TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,514
- 11,276
Hili swali nimelikuta kwenye Blog ya Dina Marios.
Mtazamo wangu:
Hili suala linawezekana, unapokuwa na mwanamke na mkawa mnaendana vyema kwa maana ya kuishi kwa amani na upendo wa kweli, akili inapata kutulia (stress free) na hatimaye, mtu kuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi sahihi hata kwenye shughuli anazokuwa anafanya. Ikiwa ni kinyume, basi mtu atashindwa ku-concentrate kwenye mambo yake kutokana na muda mwingi kuwaza migogoro yake na mpenziwe au migogoro yake binafsi (intrapersonal conflicts) kuhusu mpenziwe, hali itakayopelekea mtu huyo kufanya vibaya kwenye shughuli zake.
Leo kwenye kipindi tulikuwa na ishu moja ambayo ilipelekea kutokee mjadala ufuatao.Hivi ni kweli kuna wanawake wanakuwa na kismati flani hivi,pindi anapokuwa na mwanaume kimapenzi yule mwanaume hufanikiwa??yaani madili yake,mambo yake yote ya kipesa yanamwendea vyema akiwa na mwanamke huyo tu.Akiachana nae basi mambo yanakwenda mrama!!!!pls wanaume naomba mnisaidie kujua hili kama kweli lipo.
Asante!!!!!