Camp Gilgal
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,453
- 4,594
Mkuu tukumbuke pia karama za watumishi zinatofautiana, ndio maana utakuja kuona kuwa Mtu kama TB Joshua anatembelewa na watu wengi japokuwa wana madhehebu yao ili kupata suluhisho la kile wanachokitafuta ... Tunajua ana deal zaidi na Prophecy, sio ajabu walikwenda kutafuta unabii juu ya maisha yao ... Pengine ni kwa sababu may be alikosekana mtu wa kuwapa direction ktk madhehebu yao ... Nakumbuka ktk biblia watu wa kawaida, na hata wafalme wa kipagani walikwenda Samaria kutafuta UNABII kwa nabii Elisha ... Sio jambo geni km unapitia maandiko.Sijui kama Slaa anasali kwa Gwajima..nimeuliza baada ya kuona picha za Lowassa na Magufuli kwa TB Joshuahalafu tunaambiwa ni RC na Lutheran...nilifikiri ni walokole
Naomba tujihadhari na mihemko naomba kuuliza kuwa kujua tu niko curious.
Naomba wenye kukashifu mkae pembeni, lengo ni kuelimishana tu.
Swali langu ni hili;
Mtu anaweza kuwa mlokole na still Mkatoliki au Mlutheri?
Je, tunaweza sema mtu anasali kwa Gwajima au TB Joshua but still Mkatoliki au Mlutheri?
Je, Gwajima yeye binafsi anaweza kuwa Mkatoliki pia au Mlutheri?
Rafiki swali lako linatokana na watu wengi kutoelewa; kwanza nini maana ya neno "mlokole" hili neno haliko kwenye Biblia, asili yake ilikuwa kama neno la dharau kwa wakristo waliokuwa na ujasiri wa kukiri kwamba Yesu amewaokoa. na kama maana ya "ulokole" ndio hiyo basi kwenye madhehebu yote ya kikristo wapo! Wakatoliki wanaitwa Charismatic renewal, kwa walutheri na waprotestant wengine pia wapo, lakini kuna madhehebu mengine wanaitwa mainline pentecostals. ila kwa ufahamu wangu na uzoefu wangu watu wote hao niliowataja wakikutana mahali huwezi kuwatofautisha! Sasa hayo madhehebu yanayotutenganisha wakristo yana historia kutoka ulaya lakini kwa watu waliompokea Yesu kweli kweli huwa hawatofautiani kwenye mambo ya msingi yanayotufanya tuitwe wakristo waliompokea Yesu. I hope my little explanation has helped
My dear
Ulokole sio dini wala dhehebu.
Ni hali ambayo baadhi ya watu hujitangazia kuwa wako ktk hali tofauti ya kiimani kuliko wengine. If that is the case then hata mkatoliki au mlutheri anaweza kujiita mlokole. Waingereza wanawaterm as born again Christians. Who is not is the matter of debate.
Haya makanisa ya watu mara nyingi ni ministries yaani vituo vya huduma maalumu. Wengine inakuwa huduma ya kufunguliwa aka delivarence kama SCOAN.
Madhehebu mara nyingi yanakuwepo kila sehemu lkn ministries ndio utasikia kwa kakobe.
Kama hivyo ndivyo mkatoliki anaweza kwenda kwenye huduma say kwa mwakasege lkn kama ni jumapili basi anatakiwa aanze kushiriki misa kanisani kwake.
Nilishaenda kwa T.B Joshua, kwa Mwakasege, na huduma mbali mbali Emaus Catholic Charismatic Center
But i am sure ushakutana na walokole ambao sio RC wala lutheran
huduma zote kuanzia ndoa hadi msiba ni hapo hhapo kanisani kwao
na mtu akienda ku attend RC wanamzuia
Hizo ibada za huko hazitambuliki lakini pia hazijawekewa kipingamizi.So ni sawa kwa mkatoliki kuhudhuria ibada kwa Gwajima au TB Joshua?
na still akawa mkatoliki?
Umejibu kama nielewavyo mimi.
Nimeona si vyema nikusome alafu nisikusalimu.
Sijui kama Slaa anasali kwa Gwajima..
nimeuliza baada ya kuona picha za Lowassa na Magufuli kwa TB Joshua
halafu tunaambiwa ni RC na Lutheran...nilifikiri ni walokole
Ulokole sio dini wala dhehebu
Nashukuru kwa salamu, ama baada ya salamu; matikiti
Halafu hujanijibu unajua?
ishu mbili zile..
Sijui kama Slaa anasali kwa Gwajima..
nimeuliza baada ya kuona picha za Lowassa na Magufuli kwa TB Joshua
halafu tunaambiwa ni RC na Lutheran...nilifikiri ni walokole
Nijuavyo mimi, madhehebu yote ya kikristu, ukiondoa Roman Catholic, yanaitwa Protestants. Sasa Ukiwa Mkatoliki (kama mimi) hauwezi at the same time ukawa unaprotest against Catholic church, yaani a protestant. Sana sana utakuwa muhudhuriaji tu kwa upande mmojawapo. Hili jibu ni kwa mujibu wa mimi na linahusu Ukatoliki vs Ulokole. Kuhusu Ulokole vs other protestant churches watakuja wajibu wenyewe
Swala ni wenye 'MOYO SAFI' wala sio udhehebu. Ukimkiri na kumpokea kuwa bwana na mokozi wako(ukaacha njia zako mbaya) utakuwa umeokoka, tafuta penye mafundisho mazur go ahead
Kajamaa kanazunguuka, Swali lako ni Dk. Slaa kusali kwa Gwajima kunamuodolea ukatoliki wake?? Idiot
Makanisa yote ni biashara tu.
So ni sawa kwa mkatoliki kuhudhuria ibada kwa Gwajima au TB Joshua?
na still akawa mkatoliki?