client
JF-Expert Member
- Dec 13, 2015
- 671
- 884
KIUNGA cha mwisho mashariki mwa mji wa Aleppo kinaelekea kuanguka kwa majeshi ya dikteta, umwagaji mkubwa wa damu kuelekea mwisho wa vita ya miaka minne kwa ajili ya kuuteka mji huo.
Wakati majeshi ya serikali yakikamata maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na waasi, wanashutumiwa kuwaua watu wanaowahisi kuwa na mahusiano na makundi ya waasi. Wafanyakazi wa kujitolea huko Aleppo walitoa maombi ya msaada.
Ndugu wa kundi la waasi la Free Syrian Army, wakiwemo wanawake na watoto, ni miongoni mwa wale waliouawa, mwanaharakati Mohammad Basbous wa Aleppo Media Center aliliambia shirika la habari la Marekani la CNN leo. ”Kila saa, mauaji yanafanyika,” kundi la kutetea haki za binadamu nchini humo lilisema, na kuongeza kuwa ushahidi kwa taarifa za hapo awali kutoka kwa Umoja wa Mataifa juu ya maovu dhidi ya idadi kubwa ya raia.
Taarifa zimekuuja wakati askari wa Syria wanakamata viunga mashariki mwa Aleppo katika kile kinachoonekana kama maeneo ya mwisho ambayo waasi wanaweza kupambana na serikali. CNN bado haijaweza kuthibitisha juu ya kutokea kwa mauaji hayo.
“Vijana hasa wanauawa,” alisema Ahmad Dbais, mkurugenzi wa hospitali za shirika la Union of Medical Care and Relief Organizations.
Waandishi: Raia wanafukunzwa majumbani kwao
Raia wenye uoga walikuwa wakilala mitaani baada ya askari wa Syria kuwafukuza katika nyumba zao, mkazi na mwandishi wa habari wa Aleppo Karam al Masri aliiambia CNN.
Mkazi mwingine alielezea hali katika mji huo kama ni sawa na mwisho wa dunia.
“Ni kama mwisho wa dunia huko Aleppo. Mabomu yanaruka juu ya vichwa vya raia. Watu wanakimbia lakini hawajui ni wapi pa kwenda.”
Wengi wanatoroka
Jeshi la Syria na washirika wake wamekuwa wakiingia katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa Aleppo katika siku za hivi karibuni, alisema afisa wa serikali ya Syria.
“Itakuwa ni hali ngumu sana kwa sababu hakuna sehemu ya kwenda kwa hawa wananchi wanaokimbia,” alisema Ismail Abdalla, mwanachama wa kundi la kutetea haki za raia la White Helmets.
Abdalla aliiambia CNN kwamba kiunga cha al-Fardous kimekamatwa na majeshi ya serikali, wakati maeneo machache bado yapo chini ya waasi.
Idadi kubwa ya raia inataarifiwa kwamba wanakimbia kiunga cha al-Sukkari baada ya eneo hilo kushambuliwa vikali. Kuondoka huko kwa raia kunaendana na kusonga mbele kwa majeshi ya serikali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alielezea kushtushwa kwake na taarifa za maovu dhidi ya idad kubwa ya raia wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto.