Stanley.
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 660
- 298
Katika hali isiyokuwa ya kawaida bunge la asubuhi limemaliza kwa mvutano mkali baada ya Kafulila kuomba muongozo juu ya ESCROW na wizi uliofanyika.
Ndipo AG alipoitwa kutoa maelezo kwanza, alianza kushambulia vielelezo vya Kafulila kuwa ni vipeperushi tu hali hiyo ilipelekea Mnyika kudai kuhusu utaratibu lakini mwenyekiti [Zungu] akampotezea.
AG aliendelea kuonyesha ubabe na kumtaka Kafulila wakutane nje kama anamambo mengne ila bungeni kunautaratibu wake [walikuwa wakimwingilia wakati anazungumza wakionesha kutokubaliana naye].
Akazidi kupandwa na hasira akamwambia Kafulila wewe ni sawa na tumbili hasiyeweza kuamua mambo ya msituni [Msemo wa kijaluo kwa mujibu wa AG].
Kelele zikazidi mwenyekiti amehairisha bunge amemtaka Kafulila na Mnyika wapeleke ushahidi wao juu ya Escrow kwa CAG na PCCB.
Nadhani jioni kutazuka miongozo tena!