu.
  kwa ujumla kuna electoral vote 538 ambapo zimegawanywa kwa kila state kutokana na idadi ya watu pamoja na congressmen.
  [​IMG]

  Kwa hivyo kwa mfano Michigan kuna electoral vote 16 hivyo kila mgombea anatoa majina 16 ya wapiga kura wake. Hivyo ikiwa mgombea ameshinda katika popular vote basi anapata kura zote 16 za electoral. Vivyo katika majimbo mengine isipokuwa Nebraska na Maine ambapo electoral vote hugawanywa kutokana na wilaya mgombea alizoshinda na sio kura zote za jimbo kwenda mgombea alieshinda popular vote bali ni ki-wilaya.

  Ili mgombea ashinde inabidi apate angalau electoral vote 270. Kutokana na mfumo huu baadhi ya majimbo ni muhimu kuliko mengine haya huitwa key state kutokana na uwingi wake wa electoral vote na hivyo wagombea hujitahidi kushinda haya majimbo ili ku-boost matokeo.

  Mjimbo kumi yenye kura nyingi;
  1. California 55
  3. Texas 34
  2. New York 31
  4. Florida 27
  5. Pennsylvania 21
  6. Illinois 21
  7. Ohio 20
  8. Michigan 17
  9. Georgia 15
  9. New Jersey 15
  10. North Carolina 15
   
 5. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Tungeomba system hii ije bongo!!! maana .......
   
 6. T

  Teye Member

  #6
  Nov 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jasusi na wengine ahsanteni kwa ufafanuzi.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  Itatuvurugaa sanaa na chama fulani kitadumu milele maana watachakachua hadi basi....na wengine hawatapata hata ubunge ...hatujafikia level hiyo ya demokrasia ya wamerekani,acha tupambane utaratibu wetu hovyo wa daftari la usanii la kura
   
 8. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,287
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  early voting ikija Bongo naona itapunguza uchakachuaji sababu kura kila siku zinahesabiwa n amgombea /wagombea wanajijua wamesimmamia wapi na siku ya mwisoi ni finalization tu.
   
Loading...