ofcourse kufanya ivo si mpaka kuwe na sababu ambayo ndo mm siioni,au unaweza ukaamua kupiga beat tu mkuu bila kua natatizomapenzi bhana lazima mgombane kidogo, umpige biti kadhaa ndo yananoga kinyume na hapo mtaboana kisha mtagombana ndo mapenzi yatanoga tena, mzunguko ndo utakuwa hivyo yaani
...kinachosaidia msigombane mara kwa mara ni huo umbali mliopo,km ulivyosema mara ya mwisho mligombana sababu alichelewa kurudi,mara nyingi kuwa karibu na mtu, kunaongeza mawasiliano ya ana kwa ana,na hapo ndipo chances za kugombana/kwaruzana zinapoongezeka,ila km mko mbali, sio rahisi sn kugombana!
Kupigana iwe kwa ngumi ama maneno lazima kuwepo katika mahusiano. Mapacha wanagombana sembuse ninyi mlio lelewa tofauti!!!!??
Tena mkichukua muda mrefu bila kukwazana ama kupigana siku ikija kutokea basi mwanaume utamwagiwa maji moto, utakatwa uume, n.k, na mwamke utapigwa na kuburuzwa kama mzoga na kutupiwa vitu vyako nje.
Si ajabu! kipindi tuko mbalimbali hata mwaka unaisha hamjakwaruzana.
Na hata tukiwa karibu hukaa muda mrefu bia ugomvi.
Kwa miaka kumi hatujawahi kumaliza siku nzima bila kupatana. Mara zote mmoja ataanzisha mazungumzo ya mapatano.
Yaani uzoefu wangu na baba yangu ni kinyume kabisa na mume wangu na kipindi cha utoto nilidhani wanaume wote ni wakorofi, wakali kama baba yangu.
Sio kwamba mume ni mpole sana, ila inatokea tu. Mara nyingine anagombana na ndugu zake hadi huwa namshangaa.
Ila mi ugomvi ndo siwezi. Ukiniuzi ntalia halafu ntasamehe. Na sio goog girl kihivyo.
Inawezekana ikawa kwenu pia. Kuna wengine nawafahamu nao hawana hulka ya ugomvi.