Swine Flu na ajira zetu Buzwagi

Metallic

Member
Aug 14, 2009
57
6
Wakuu naomba msaada wenu wa kisheria uykoje kwenye hili la MAFUA YA NGURUWE ambayo yamevamia kazini kwetu Buzwagi Gold mine.
Uongozi ulitangaza kuzuia baadhi ya wafanyakazi (non essential employees)wasije kazini kwa lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa, lakini kwa sharti lakutokwenda mbali na makazi yao in case akihitajika apatikane kirahisi. Pia watalipwa mshahara kama yuko kazini as usual.

Upande wa pili wa shilingi uko hivi;
Wale (essential employees) kama walivyoitwa na uongozi wa mgodi watakuja kazini kama kawaida ila kama utajisikia hauko COMFORTABLE kufanya kazi katika mazingira haya( ya ugonjwa ambao WHO imeutangaza kuwa ni janga la dunia) utaruhusiwa kupumzika kama wale wengine (non essential employees) lakini hutalipwa mshahara kwa siku zote ambazo hutakuwepo kazini kwa kuhofia mafua ya nguruwe ambayo watu zaidi ya 24 wameshaambukizwa.

Je Kampuni inamtendea haki huyu mfanyakazi ambae anafanya kazi kwenye mazingira hatarishi kwa afya yake kwa kutomlipa risk allowance na kutokumpatia kinga ya ugonjwa (vaccine)zaidi ya kumpa hand sanitizer na mask???

Je ni haki kukataa kumlipa mshahara wake mtu ambae anajiona hawezi kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi, na kumlipa mwingine ambae kampuni imemwambia asije kazini kwa sababu zile zile??


Jamani naomba msaada wenu tafadhali ukizingatia hii ndo kampuni yenye kujali usalama kwa misemo mizuri kama;
  • Every body going home safely and healthly everyday.
  • No job is necessary to be done unsafe., etc
Na je hili la kufanyishwa kazi kwenye mazingira yenye SWINE FLU likoje??wakati tunaenda majumbani kwetu jioni kukutana na jamii hasa familia zetu??:confused:.
 
Back
Top Bottom