Naona sasa CCM imeamua kuzunguka na mawaziri na kuwaita baadhi ya watendaji wa serikali kwenye mikutano yenu. Mimi sijawaelewa mna maana gani na nina maswali machache yanayonisumbua kichwani kama ifuatavyo,
Moja, mnategemea mawaziri na watendaji hawa wawaambie nini wananchi wakati wao ni sehemu ya matatizo? Kwa mfano Waziri wa kilimo na wa ushirika na masoko wamekuwepo na wamekuwa wakishuhudia bei ya kahawa ikishuka toka shilingi elfu tano kwa kilo ikaja 3500 kwa kilo na sasa ni shilingi 2000. Pamba nayo matatizo ni hayo hayo. Unatemea wawaeleze wakulima kuwa bei ni nzuri wawaelewe?
La pili, Mnategemea waziri wa viwanda na biashara au waziri wa fedha na uchumi awaeleze nini wananchi wakati huu wa mfumuko mkubwa wa bei. Unategemea wananchi wakushangilie kusikia takwimu za kuwa uchumi unakua wakati bei za vitu zinapanda kila kukicha?
Unategemea waziri wa fedha na wa utumishi awaambie nini watumishi wa umma wakati wafanyakazi wanapata mishahara tarehe 38 na wengine mishahara yao haijarejkebishwa zaidi ya miaka miwili iliyopita?
La tatu, Je ni nani atawalipa posho hawa mawaziri wanaopiga kampeni za CCM?
La nne, Si kwamba CCM inataka iwatengenezee posho hawa jamaa ili asilimia fulani irudi CCM?
Je CCM inatambua kuwa sasa watanzania hawataki ngonjera ila wanataka kuona vitu vikifanyika. Hawataki kusikia hili jambo lipo kwenye mchakato ila wanataka kuona bei nzuri za mazao yao na masoko ya uhakika, mishahara ikilipwa kwa wakati bila kuwa na malimbikizo, mfumuko wa bei usiotisha.