Kwa kweli mimi nashindwa kabisa kuelewa pesa ina nafasi gani muhimu katika mapenzi ya kweli nadhani umuhimu wa pesa katika mahusiano ni mtu kutaka kwenda juu kwa kupitia mgongo wa mwenzie au woga wa kuishi maisha yasiyo ya pesa (kwa wale wenye pesa wanaotaka kupata wenye nazo wenzao tu) kwa mtazamo wangu mimi kuwa na pesa kunaweza kuwa mzigo tu kuliko hata kutokuwa nazo, nani ambaye anaweza akasimama akasema anapesa karidhika na kusema baaasi hizi zinatosha!!?
Binadamu anavyozipata pesa zaidi ndio anavyozihitaji zaidi na ndio anavyozitafuta zaidi
na pesa zinaweza kusababisha insecurity kwa aliyenazo zaidi hata ya asiyenazo
kwa sababu mwenye pesa anakuwa kwenye presha akifikiria na ku fanya kazi ya ziada ku zi keep, mambo yakiyumba kidogo utamwona atakavo panic kuzikumbatia hizo hela, aki lose hata kama ni kiasi kidogo tu inakuwa kaaazi kwelikweli hata kwenye utapeli/ufisadi/wizi/uchawi atageukia tu almradi angalau asirudi kwenye kupanda daladala
.
hata wenye utajiri mkubwa wanaodai wanausecurity ya kutosha kulinda mali zao bado hawapo excluded kwenye kufilisika na wanajua hilo na linawapa tumbo joto, ukiwaona outward utadhani wana raha sana, lakini ukiwa karibu nao mbona utajua mengi?
kama asiyenazo anakuwa kwenye presha akifikiria jinsi ya kuzipata na aliyenazo anakuwa kwenye presha ya kuzikeep na kupata zaidi ina maana fedha kama ilivyo haina msaada wowote kwenye mapenzi,
mie naona wawili wakipendana washirikiane, wasaidiane katika hali yoyote ile, watafute wote, waridhike na walichonacho (ni rahisi zaidi kuridhika kama huna pesa nyingi kuliko ukiwa nazo) maisha yakiwa ya dhiki au ya pesa (kuna waliolala matajiri wakaamka masikini na waliolala masikini wakaamka matajiri) washikamane pamoja wakati huo huo wa concentrate kwenye maswala yenye uzito ktk kuimarisha penzi lao