Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Ninaiheshimu sana kamati ya pili ya Magufuli kuhusu suala la makanikia, na mapendekezo waliyotoa.
Hata hivyo, nimesikia Kamati ya Magufuli wakisema Acasia haipo nchini kisheria, kwamba haijawahi kusajiriwa kama kampuni inayofanya biashara nchini Tanzania. Nina swali ambalo linalenga kupima umakini wa wasomi wetu katika kuchambua mambo. Lengo sio kukosoa kamati, lengo ni kuangalia umakini wetu katika kuchambua mambo.
Nakumbuka kwamba Acasia ni matokeo ya kubadili jina toka African Barrick Gold kuwa Acasia Gold. Sasa, hivi kutosajiriwa kwa Acasia ndio kosa lao au kosa ni kwamba African Barrick Gold walipobadili jina kuwa Acasia Gold hawakutoa taarifa kwa Msajiri wa Makampuni Tanzania? Hivi nikiwa na kampuni nikaibadili jina, nahitaji kufanya usajiri mpya kwa kutumia jina jipya la kampuni?
Je, ilibidi African Barrick Gold wafute usajiri wa mwanzo walipobadili jina, au watoe tu taarifa? Na kama ni usajiri mpya, haitamaanisha lesseni itabidi zitolewe upya? Kama Acasia haipo nchini kisheria, bado tunaitambua African Barrick Gold kuwa mmiliki wa hii migodi?
Wasiwasi wangu ni kwamba, pamoja na udanganyifu na dhambi zote za Acasia, kama kamati hii haijaliwakilisha suala la uwepo wa Acasia nchini inavyotakiwa, kuwa ni suala la kutokuwapo kwa taarifa kwamba African Barrick Gold imebadilisha jina, basi ukweli ni kwamba Tanzania tuna tatizo kubwa sana la wataalamu wetu kutokuwa makini katika mambo mengi, na jambo la kutisha na kisababshi kikubwa kuwa hata wale tunaowaamini wanashindwa kuona mapungufu katika mikataba ya kitaifa kwa kuwa hawako makini, vigilant, katika kutathmini (assess and review) mambo.