Syria yaiambia Ufaransa: "Hatuna haja nanyi waungaji mkono wa magaidi"

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Syria yaiambia Ufaransa: "Hatuna haja nanyi waungaji mkono wa magaidi"
Jan 29, 2019 03:17 UTC
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria jana usiku ilijibu matamshi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliyelalamika kwamba Damascus haioneshi ishara yoyote ya kufanya mazungumzo ya kisiasa na nchi yake na kuongeza kuwa, Syria haina haja na tawala kama za Ufaransa zinazounga mkono vitendo vya kigaidi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa tamko rasmi na kusema kuwa, misimamo ya Emmanuel Macron iliyo dhidi ya serikali ya Damascus imeshindwa kikamilifu na hilo linaonesha kufeli njama za Paris dhidi ya wananchi wa Syria.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, rais wa Ufaransa hivi sasa anajaribu kujisafisha na damu ya wananchi wa Syria iliyomwagwa kidhulma na magaidi wanaoungwa mkono na madola ya Magharibi ikiwemo Ufaransa, lakini serikali ya Damascus haina haja na watu ambao mikono yao imejaa damu ya wananchi wa Syria.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari na mwenyeji wake Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri mjini Cairo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jana Jumatatu alilalamika kuwa, serikali ya Syria haioneshi hamu yoyote ya kufanya mazungumzo na Paris na kurejesha uhusiano na dola hilo la kikoloni la Ulaya.
Katika siku za hivi karibuni nchi nyingi za Kiarabu zikiwemo za Umoja wa Falme za Kiarabu, Morocco, Jordan, Sudan na Mauritania zimekuwa zikipigana vikumbo katika juhudi za kurejesha uhusiano wao na serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria.
 
Nosooner or later magaidi wanaoita wenzao magaidi watajulikana tu

"ᵀʰᵉ ᶠⁱʳˢᵗ ʳᵘˡᵉ ᵒᶠ ʷᵃʳ ᵃⁿᵈ ᵇᵘˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱˢ ᵗᵒ ᵏⁿᵒʷ ʸᵒᵘʳ ᵉⁿᵉᵐʸ"
 
Back
Top Bottom