Swali: Wahindi wamesaidia kupandisha uchumi wa Tanzania au kuua?

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Wana jamii kwanza nianze kwa kuomba samahani sina maana kuleta therad ya kubagua ndg zetu wenye asili ya asia hasa wahindi, lakini nataka tuweze kutambua na kuheshimu mchango wao katika uchumi wa nchi yetu, naomba tujadiri hili swala kwa kina kidogo kwa kuweka mifano.

1. KUCHANGIA UCHUMI:
Hakuna ubishi wahindi ndio wanashikilia uchumi wa Tanzania ukiangalia makampuni na viwanda vingi ni vya wahindi, kila kiwanda kimetoa ajira nyingi kwa watanzania, ukienda mikocheni industrial area, Nyerere Road na nk mida ya jioni na asubuhi utaona ninachongea, siwezi kuvitaja viwanda ni vingi sana, kuna viwanda vimeajiri watanzania mpaka 500 au zaidi. pia hulipa kodi kwa serikali kama VAT, CORPORATE TAX, INCOME TAX, P.A.YE. na NK.

Ukweli watanzania wengi hukimbilia kutafuta ajira hata akimaliza elimu ya chuo kikuu, ni wachache sana wenye maono ya kuwekeza au kufanya biashara ili atengneze ajira. Mfano, kuna kijana mwenye asili ya kihindi, lkn maisha yao ni ya kawaida sana, alifanikiwa kusoma degree ya uhasibu, baada ya kumaliza aliajiriwa kwenye makampuni kama miaka 4 hivi baada ya hapo alianzisha kampuni ya ku print, siwezi kuitaja hapa, kwa sasa ameajiri vijana wa kitanzania na kihindi wasiozidi 10, sasa ni boss ana pesa nzuri na ana maisha mazuri.

2. KUANGUSHA UCHUMI:
Kama ilivyo kwa mfanya bishara yoyote, lengo ni kutumia firsa yoyote atakayoipata kutengeneza faida, mfanyabishara yoyote mwenye malengo, ukimpa upenyo lazima ukuumize, mfano mfanyabishara anayenunua mazao, hata kama soko la mchele ni zuri kiasi gani, anaweza kuwa anauza bei ya jumla kilo 5000/= lkn mwananchi akisema anauza kilo 300/= angependa apunguziwe hata hiyo 300/=,

Mfanyabiashara yoyote hapendi msamiati unaoitwa kodi, kwaani kwa liosoma biashara au finance management wanajua kodi siyo asset bali na liability. Liability ni moja ya risk katika uwekezaji hasa zikiwa juu. Hivyo basi serikali ikiwa lege lege wahindi huweza kutumia opportunity hiyo kutengeneza faida.

Wahindi ni wajanja sana kwenye deal, wanajua kula na taasisi za serikali, wanajua kutengeneza faida. wanajua kujiweka karibu na watawala hata vyama vya siasa, ndiyo maana wakati wa uchuguzi wahindi huwekeza kwenye uchaguzi ili asichauliwe mtu atakayeweza kuharibu mifumo yao, (the one who can spoil their network) ndiyo maana tuliona magunia ya pesa yakikamatwa kule Dodoma na baadae POLISI waka tangaza eti pesa zilikuwa zinaenda kununua alizeti. Hao ndiyo wahindi.

Kila deal kubwa lazima muster mind awe mhindi. angalia EPA, ESCROW ACCOUNT, RICHMOND, MEREMETA na madubwasha yote makubwa lazima wapo, angalia orodha ya wafanya biashara walioweka pesa nje ya nchi, ukianza na ile orodha ya ZITO waliweka pesa huko USWISI na visiwa vya Uingereza utawakuta ni wahindi, hata orodha ya juzi ya visiwa vya PANAMA watanzania wote waliotajwa ni wahindi,

Kitendo cha kuhamisha pesa kwenda nje ya nchi kuna shusha thamani ya pesa ya nchi, kwaani itabidi ile local currency inunue pesa ya nje km DORA ya marekani, pound na nk. pia hupunguza fursa za uwekezaji ndani ya nchi. Mfano hiyo mipesa iliyowekwa tu huko nje ingewekezwa hapa nchini tungekuwa na viwanda vingapi? watanzania wangepata ajira kiasi gani?

ADUI NI NANI KABLA YA KUWALAUMU WAHINDI:

Adui namba moja ni serikali yetu na adui namba mbili watanzania wenyewe, hebu JUMRISHA pesa za EPA, ECROW, RICHMOND, MEREMETA na PESA AMBAZO MAKAMPUNI YA MADINI YANATANGAZA KUPATA HASARA KILA MWAKA huku ukweli wanapata faida kubwa sana, hizo pesa zote zinaenda nje ya nchi. watu wachache ndani ya serikali wamefaidika na wengine wamekuwa wabia kwenye makampuni ya nje.

Haya yote yamekuwa yakifanyika watanzania tukiwa kimya, watu wachache sana hujitoa mhanga kupambana kwa niaba yetu, lkn shukrani yetu imekuwa na kuwapiga chini hata kugombea ubunge, mfano, DAVID KAFURILA alipambana kwa niaba ya watanzania mpaka baraza la mawaziri likavunjwa, viongozi wengi walifuzwa, lkn shukrani yetu watanzania ni kumnyima kura kuridi bungeni kuendelea kufichua uozo wa serikali.

Dr, Slaa alijitolea kupambana na serikali, ndiye alisababisha watanzania tukaijua EPA na RICHMOND, lkn CHADEMA walipomfanyia fitina baada watanzania wengi tulimwita msaliti. Zittoa Kabwe aliwahi kufungiwa kuhudhuria bunge kisa aliwambai watanzania kuhusu ufisadi wa BUZWAGI, lkn matokeo yake mawaziri kadhaa waliachishwa nafasi zao, nafikiri wengi mnamkumbuka Nazir Kalamagi aliyesafikiri kwenda LONDON kusaini mkataba hotelini kwa niaba ya serikali.

Watanzania wengi tulifurahia kufungiwa kwa ZZK na Mh Samwel Sitta spika wa bunge wkt ule. Watanzania ni mambumbu, tunajua kulalamika tu, lkn kazi hakuna. Ukipata kibarua ruhusa kila wiki, mara babu mgonjwa, mara jirani msiba huku siyo kweli, mara nimechoka, mara tunaonewa tugome, malalamiko hayaishi.
 
Kama unakampuni yako.. Ajiri Muhindi as Finance Manager. Yaani wanakila mbinu za kukwepa kodi. In ma opinion wamechuma kama watu wengine tu. Hivi NHC hakuna alietumbuliwa.
 
ogopa sana watu waliokaa kwenye jamii miaka zaidi ya 100 wametengemana na nyinyi wakawa wazalendo c kweli hata kdg leo wahindi wana miaka zaid ya 100 tanzania lakini bado wamejitenga na jamii yetu wanamashule yao wana mitaa yao wengi wanapassport mbili wakiwa wenyewe huwezi kuwakuta wakaongea kiswahili hata cku moja japo wengine hata india hawapajui hatuwaoni vijana wao wakienda JKT au police ila wanaonekana kwenye siasa tu na tumeshawapa jina la watanzania wenye asili ya asia ingawa wapo wengine hata kiswahili hawakijuh jambo la kujiuliza kwenye mashule yao wanatumia syllabus gani kama c kihindi??? wakat wa kampeni za uchaguzi niliwah kuona bango la mgombea wa ccm limeandikwa kihindi alikuwa mgombea wa udiwani kama ckosei pale kisutu
 
ogopa sana watu waliokaa kwenye jamii miaka zaidi ya 100 wametengemana na nyinyi wakawa wazalendo c kweli hata kdg leo wahindi wana miaka zaid ya 100 tanzania lakini bado wamejitenga na jamii yetu wanamashule yao wana mitaa yao wengi wanapassport mbili wakiwa wenyewe huwezi kuwakuta wakaongea kiswahili hata cku moja japo wengine hata india hawapajui hatuwaoni vijana wao wakienda JKT au police ila wanaonekana kwenye siasa tu

Kwa nini watanzania tusijifunze kutoka kwao kwa sababu miaka 100 inatosha kujifunza badala ya kuwalaumu tu, hakuna cha kujifunza? watanzania tunachangiana kwenye harusi na Misiba, lkn kama tungekuwa tunachangiana kwenye kutafuta mitaji, kilimo na nk, tungekuwa wapi? mfano kule kujijini kila nyumba kumi wangepangwa kwa siku kumi kulima shamba moja kwa siku, baada ya mwaka mmoja wangekuwa wapi? maana waliposhinda wanalima watu 10 ni zaidi ya eka moja. kwa hiyo kila familia ingekuwa na eka zaidi ya mbili za mazao ya chakula au biashara. lkn tangaza mchango wa harusi au send off, utaona ahadi kibao mara me laki moja, milioni na nk. magonjwa hakuna, jirani atakosa laki 2 za kwenda rufaa mhimbili subiri afe utaona hiyo michango, mara kiroba cha mchele, mara jeneza peke yake. wkt wahindi wana sacos zao kila mtu ana changia na baadae huwezeshwa na kusimamiwa baada anaendelea mwenyewe.
 
Kwani uchumi wa Tanzania ukoje?

Ndugu yangu Jingalao.
Uchumi wa Tanzania kiuhalisia haupo mikono mwa watanzania.
Kwa mfano katika fursa ya uwekezeji bado tunaendeleza siasa kupita kiasi ndio maana viongozi wachache na wageni wanafaidika.

Wazo la langu. Serikali ya sasa ingejikita kumpa matanzania kipaombele kwanza mgeni baadaye.

Wangetengeneza sera mbadala ambayo itawawezesha watanzania kufungua viwanda. Pia katika shuguli za kilimo, mifugo na Uvuvi bado serikali haijakuwa na nia ya dhati kabisa kubiresha uwezo wa wazawa.
 
uchumi wa nchi hii umeishatekwa na makanjibai kwa asilimia 100%
 
Zaidi ya 85% (maoni yangu) ya uchumi wa nchi upo mikononi mwa wahindi. Bahati mbaya sana, wahindi sio watu wa kuamini sana, uchumi wao hautusaidii hata kidogo coz wameushika wao, wanawekeza zaidi nje (Canada, India nk), hawajengi na kuongeza wigo wa ajira ndani ya nchi, hawajichanganyi kuonyesha sisi ni jamii moja....
Yapo mengi, ila kuwategemea wahindi kukuza uchumi ni kujidanganya.
 
mada nzuri
kama hatutajifunza mwaka 2025
njoo na thread "wachina wamesaidiaje uchumi" maana trend africa inaonyesha wachina wanafurika kwa kasi.
maendeleo huja kwa kutambua kosa na kujirekebisha fasta.
 
Mamlaka na nguvu za jamii yoyote zipo kwenye uchumi. Dola yenye msingi imara ni ile ambayo uchumi wake upo mikononi mwa raia wake.

Kama uchumi wa nchi unakuwa mikononi mwa wageni kwa asilimia kubwa, hata serikali huwaogopa wageni na maneno kama hawa wakiguswa nchi itayumba ni kawaida. Bila kujielewa kuanzia raia mpaka serikali waweza kuwa watumwa katika nchi yao.

Kinachotakiwa ni kwa serikali kuweka mikakati ya uhakika ya siri na ya wazi, kuhamisha uchumi kutoka kwa wageni kwenda kwa wenyeji. Hiyo ndiyo maana halisi ya uhuru.
 
Ni wakwepa kodi mahiri sana, hawalipi mafao ya wafanyakazi, wadhalilishaji wakubwa wa wafanyakazi wazalendo, wanalipa mishahara midogo sana, hawafuati sheria za kazi, wanahamisha pesa za kigeni, wanachuma hapa na kuhamishia kwao, ni vinara wa ghiliba na kuwarubuni kwa rushwa ndogo ndogo watumishi wa umma kupindisha sheria, kanuni na taratibu ili ziwanufaishe wao; kwa hiyo ukiyathamanisha yote hayo kwa pamoja net impact kwenye uchumi wetu ni NEGATIVE
 
Sasa kama haya yote tubayajua suruhisho ni nini? tuendelee kulalamika? lete pendekezo la kumaliza hilo tatizo.
 
Mamlaka na nguvu za jamii yoyote zipo kwenye uchumi. Dola yenye msingi imara ni ile ambayo uchumi wake upo mikononi mwa raia wake.
Kama uchumi wa nchi unakuwa mikononi mwa wageni kwa asilimia kubwa, hata serikali huwaogopa wageni na maneno kama hawa wakiguswa nchi itayumba ni kawaida. Bila kujielewa kuanzia raia mpaka serikali waweza kuwa watumwa katika nchi yao.
Kinachotakiwa ni kwa serikali kuweka mikakati ya uhakika ya siri na ya wazi, kuhamisha uchumi kutoka kwa wageni kwenda kwa wenyeji. Hiyo ndiyo maana halisi ya uhuru.

Ukweli wakiguswa kwa sasa uchumi utayumba, mfano ni sakata la sukari hivi karibuni. leo hii wakifungwa viwanda vyao na kuondoka mbona tutakoma, kwa sababu vinywaji vyote vinamilikiwa na wao, viwanda vya sabauni wanamiliki wao, viwanda vya nguo wanamiliki wao, viwanda vya madawa wanamiliki wao, bidhaa zote za nyumbani wanaingiza wao au ketengeneza wao, Tena sasa wana BOT yao pale POSTA jirani na ofisi za shirika la kazi duniani na Holiday Inn Hotel. BANK OF INDIA. sasa sijui inafanya kazi gani hapa nchini, maana sijawahi kuona mswahili akiweka pesa huko, kila anayeingia na kutoka ni mhindi. Bank nyingine wanayoitumia na BARODA, M-BANK, HABIB BANK, DIMOND. Huwezi kukuta mhindi ameweka pesa zake kwenye hizi bank za kibongo, yaani CRDB, NMB NA NBC labda kwa transaction ndogo ndogo.
 
Pendekezo la kumaliza lawama waindi wasifungua kampuni/ kiwanda/ Mashamba bila kuwa na shea ya mtanzania nhc iwe inawapangisha miaka miwili alafu waame mashule yao yalazimishe mchanganyiko tempo zote zichomekwe usalama wa tf
 
Kwa sasa tumechelewa inabidi tuanze kidogo kidogo kwa sababu waki sabotage tu tumekweisha, maana AGA KHAN HOSPITAL HAITOA HUDUMA, HINDU MANDAL, HAITATOA HUDUMA, SUKARI ITAKAUKA, NGANO ITAKUWA HAKUNA, MADAWA YATAKOSEKANA, SODA TUTAKOSA, NONDO NA VIFAA VYA UJENZI TUTAKOSA, kwa kifupi kwa sasa haitakiwi kukurupuka. twende nao taratibu tutaumia wameshika mpini sisi tumeshika makali. Wahindi ni wajanja sana huyo usalama wa taifa watamtambua tu, na wakisha mtambua atafunikwa na pesa hakukutakuwa na kitu tena. Kama waliweza kupenya mpaka kamati kuu ya CCM, na mpaka sasa wana influence nani awe Rais wa nchi wewe unafikiri hapo kuna usalama wa nchi tena?
 
Kwa nini watanzania tusijifunze kutoka kwao kwa sababu miaka 100 inatosha kujifunza badala ya kuwalaumu tu, hakuna cha kujifunza? watanzania tunachangiana kwenye harusi na Misiba, lkn kama tungekuwa tunachangiana kwenye kutafuta mitaji, kilimo na nk, tungekuwa wapi? mfano kule kujijini kila nyumba kumi wangepangwa kwa siku kumi kulima shamba moja kwa siku, baada ya mwaka mmoja wangekuwa wapi? maana waliposhinda wanalima watu 10 ni zaidi ya eka moja. kwa hiyo kila familia ingekuwa na eka zaidi ya mbili za mazao ya chakula au biashara. lkn tangaza mchango wa harusi au send off, utaona ahadi kibao mara me laki moja, milioni na nk. magonjwa hakuna, jirani atakosa laki 2 za kwenda rufaa mhimbili subiri afe utaona hiyo michango, mara kiroba cha mchele, mara jeneza peke yake. wkt wahindi wana sacos zao kila mtu ana changia na baadae huwezeshwa na kusimamiwa baada anaendelea mwenyewe.

umesema kweli kabisa! hii tabia ya michango ya harusi ni kero kweli kweli na ni lazima tubadilike!
 
Sasa kama haya yote tubayajua suruhisho ni nini? tuendelee kulalamika? lete pendekezo la kumaliza hilo tatizo.

Tumeshawasilisha kwa taasisi husika miaka mingi huko nyuma, tatizo lilikuwa ufuatiliaji wa 2 zilizopita ulikuwa dhaifu sana kwa sababu ni hao hao waliokuwa wamewekwa mifukoni! Ni matumaini yetu awamu ya tano itayafanyia kazi na wameshaanza kwa mfano, mikataba ya kazi inatolewa na mafao yanafuatiliwa, unyanyasaji wa wafanyakazi umedhibitiwa, kwa sababu sasa hivi ukitendewa ndivyo sivyo ukiripoti linafanyiwa kazi tofauti na huko nyuma, zkodi zinakusanywa, bureau de change zimepigwa kabali kutorosha fedha hovyo ni kugumu nk. Nk. Awamu ya 5 imeanza vizuri, tunaona mwelekeo mzuri, wakaze buti, viva JPM
 
Kwa sasa tumechelewa inabidi tuanze kidogo kidogo kwa sababu waki sabotage tu tumekweisha, maana AGA KHAN HOSPITAL HAITOA HUDUMA, HINDU MANDAL, HAITATOA HUDUMA, SUKARI ITAKAUKA, NGANO ITAKUWA HAKUNA, MADAWA YATAKOSEKANA, SODA TUTAKOSA, NONDO NA VIFAA VYA UJENZI TUTAKOSA, kwa kifupi kwa sasa haitakiwi kukurupuka. twende nao taratibu tutaumia wameshika mpini sisi tumeshika makali. Wahindi ni wajanja sana huyo usalama wa taifa watamtambua tu, na wakisha mtambua atafunikwa na pesa hakukutakuwa na kitu tena. Kama waliweza kupenya mpaka kamati kuu ya CCM, na mpaka sasa wana influence nani awe Rais wa nchi wewe unafikiri hapo kuna usalama wa nchi tena?

kikubwa ni kugundua! maana zamani tulikuwa kama vipofu..... sasa tumewashitukia...vita kwisha intime!
 
Back
Top Bottom