Kiwi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 1,054
- 990
Wanajamvi heshima kwenu,
Wakati tunaendelea na kampeni za uchaguzi na wakati wengine tukiwa tunajipanga kuelekea Jangwani kesho kushuhudia ufunguzi rasmi wa kampeni za UKAWA, naomba kujuzwa kama Bunge lilishavunjwa? Hili swali niliwahi kuliuliza lakini nilimuudhi sana mwanajamvi mmoja akanitolea lugha isiyopendeza.
Kwa kumbukumbu zangu JK alipaswa kulivunja Bunge Dodoma kabla ya kikao cha kuwajadili wagombea urais kwa tiketi ya CCM. Lakini kulitokea sintofahamu na akaahidi (kama sikosei) kulivunja Bunge 20.8.2015. Tangu kipindi hicho mpaka sasa yametokea mabadiliko mengi kiasi cha mimi binafsi kushindwa kufuatilia na kuweka kumbukumbu sahihi.
Kama Bunge halijavunjwa, litavunjwa lini wakati kila mtu sasa hivi yuko kwenye kampeni? Baadhi ya wabunge wamesharudi kwenye majimbo yao kuomba ridhaa ya miaka mingine mitano, watakatiza kampeni ili warudi kwa shughuli hiyo? Je itakuwaje kwa wabunge wapya (na wa zamani watakaorudi tena) ambao watachaguliwa Oktoba 25? Wanajamvi naomba kupewa elimu kuhusu hili.