swali/ msaada,, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

swali/ msaada,,

Discussion in 'JF Doctor' started by vox, May 14, 2010.

 1. vox

  vox New Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi ni kwanini kila KIZIWI lazima awe BUBU pia?ni maelezo gani ya scence yanayojaziliza THEORY hiyo,,naombeni mchango wenu.bless u
   
 2. E

  Exav Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kidogo ninachofahamu mimi ni kuwa, katika hatua mbalimbali za mtoto kukua, kuna wakati wa kujifunza kuongea. Hii hufanyika kupitia maneno anayosikia kila siku kwa watu walio karibu nae kama wazazi, ndugu n.k wanaomzunguka yeye. Ndiyo maana lugha ya kwanza atakayozungumza huyu mtoto ni ile inayozungumzwa na wazazi wake au niseme walezi wake na si vinginevyo. Kwa hiyo kama ni kiziwi kwa kuzaliwa hataweza kuongea hata akiwa mkubwa, labda tatizo hili liishe kisha asikie na kuanza kujifunza. Uwezo wa kusikia (unaweza kuwa na masikio lakini husikii - kiziwi) ni muhimu sana katika kujifunza vitu mbalimbali si kwa watoto tu hata kwa wakubwa pia.

  Hata hivyo, wenye ufahamu mzuri wa mambo haya ama baiolojia yake wanaweza kunisahihisha na kutuelimisha zaidi.

  Nawasalimu sana WanaJF wote na naomba kujiunga nanyi. Samahani kwa kutopitia kwenye jukwaa la utambulisho.
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kiziwi anakuwa bubu kwasababu hasikiii, angekuwa anasikia angekuwa na uwezo kujifunza lugha wanayoongea wenzao, sasa yeye hajawahi kusikia lugha yoyote, n hajui cha kuongea, ndo maana ataishia kusema baab baaa baa tu. kwahabari ya ulimi kuwa mzito, sijui inatokana na mazoezi akiwa mdogo, kwasababu kama angekuwa anasikia alipokuwa mdogo, angejifunza, tunawaona watoto wadogo ambao hawajaanza kuongea wanavyokuwa na ulimi mzito pia, hivyo kama hawatasikia lugha na kujifunza, basi watabaki hivyohivyo kama walivyokuwa watoto wadogo....huu ni ufahamu wangu ambao si wa kidaktari...madaktari walete majibu basi...
   
Loading...