Swali mipango miji: Mwenge ni Stand au Soko? (Picha)

kama ubungo ni hatari sana maana soko lipo high way hivyo gari likosea kidogo lazima lile vichwa ukiongeza na songas ndo balaa tupu selikari iko wap kwa haya mambo au wanasumbili ajali ndo wajue!
..Utakuta na STJ zinapaki kufanya manunuzi siju ndio nini?
 
mkuu napeleka masikitiko yangui makubwa kwa serikali ukiwa pale mida ya jioni atajionea watu wakiwa wananunua na kuuza vitu then kuna wale mabaunsa wanapita na kuchukua fedha kwa wale wanaouza vitu pale ukiwauliza fedha ni za nini wanakuambia ushuru na mbaya zaidi hawapewi risiti.
 
Jana nilikuwa nasikiliza Radio One toka mabandani mwa kuku nikasikia mjadala juu ya ufanyaji wa biashara kwenye vituo vya mabasi ya daladala (hususani Tegeta). Leo naona wengine wanataja Mwenge...na kesho utasikia wengine wakitaja Buguruni nk. Ukweli ni kuwa nchi yetu inaendeshwa kienyeji mno kiasi kwamba tukipata viongozi wanaoendesha mambo kisheria watapigwa mawe na kuambiwa ni wabaya. Vituo vya mabasi ni vituo vya mabasi full stop!

Halmashauri hazipendi kuwaudhi wapiga kura (kana kwamba na wao wanapigiwa kura). Ukweli ni kwamba tusipoachana na siasa za maji taka hatutafikia maendeleo tuyatakayo...tutabaki kulalama kila iitwapo leo kuhus mabo kadhaa yanayojitokeza. Iwapo si eneo la biashara na watu wakaonekana wanafanya biashara...sheria iachwe ichukue mkondo wake. Iwapo tutaendelea kuoneana aibu kuna watakaofaidika kwa kitambo tu lakini ukweli ni kuwa wengi wataathirika kwa muda mrefu.
 
Kama tunataka kuamini kuwa penye soko lazima stand, basi ubungo ndani ndo lingekuwa soku kuu Tanzania. Naona jiji letu linahitaji kufumuliwa na kufumwa upya. Kuanzia watendaji mpaka miundombinu.
 
Hivi umeshafika Ubungo ukapaona? Hiyo Mwenge cha mtoto mbona! Nadhani bado kidogo tu watafunga barabara.
 
Back
Top Bottom