Swali la kizushi kwa Nape Nnauye

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
273
Naona sasa CCM imeamua kuzunguka na mawaziri na kuwaita baadhi ya watendaji wa serikali kwenye mikutano yenu. Mimi sijawaelewa mna maana gani na nina maswali machache yanayonisumbua kichwani kama ifuatavyo,

Moja, mnategemea mawaziri na watendaji hawa wawaambie nini wananchi wakati wao ni sehemu ya matatizo? Kwa mfano Waziri wa kilimo na wa ushirika na masoko wamekuwepo na wamekuwa wakishuhudia bei ya kahawa ikishuka toka shilingi elfu tano kwa kilo ikaja 3500 kwa kilo na sasa ni shilingi 2000. Pamba nayo matatizo ni hayo hayo. Unatemea wawaeleze wakulima kuwa bei ni nzuri wawaelewe?

La pili, Mnategemea waziri wa viwanda na biashara au waziri wa fedha na uchumi awaeleze nini wananchi wakati huu wa mfumuko mkubwa wa bei. Unategemea wananchi wakushangilie kusikia takwimu za kuwa uchumi unakua wakati bei za vitu zinapanda kila kukicha?

Unategemea waziri wa fedha na wa utumishi awaambie nini watumishi wa umma wakati wafanyakazi wanapata mishahara tarehe 38 na wengine mishahara yao haijarejkebishwa zaidi ya miaka miwili iliyopita?

La tatu, Je ni nani atawalipa posho hawa mawaziri wanaopiga kampeni za CCM?

La nne, Si kwamba CCM inataka iwatengenezee posho hawa jamaa ili asilimia fulani irudi CCM?

Je CCM inatambua kuwa sasa watanzania hawataki ngonjera ila wanataka kuona vitu vikifanyika. Hawataki kusikia hili jambo lipo kwenye mchakato ila wanataka kuona bei nzuri za mazao yao na masoko ya uhakika, mishahara ikilipwa kwa wakati bila kuwa na malimbikizo, mfumuko wa bei usiotisha.
 
MKALIKENYA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,196
484
Nape nadhani hii nguvu unayoitumia kutunga uongo dhiki ya CHADEMA ungeitumia kumjua BABA yako ni nani kati ya MWANDOSYA na MNAUYE.
 
KOMBESANA

JF-Expert Member
Jun 18, 2009
918
212
Naam Nape,hii pia ni defining moment!Haya,face it dear!Kidumu Chama cha Mapinduzi,yale ni mambo ya kupima commitment kwa Chama kwa MWANAMKE mwana CCM,Kitanda hakizai haramu anyway!Tuyaache hayo
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
938
icon1.png
Re: Swali la kizushi kwa Nape Nnauye

- Unataka Katibu Mwenenzi wa Chama Tawala aje hapa ajibu masuala ya kizushi? Really?

Es!
 
MpangoA

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
360
229
Japo mada inachakachuliwa, lakini hii ya kutotajwa inaleta shaka. Nani alipeleka hilo tangalo la kumbukumbu. Kwa nini Nape hayumo kwenye list? Ila mambo mengine bwana. Si wangemtaja tu mpaka umma tujue..Pole sana Nape kwa kukosa kambi. Ipo siku utaulizwa hili suala kweupe kwenye kadamnasi.
 
mmang'ula

Member
Nov 27, 2012
22
3
Pole mwenezi haya ndo matunda ya kubeza waliokutangulia kuona jua sasa wanakuhabarisha ur truly identity. Ukifahamu ndo ukurupuke na mengine kama jadi yako vuvuzela.
 
Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,449
714
Mleta mada ana hoja mujarab, lkn wachangiaji wengine wameanza kushambulia personalities.

Nashindwa kuona tofauti ya Nape na ninyi mnaomuingiza Prof Mwandosya na Marehemu Kanali Nnauye.

Mnashusha hadhi ya JF bandugu.
 
KISANTILITEDI

Member
Dec 31, 2009
96
27
Ndugu zangu Watanzania naona tunakokwenda sio kuzuri. Katika jambo watanzania tunapaswa kujivunia ni maadili na nidhamu. Namuheshimu Nape kama kiongozi na pia kama kaka katika taifa japo naweza nikawa natafutiana nae kimawazo. alieanzisha hii thread kauliza maswali ila thread imekosa mwelekeo na wala sidhani kama Nape atakuwa tayari kujibu.. huwezi katika hali ya kawaida kumuuliza mtu baba yake ni nani? kwani wewe unajua baba yako ni nani.

kwanza ni kumpongeza Nape kwa jinsi alivyojitahidi mpaka leo hii wewe unamjadili! kwani leo ni watanzania wangapi hawajui baba zao. na kuna wengine hapa wana watoto hawataki kujitambulisha kwao. sio vizuri wala nidhamu kumwaattack Nape kwa style hiyo. Jana nilisoma thread ya Nape alimwita Dr Slaa Babu, sio kwamba alimkashifu..

Ile ilikuwa ni lugha ya taswira tuu ili kupunguza nguvu ya Dr slaa, Nadhani hata Dr akija hapa atasema kuwa anamuheshimu Nape na najua ndivyo hivyo NApe anamuheshimu Dr. Ningependa niione jamii Forum ikiwa na hoja za kujenga na pia watu tupunguze ushabiki. tuwe tunafikiria hiyo ndivyo tutakavyojenga taifa letu.. tunatafautiana kimtazamo tuheshimu mitazamo ya wenzetu na pia tujenge hoja na kabla ya kujenga hoja tutafakari kwanza mchango wake kwenye Jamii. Pia ndugu zangu wa chadema naomba tupunguze jazba kwenye ushabiki. sijasema tupunguze ushabiki, napenda ushabiki na ninashabikia chadema. lakini tuangalie misingi yetu na pia tuangalie ni Tanzania ya namna gani tunaitaka, kisha tuijenge.. naamini watanzania wote kwa pa1 tutaijenga nchi yetu. Asanteni sana na ninawatakia jioni njema wandugu
 
Kichuli

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
320
54
Umeona ee nawambiaga washabiki wa chadema wote mnafanana na wanywa gongo hivi kweli unaweza kumuliza mtu kuhusu baba yake je wewe umekuwa kitanda kwamba wakati wanamtafuta mtoto walipitia kwake? Nape ni kiongozi makini anaheshima za kutosha na ndiyo maana ccm ikamwamini ikampatia jukumu la kuwasambalatisha chadema kwa hoja na wala sio matusi kama ya kwenu lakini pia muelewe kwamba humu watu wengi sana wanasoma forum hii sasa unapo ingiza hoja humu ambayo hata wewe mwenyewe inakuzidi basi ni hatari sana kwa wana jamii forums wote wanaosoma na kuchangia humu ndani!!
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,859
7,320

Ukishimu wengine nawe utaheshimiwa kitendo cha Nape kumdhalilisha Dr . Slaa unaona ni sawa? je unakumbuka maneno machafu aliyoyatoa Nape akiwa Mwanza nadhani kwenye kampeni za udiwani pale furahisha? , Umesahau matus aliyoyatoa majuzi kwenye ziara kusini?

Binafi Nape awali nilikuwa namueshimu sana enzi zile za arakati za kuipigania UVCCM na ufisadi lakini kumbe ilikuwa ni njaa tu sasa ameshiba anaanza kuonekana sura yake halisi kiukweli amekuwa mtu wa ovyo sana tofauti na fukra zangu za awali mtu kama huyo huwezi tegemea aheshimiwe wakati hiyo hadhi hana.

Kwa mwendo huu namtabiria hali mbaya sana ya kisiasa mbele ya safari.
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,716
Ndugu zangu Watanzania naona tunakokwenda sio kuzuri. Katika jambo watanzania tunapaswa kujivunia ni maadili na nidhamu. Namuheshimu Nape kama kiongozi na pia kama kaka katika taifa japo naweza nikawa natafutiana nae kimawazo. alieanzisha hii thread kauliza maswali ila thread imekosa mwelekeo na wala sidhani kama Nape atakuwa tayari kujibu.. huwezi katika hali ya kawaida kumuuliza mtu baba yake ni nani? kwani wewe unajua baba yako ni nani.

kwanza ni kumpongeza Nape kwa jinsi alivyojitahidi mpaka leo hii wewe unamjadili! kwani leo ni watanzania wangapi hawajui baba zao. na kuna wengine hapa wana watoto hawataki kujitambulisha kwao. sio vizuri wala nidhamu kumwaattack Nape kwa style hiyo. Jana nilisoma thread ya Nape alimwita Dr Slaa Babu, sio kwamba alimkashifu..

Ile ilikuwa ni lugha ya taswira tuu ili kupunguza nguvu ya Dr slaa, Nadhani hata Dr akija hapa atasema kuwa anamuheshimu Nape na najua ndivyo hivyo NApe anamuheshimu Dr. Ningependa niione jamii Forum ikiwa na hoja za kujenga na pia watu tupunguze ushabiki. tuwe tunafikiria hiyo ndivyo tutakavyojenga taifa letu.. tunatafautiana kimtazamo tuheshimu mitazamo ya wenzetu na pia tujenge hoja na kabla ya kujenga hoja tutafakari kwanza mchango wake kwenye Jamii. Pia ndugu zangu wa chadema naomba tupunguze jazba kwenye ushabiki. sijasema tupunguze ushabiki, napenda ushabiki na ninashabikia chadema. lakini tuangalie misingi yetu na pia tuangalie ni Tanzania ya namna gani tunaitaka, kisha tuijenge.. naamini watanzania wote kwa pa1 tutaijenga nchi yetu. Asanteni sana na ninawatakia jioni njema wandugu
Nadhani Nape ndiye angeanza kuwa na hayo maadili kwanza. Lugha za mitaani anazoziandika hapa hata hazifanani na wadhifa wake. Kwa jinsi hiyo ndio maana watu wanajibu hoja zake kulingana na lugha anayoitumia yeye mwenyewe!!!
 
Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,691
475
100%, haya ni maswali ya msingi, vilaza hawatakujibu maana wamezoea kupiga domo,
 
Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,691
475
Ndugu zangu Watanzania naona tunakokwenda sio kuzuri. Katika jambo watanzania tunapaswa kujivunia ni maadili na nidhamu. Namuheshimu Nape kama kiongozi na pia kama kaka katika taifa japo naweza nikawa natafutiana nae kimawazo. alieanzisha hii thread kauliza maswali ila thread imekosa mwelekeo na wala sidhani kama Nape atakuwa tayari kujibu.. huwezi katika hali ya kawaida kumuuliza mtu baba yake ni nani? kwani wewe unajua baba yako ni nani.

kwanza ni kumpongeza Nape kwa jinsi alivyojitahidi mpaka leo hii wewe unamjadili! kwani leo ni watanzania wangapi hawajui baba zao. na kuna wengine hapa wana watoto hawataki kujitambulisha kwao. sio vizuri wala nidhamu kumwaattack Nape kwa style hiyo. Jana nilisoma thread ya Nape alimwita Dr Slaa Babu, sio kwamba alimkashifu..

Ile ilikuwa ni lugha ya taswira tuu ili kupunguza nguvu ya Dr slaa, Nadhani hata Dr akija hapa atasema kuwa anamuheshimu Nape na najua ndivyo hivyo NApe anamuheshimu Dr. Ningependa niione jamii Forum ikiwa na hoja za kujenga na pia watu tupunguze ushabiki. tuwe tunafikiria hiyo ndivyo tutakavyojenga taifa letu.. tunatafautiana kimtazamo tuheshimu mitazamo ya wenzetu na pia tujenge hoja na kabla ya kujenga hoja tutafakari kwanza mchango wake kwenye Jamii. Pia ndugu zangu wa chadema naomba tupunguze jazba kwenye ushabiki. sijasema tupunguze ushabiki, napenda ushabiki na ninashabikia chadema. lakini tuangalie misingi yetu na pia tuangalie ni Tanzania ya namna gani tunaitaka, kisha tuijenge.. naamini watanzania wote kwa pa1 tutaijenga nchi yetu. Asanteni sana na ninawatakia jioni njema wandugu

ukweli siku zote ni dawa chungu, hana budi kumeza hivyo hivyo, pili wewe si msemaji wa nape, mwache mwenyewe aseme
 
Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,691
475
Umeona ee nawambiaga washabiki wa chadema wote mnafanana na wanywa gongo hivi kweli unaweza kumuliza mtu kuhusu baba yake je wewe umekuwa kitanda kwamba wakati wanamtafuta mtoto walipitia kwake? Nape ni kiongozi makini anaheshima za kutosha na ndiyo maana ccm ikamwamini ikampatia jukumu la kuwasambalatisha chadema kwa hoja na wala sio matusi kama ya kwenu lakini pia muelewe kwamba humu watu wengi sana wanasoma forum hii sasa unapo ingiza hoja humu ambayo hata wewe mwenyewe inakuzidi basi ni hatari sana kwa wana jamii forums wote wanaosoma na kuchangia humu ndani!!

kama kawaida yenu,mnakimbilia kushika kwenye kidonda, mbona hoja za kujibu ziko nyingi!!
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,716
Du!!! Kumbe pamoja na makeke yote huyu bwana alipatikana kwa mwendo mdundo ee!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom