SYNOVATE kwafuka moto..................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SYNOVATE kwafuka moto.....................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tanzania Daima la leo linatuhabarisha ya kuwa SYNOVATE ambao wengi tunaamini ni magwiji wa kuchakachua matoeko ya kura za maoni ya Uraisi hawajawalipa wafanyakazi wao mishahara yao na haki zao nyingine za kimsingi................

  Yaani sasa zimwi la kuchakachua limewafikia hata makucha yao kwa kazi hiyo?

  Kwa maoni yangu SYNOVATE inabidi watueleze yale mabilioni waliyopewa na UNDP na taasisi nyingine kwa ajili ya kuboresha elimu ya uraia hapa nchini waliyapeleka wapi....................au hata hapa nchini hawakuzifikisha hayo mabilioni na yaliishia Kenya?

  Tunahitaji majibu haya kwani hakuna sababu nyingine ya kuelezea kwa nini wanataka kuchakachua mishahara ya wafanyakazi wao......................au wanataka kuwaadhibu kwa kuvujisha siri zao za uchakachuaji wa kura ya maoni ya Uraisi?.....................can someone in higher ranks there tell us something..........

  Synovate kwafuka moto


  na Ratifa Baranyikwa


  [​IMG] TAASISI ya Synovate, inayojishughulisha na masuala ya utafiti na masoko, imedaiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake. Wafanyakazi wanaoidai taasisi hiyo ni wale wanaofanya kazi kwa mkataba maalumu ambao ni takriban 126 na kiasi wanachodai ni karibu sh milioni 75.
  Akizungumza na gazeti hili jana mmoja wa watendaji wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wafanyakazi wanaodai ni wale waliokuwa wakiendesha tafiti za Synovate katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.
  Alisema utafiti waliokuwa wakiuendesha ni ule ambao Synovate iliingia mkataba na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu wafanyabiashara wa kati jinsi wanayoweza kuchangia pato la taifa.
  Mtoa taarifa wetu huyo alidai kuwa, Wizara ya Viwanda na Biashara ilikwishailipa fedha Synovate na kwamba wafanyakazi hao walikwishakamilisha kazi yao tangu mwezi Septemba mwaka huu.
  Kutokana na hilo, hivi majuzi wafanyakazi hao walikutana kwenye ofisi za Synovate na kufanya mkutano wakiomba kukutana na meneja wa taasisi hiyo kudai malipo yao, hali ambayo ilizusha mzozo mkubwa.
  Mzozo huo uliibuka baada ya meneja huyo wa Synovate tawi la Tanzania, Aggrey Owino, kutamka kuwa ofisi haina hela na kuwataka wafanyakazi hao wakubali kugawana kiasi cha sh milioni kumi zilizopo kwa kila mmoja kupata kiasi cha laki na nusu.
  Wafanyakazi hao ambao kila mmoja anadai kiwango chake kulingana na kazi aliyopangiwa, walikataa kugawana fedha hizo, kwa maelezo kuwa kiasi hicho ni kidogo kwani hakifiki hata nusu ya madai yao.
  Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wafanyakazi hao alisema kuwa kutaaa kwao fedha hizo kulimlazimu meneja huyo kuwalipa watu 16 tu madai yao yote badala ya kuwalipa wote kidogo kidogo.
  "Hivyo kiasi kulichobaki ambacho taasisi inadaiwa ni shilingi milioni 65 na sisi tumewaambia hatuwezi kukubali kulipwa kidogo, wakitaka watulipe zote ingawa meneja alitoa kauli ya kejeli kwamba ambaye hataki aondoke…lakini watu waligoma, " alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
  Wafanyakazi hao pia katika suala la kudai malipo wanasema hii si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kuwanyanyasa wafanyakazi wake.
  Gazeti hili lilipomtafuta Owino ofisini kwake kuzungumzia suala hili, mwandishi alielezwa kuwa hayuko nchini amekwenda kwao Kenya kwa ajili ya sikukuu za Krismasi.
  Taasisi ya Synovate ni moja kati ya taasisi ambazo zimekuwa zikiendesha tafiti mbalimbali hapa nchini.
  Moja ya tafiti ambazo zilizua maneno ni ule wa kura za maoni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ambapo utafiti wake ulionyesha kuwa mgombea wa urais wakati huo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, alikuwa anaongoza kwa asilimia 61.
  Wakati Dk. Willbrod Slaa aliambulia asilimia 16, Profesa Lipumba asilimia (5) na wagombea urais wengine asilimia 5.
   
 2. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama walitenda dhambi hii ya uchakachuaji, lazima iwatafune na watafunga ofsi warudi kwao narobi!
   
 3. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Maskini synovate. Ina maana jk hakuwapa fungu lao. Yaelekea waliingia gharama sana kupika matokeo ya kura za maoni
   
Loading...