Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani?

Tanzania mpya yenye national spirit itapatikana kupitia Vita, cha kusikitisha ni kuwa Vita haitatokea sababu hao viongozi wenyewe hawapo tayari, maana ni wakati vita inaendelea huenda ukatokea uasi na vita nyingine ya ndani walengwa wakiwa ni wao na wote waliofaidika kupitia wao na mifumo yao mibovu waliyoiweka kwa makusudi.
Believe me, wanaimba ngonjera za vita lakini wao hawapo tayari kabisa, as you said si JWTZ pekee watakaopigana vita hii bali kila mtanzania kijana atahusika, hapo ndipo panawaumiza vichwa...maana kila penye keki ya taifa walitanguliza familia zao, marafiki, ndugu, mahawala mbele na maslahi binafsi yao binafsi....Je undhani watakuwa tayari kuwatanguliza mbele kwenda vitani?? Forget kabisa???
Nadhani turudi sasa kwenye ile mijadala mingine kama ile ya wanakamati wa kamati za bunge kujihusisha kuchukua rushwa n.k hili halijafika wala halitafika kwenye conclusions wanazoziimba....Malawi wenyewe mkononi wameshika Heligoland Treaty, wakati sisi tunahangaika kutafuta silaha zilipo...very funny.
 

Mkuu Mwanakijiji, nakubaliana na wewe kuwa vita wakati wowote ule ni mbaya kwa jamii.
Ni mbaya kwa elimu, mbaya kwa hospitali, mbaya kwa maendeleo, ni mbaya mbaya mbaya!

Lakini inabidi tujiulize kitu kimoja , mtu akikukalia utosini utamwacha kwa vile hupendi kupigana?
Uchezewe chezewe tu kwa vile we mpole na hutaki vita?

Gharama ya kudharauliwa ni mbaya zaidi kimataifa na inabidimajirani waelewe hivyo.
Tuna miaka mingi sana kuanzia Kenya,Uganda,Burundi,Congo,Zambia, hiyo Malawi na hata Msumbiji.

Hili swala la mpaka wa Malawi halikuanza leo, bali mara tu baada ya uhuru, na utata wake si mgeni.
Mwalimu alipeleka vikosi huko ku-assert position ya Tanzania miaka ya nyuma, na Malawi wanaliewa hilo.

Sitta, Membe na Lowassa wamefanya vema kuikumbusha Malawi kwamba Tanzania tupo na wasijichukulie sheria mkononi katika suala ambalo hatujakubaliana.

Kwamba Malawi wameuza vitalu vya ku explore mafuta/gesi katika sehemu ambayo ndiyo tunagombea ni dalili ya DHARAU.

Nchi haidharauliwi kirahisi namna hiyo.
 
Kingine kilichonitatiza mimi ni pale kila mtu alionekana kama vile ni AMIRI JESHI MKUU wa majeshi yetu:-
-Alianza Samwel Sitta alipokuwa akikaimu kama kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni;
-Akaja Membe, Waziri wa Mambo ya Nje;
-Lowasa ndiye akafunga kazi kabisa. Akasema Jeshi liko tayari kiakili, kivifaa,...
Hawa wote watatu ndio tunaoambiwa wanauwania huu uamirijeshi mwaka 2015. Wangesubiri waupate kwanza kuliko kumdhalilisha Amiri Jeshi Mkuu aliyepo sasa. Vita ya Kagera aliitangaza Mwalimu mwenyewe ingawa walikuwepo watu kwenye nafasi hizo walipo akina Sitta, Membe na Lowasa. Huu pia ni uvunjaji wa makusudi wa katiba yetu ya JMT.
 
Mzee Mwanakijiji huwa nakueshimu sana lakini leo umeongea pumba.Taaluma yako ya uandishi wa makala huishie huko huko.Wala hujui lolote juu ya Jeshi na hasa JWTZ,wala hujui hasa chanzo kilichokuwepo cha vita kati ya TZ na UGANDA,sanasana utaeleza ni mipaka lakini chanzo hadi kuwa mipaka ilikua nini hujui unaishia kubwabwaja.Labda ni kwambie jambo la msingi,kama mnatuchokoza mkazania hatutaweza kufanya lolote eti hatuna hela,tayari mmefeli vita,kwa taalifa tutawapiga ndani ya dk 30,naongea kama mmoja wa JWTZ,we kaongelee kwenxe magazeti mi ntaongea kwa vitendo,subiri utaniambia
 
Last edited by a moderator:
MM,
Ningekuwa na madaraka ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ningeagiza ukamatwe mara moja na ufunguliwe kesi ya uhaini. Nchi inapokuwa kwenye hali tete namna hii hutakiwi kutoa habari yenye heading ya namna hii, bila kujali ina ukweli ama la.

Na, ashuming kweli hatuna hela, unataka adui sasa atuvamie akijua kuwa hatuna hela? Ningeomba hii mada ifutwe na tuendelee na mijadala mingine, na pia watu wawe waangalifu na watu popular ndani ya forum hii kwa sababu wakati mwingine huwa wanachemsha saaaana ila tunashindwa kuona sababu ya popularity iliyowafunika.
Kwa hili MM ningekuomba usiongee sana hapa, kama una nafasi ongea na hao viongozi na wana siasa ana kwa ana, au hata kwa simu, uwape duku duku lako na si kukaa unamwaga mwaga mambo yako hapa hadharani. Hili swala ni tete na tusilijadili sana hapa, tuviachieni vyombo vinavyohusika vitali-handle. This case is a unique one and very different fron RICHMOND, KAGODA or whichever. Tuliache tusikae tunapayuka payuka hapa. Mwenye hoja, akaongee na viongozi wetu wapo watamsikiliza, na siyo ku-publicize, tuna jeopardize usalama wa nchi yetu na tukiendelea hivi ipo siku itakuja kutugharimu, japo siyo sasa!
 
Kama tutakwenda vitani vijana woote mi siendi mpaka nimuone Ritz yupo pembeni yangu Mbambaa bay tunaelekea Malawi

mambo ya kina Ritz,lowasa,membe,na nani na nan pamoja na mpuuzi Mzee Mwanakijiji sisi hatuyaangalii wakati tunaenda ulingoni,kwenda ulingoni wengine ndio kazi yetu kwanza tunahamu,sisi tutawaface maadui tu mambo mengine ni baada ya ushindi,we baki jf lakn sis tutaenda kupigana kwa ajili ya nchi yetu na watu wake
 
Last edited by a moderator:

i wish every Tanzanian would know, understand and contemplate this...well said MM.
 
Wakati ndio huu, acha ushamba,unaandika usichokijua na pengine JWTZ ulikwenda kwa intake ya upishi au kucheza ngoma.Vita haipiganwi bila fedha na ndio maana logisitics kama mafuta na vyakula vitapatikanaje.?Mwanakijiji amehit point sanasana wewe pengine ni ufinyu wa elimu yako haivuki zaidi ya kivuli chako.
 
Last edited by a moderator:
Akamatwe kwa kosa lipi? Wa kututangazia nchi iko tayari kwa lolote ni Sitta au Lowasa? Waambie wanaSIASA wetu wasilikuze suala hili kwa malengo yao kijinga.
 
Makanyaga leo nimemshanga sana MM, huyu jamaa sikujui kuwa ni mpuuzi kiasi hiki,Namwambia tena kupitia kwako,Sisi(wapigangaji) hatuangalii matakataka ndani ya serikali kipindi hiki,tunachoangalia ni adui tu,Tutawapiga malawi kwa muda wa dk 30 na hapo ndipo mtakapo tuheshimu
 
Last edited by a moderator:
Uanajeshi wako una walakini. Amiri Jeshi Mkuu wako ni Sitta? Ni Membe? Ni Lowasa? Unapokea amri kutoka kwa yeyote tu!
 

na ndio maana huna hayo madaraka.keep on wishing.
 
Nakuunga mkono mpiganaji!!
 

sikulaumu elimu yako/ufahamu wako na ndio umeishia hapo,kaa ukijua hatujiandai mara tukisikia kuna vita,huwa tupo kamili wakati wote na siku zote.Mi sigombani na wewe kwa ujinga na upuuzi uliojazwa na MM,bwabwaja na maneno yanayotoka kwenye stock ya ubwege,lakn nakuapia tupo tayari,neno TAYARI namaanisha tayari kinamna yoyote ile,na huyo mama yenu tunawaletea hapa tena akiwa uchi,ngoja nikuache
 
Last edited by a moderator:
Dear Mwanakijiji,

As much as you have a point to say it is just a matter of the government to adjust itself. Unapolinganisha suala la vita na mishahara ya wananchi nadhani you are missing a point somewhere. Kwasababu gani mishahara ya wafanyakazi wa serikali au taasisi za serikali ni kuongeza mzigo wa gharama za uendeshaji wa serikali. Tofauti na inapotokea emergency kama hii ya vita ambapo tunaweza kujipanga gharama za serikali zikaongezeka kwa muda fulani tukiona hatutaweza kuendelea basi tunaweza kumaliza vita tukarudi kujipanga. Mwanakijiji huwezi ukafuta suala la vita kwani mipaka ya nchi ni mali ya nchi husika lazima ilindwe kwa gharama yeyote. Sasa kama wamekutuma wamarekani kuja kuwachanganya watu hapa na spin off zako waambie watanzania wako makini diplomatic discussions zina nafasi yake but hatuwezi kusema eti turule off war option hilo si suala la kubeza.

Nilikuwapo!
 

Waandishi wengine wavumilieni bure tu maana wanaandika kwa kutaka sifa.
Miaka ya Mwalimu wakati kuna suala tete mobilisation ya kitaifa alikuwa anaandika mwenyewe tahriri ya habari ili jamii tuwe na msimamo mmoja.

Sasa hili la Mwanakijiji kutaka kuonekana kupinga kila kitu kinamwonesha in a different light.
Aidha ni mwoga, au ni fifth columnist au analipwa kufanya hivyo.
Kwa vyovyote vile hali ya kiuchumi ya Tanzania leo ni much better off kuliko 1978, na vile vile kama vita itazuka, wapenda nchi wataenda mbele.

Makala kama hizi za Mwanakijiji kwa kweli zinaonyesha mtu mwenye akili inayomfaa yeye mwenyewe na hali ikiwa mbaya zaidi mpakani, itachukuliwa kuwa inamsaidia adui.
 
Uanajeshi wako una walakini. Amiri Jeshi Mkuu wako ni Sitta? Ni Membe? Ni Lowasa? Unapokea amri kutoka kwa yeyote tu!

Nashukuru,lakni wakati ukifika kila ulio mtaja hapo juu ndio utajua nafasi yake,ukishajua nafasi zao ndio uje uniulize tena ni Nani Amiri Jeshi Mkuu.SISI NI WATU WA VITENDO KWA MASLAHI YA NCHI NA WATU WAKE BILA KUJALI KUNA WANANCHI WAJINGA NA MTAILA KAMA WEWE
 
Sahihi sana mze mwanavillage,ila apo pa kusema wanaume wote 18+ twende vitani,ween4 hatupo tayari na hatutaki kabsaa uo upuuzi,hawakuona umuhim wetu kabla af leo kwenye kifo ndo wanatuweka mbelembele! Maisha ya kitz hayatufanyi tupate uchungu wa kufia nchi. Kama jeshi lisipotosha wapeleke watoto wao ili wakapiganie maslahi na miradi ya baba zao,akina sie hapana kwa kweli.
 

Mkuu,

Mwanakijiji kama hujamstukizia ni jasusi ambaye anachonganisha mada ili apate kujua reaction yenu ikoje. Na nazidi kujidhihirisha nachokisema kwa makala yake hii na nyengine aliyoiweka leo asubuhi. Kwanini mada zake mara nyingi ni controversial aiming at getting attention. Mfano hii inashangaza analalamika hatuko tayari kwenda kwenye vita wakati nikimuuliza JE WAMALAWI WAKIGOMA KUTUPA ENEO LETU TUWAAMBIE HAYA ASANTE TUNAWASHUKURU NA TUNA MBEYA MNAWEZA KUCHUKUA NA PIA RUKWA. HUO UTAKUWA UPUMBAVU WA HALI YA JUU!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…