Swali la kufungia mwaka; Kwanini mahakama ya mafisadi imekosa kesi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wakati wa kampeni Mh JPM alisema kua anaenda kuanzisha mahakama ya mafisadi kuwashughulikia mafisadi wote waliolitafuna taifa letu miaka yote bila huruma, ndio amaepewa ridhaa akaianzisha hiyo mahakama! Je, ni kwanini inakosa kesi? Hao mafisadi waliolitafuna taifa letu miaka yote wako wapi?

Je, 2020 watawaambia nini watanzania ikiwa watataka ridhaa tena?
 
Imekosa kesi kwa sababu, Lowassa sio fisadi; ilikuwa UONGO MTUPU!

Rostam Aziz & Yusuf Manji sio mafisadi, mlisumbuliwa tu na UBAGUZI WA RANGI!!

Kwamba eti kulikuwa na Escrow Saga... ni UZUSHI wenu tu nyie watu!

Eti MV Dar es salaam ilinunuliwa kwa mabilioni ya pesa wakati speed yake Dar es salaam hadi Bagamoyo ni bora upande mtumbwi... huo ni uzandiki mlioleta ili kumkwamisha Mtukufu!

Eti oh! Mbona Lizaboni wa JF alisema Emmanuel Nchimbi kajimilikisha floor mzima lile Jengo la UVCCM na bado kapigwa Ubalozi... shenzi taipu; hilo jengo linawahusu nini?!

Halafu hakuna mijitu inayonikera kama inayopenda kukumbushia kumbushia nyumba za serikali eti zilizouzwa na nanii... nyumba zile nyie zenu?! Nyumba aache mkoloni kihele hele muwe nacho nyinyi?! Shenzi taipu... wivu tu!

Nitarudi kuongeza mengine lakini tu mjue... sababu za mahakama ya mafisadi kukosa mafisadi ndio zile zile ambazo zimefanya vijiji na mitaa yenu ikose 50 Million tulizowaambiwa! Kuna mwenye tatizo hapo?

Btw, hivi hamfahamu kwamba Majaji wetu wengi hawana PhD?! Sasa watazichambua vipi kesi za mafisadi?
 
Dahh......!!
Hivi...... Chenge na Rugemarila wapo wapi?
Samahani kwa kutoka nje ya mada...
 
Wakati wa kampeni Mh JPM alisema kua anaenda kuanzisha mahakama ya mafisadi kuwashughulikia mafisadi wote waliolitafuna taifa letu miaka yote bila huruma, ndio amaepewa ridhaa akaianzisha hiyo mahakama! Je, ni kwanini inakosa kesi? Hao mafisadi waliolitafuna taifa letu miaka yote wako wapi?

Je, 2020 watawaambia nini watanzania ikiwa watataka ridhaa tena?
Hivi kwa uelewa wako ni sifa kuwa na kesi nyingi au ni sifa kutokuwa na kesi mahakamani?
Kweli watanzania uelewa wetu ni 0+
 
nina maana viongozi wengi wangeteketea kwenye mahakama ya mafisadi ivyo bora wakaushe

Wanalindana na hakuna mabadiliko yatakayotokea kama tutaendelea kuwabeba beba namna hii. Frais hayuko serious na mambo muhimu siku si nyingi ataingiza kwenye kupiga madili awe kama wale wale tu waliopita.
Bado nasema Tz tuna safari ndefu
 
Wamesema wanafanya mpango wa kuliomba bunge libadilishe tarakimu. Kwa sasa Fisadi ni yule wa kuanzia Tshs bilioni 1. Wanataka washushe at least mpaka million milioni 400 ili wakukamate nawewe ulienzisha huu uzi.
Wakiona hapo hawajapata mtu tena washushe ianzie shilingi 500 watukamate wote. Tunaotafutwa mara nyingi kwenye hizi kesi ni walalahoi ukae ukijua hilo
 
Hivi kwa uelewa wako ni sifa kuwa na kesi nyingi au ni sifa kutokuwa na kesi mahakamani?
Kweli watanzania uelewa wetu ni 0+
Uelewa wako ni wa kiwango cha nchini sana, umesoma mada ukaelewa vizuri? Nini Dhamira ya uanzishwaji wa mahakama hiyo?
 
Back
Top Bottom