Swali la Kimantiki: CCM wamuue Alphonce Mawazo kwa sababu zipi hasa?

kama ndo wanasheria tulionao mnaandika hivi, I'm sure tuna safari ndefu ya kufika nchi ya ahadi!!!

Nadhani hawa ni kati ya wanasheria wasioelimika wanaotegemewa na chama kikubwa kuwasaidia kuwatetea humu jf ila hahati mbaya sana kwao huwa hawana hata muda wa kusikiliza taarifa za habari za vyombo mbali mbali. Kwa wengi tuliosikiliza taarifa ya habari saa mbili usiku jana tarehe 14 tuliwaona na kuwasikiliza wananchi pale nje ya hospitali ya wilaya ya Geita na wanaoaminika kumleta pale nd.Mawazo wakisema wazi walivamiwa na kundi la green guards. Hawa green guards walijiandaa na silaha za mapanga,mashoka na nondo na kuwazidi nguvu. Kwa kutumia akili kidogo tu utaona mlengwa haswa pale alikuwa ni marehemu Mawazo. Walijitahidi kupambana huku wakiwa hawana silaha na hawakupata msaada wowote wa polisi na wala pale hospitali hatukuliona gari la polisi. Hili suala lipo kisiasa zaidi ya kulihusisha na visasi hata kama haukuwepo uhusiano mwema na Zitto siku za nyuma.Polisi wasingeweza kutumia silaha za jadi kumuua Mawazo na wala hawana mafunzo hayo. Wana uwezo wa kumweka rumande wakati wowote. Wanaweza kumfungulia makesi mengi watakavyo na hata kumshona risasi katika mazingira tata. Zitto hamiliki green guards na hata polisi hawana mamlaka na hivyo vikundi na wala katika mauaji ya Mwangosi polisi hawakutumia silaha za jadi bali risasi. Kutueleza mafanikio ya ccm Geita na kuwa marehemu hakuwa tishio kwao hayo ni kadri ya maono yako wanaojua alikuwa tishio kiasi gani ni waliokuwa nae kwenye kampeni. Kamanda Mawazo awe na visasi lakini watekelezaji wa adhabu wawe green guards sijui katika uanasheria wako ambao hufundishwa pia misindi ya awali ya uchunguzi/upelelezi hautii shaka au ni yale majigambo mliyo nayo ya kujipachika udaktari na uprofesa bila kujua mnavunja sheria? Tumempoteza Mawazo wala sitegemei haki yoyote kutendeka ila ninachoamini ni kuwa damu ya Mawazo inayolia ardhini itapata majibu kwa wabaya wake kuumbuka vibaya na usishangae hata wapangaji wa mauaji hayo kutajwa hadharani. R.I.P. KAMANDA ALPHONCE MAWAZO.
 
Hata angeshinda kesi yake kulikuwa na threat gani kwa CCM iliyoshinda viti zaidi ya nusu ya viti vyote majimboni kwenye uchaguzi huu??????
Naona unatetea ccm na Polisi kwamba hawajauwa, na unataka malumbano ya hoja (debate) na wanaodai ameuwawa! Naona wewe labda umesoma sheria lakini huja soma utu wala ubinadamu. Upo tayari kutetea 'unachoshabikia' hata kama kina madhara na maumivu kwa wengine. Hii debate Kama wewe ni mwanasheria, lakini hujui maana ya sheria, kwamba ni kulinda watu, sasa unalinganisha 'ukorofi' gani wa Mawazo na Tendo la kumkata mapanga na kumuua?!
 
Amani ya Bwana iwe nanyi wadau,

Kwanza kabisa napenda kuanza kutoa pole kwa wale wote walioguswa na kifo na ndugu Alphonce Mawazo. Kifo chochote sio jambo la kawaida kwa hiyo hata iweje lazima pole itolewe hasa kwa wale walioguswa kwa dhati na kifo hiki.

Nikiwa natafakari kifo hiki kumekuwa na maneno mbalimbali yamekuwa yakiendelea humu mitandaaoni kwa watu kurushiana maneno hasa wakihusishana na kifo hiki. Watu hawa kwa kifupi ni wafuasi wa CHADEMA wakisema kuwa CCM wanahusika na kifo hiko, wengine wanadai kuwa ni polisi na huyu si mwingine bali ni mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini ambaye ameenda mbali zaidi hadi kuwataja polisi kuwa wanahusika na kifo hicho.

Nikiwa mwanasheria na mdau wa mambo ya kisheria hapa napenda nishirikiane na wenzangu jambo hili, nalo ni kama nilivyoandika kwenye kichwa cha thread husika kuwa CCM WAMUUE MAWAZO KWA SABABU ZIPI HASA?

Hili swali linaweza kuonekana la ajabu kwa watu ambao sio critical thinkers ila kwa critical thinkers ni swali la msingi na la muhimu sana kwa sababu hata upande kwa upelelezi unapoanza kuchunguza tukio ili kumuhusisha mtuhumiwa na mauaji kwanza wanaanzaga kuangalia MOTIVE YAANI KWA LUGHA NYINGINE INTENTION.

Kwa wale msioelewa maana ya motive ni nia au dhamira ya mtenda kosa. Sasa kwenye hili tukio ili kuwahusisha CCM napenda kuuliza kuwa Je kuna sababu zipi hasa kwa CCM kumuua ndugu Mawazo ili tu kuweza kutengeneza au kupata motive yao?

Sijaandika ili kuwatetea CCM ila as long as taarifa za kipelelezi hazijatoka napenda tujiulize kwa pamoja kuna sababu gani za msingi kwa CCM kama chama kupanga au kutekeleza mauaji ya ndugu Mawazo?

Nimefikiria sana hata sijaweza pata hata moja kwa sababu hata kwa Geita mawazo hakuwa threat kwa chama kwa kusema kuwa hali ya upinzani kwenye uchaguzi huu kwa Geita imeonyesha kuwa haikuwa nzuri yaani hata ushawishi wao haujaonekana kwa sababu robo tatu ya mkoa tena kama sio wote kwenye uchaguzi uliomalizika imeenda CCM sasa kulikuwa na threat gani kwa CCM hadi waseme wamuue ndugu mawazo? kwa sababu ili iweze kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo lazima narudia ni lazima ili motive ipatikane tuweze kujiridhisha kiwango cha threat ambacho ndugu mawazo alikiweka kwa CCM. Kama hakijapatikana basi hapo hatuwezi kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo.

Jambo la pili ni kuhusiana na Polisi kwa sababu ndugu LEMA amejaribu kuwahusisha polisi, swali lilelile napenda kuli impose hapa Je, ndugu Mawazo alikuwa na threat gani kwa polisi hadi polisi wahusike na mauaji yake? Hadi sasa swali hili halijaweza kujibiwa popote pale.

Napenda kumaliza kwa kusema ingawa haturuhusiwi kuongelea upande negative wa marehemu ila hapa lazima tuseme kitu. Marehemu alikuwa anajulikana vizuri sana kuwa ni mtu mtata sana hasa kitabia na hulka na hata kuna thread humu ndani alizokuwa akimsema vibaya kwa vitisho ndugu Zitto Kabwe zinaonekana humu ndani. Naomba tusiondoe nadharia hii kwenye kifo cha marehemu kuwa inawezekana marehemu alikuwa kwenye ugomvi na wauaji wake na kwenye huo ugomvi ndo yakatokea yaliyotokea. Na pia inawezekana yeye ndo alikuwa mgomvi kwa sababau hadi sasa hivi hatujaweza kuelezwa kuwa marehemu alikuwa na nani na kitu gani kilitokea hadi kusababisha mauti yake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.
Mkuu niki rejea kwenye historia matukio ya namna ya kifo cha Mawazo,tukianza na la Mwangosi, taarifa ya awali ya polisi ilisema kuwa marehemu alirushiwa kitu kutoka ofisi ya cdm kikamlipua na kumsababishia mauti, baada ya picha za tukio kuzagaa ikaonekana jinsi marehemu alivyokuwa amezungukwa na maaskari watatu kiasi cha kuibua maswali yanayo hoji uhakika wa taarifa ya polisi. Ni picha na video zilizo wekwa mitandaoni ndo zilizo badilisha kauli ya police! na kupelekea mmoja tu narudia mmoja tu miongoni mwa waliokuwa wame mzunguka alifunguliwa mashtaka, lakini pia kwenye kesi hiyo ambayo sijui ilivyo isha, tulishuhudia jinsi polisi walivyo mlinda na kumfunika mwenzao dhidi ya waandishi wa habari asipigwe picha tofauti na wafanyavyo kwa watuhumiwa wengine wenye tuhuma sawa na askari mwenzao "mmoja", kubwa zaidi Kamuhanda RPC wa Iringa akapandishwa cheo. Hivi ulijiuliza the motive behind kifo cha Mwangosi?.
Tukio la soweto arusha unalikumbuka ndugu mwana sheria? hivi kuna yeyote aliye funguliwa mashtaka?. Humu JF pro ccm waliamini kuwa cdm wame jilipua ili ku extract sympathy za wana Arusha! na hivyo wapate kura za huruma!?! huku pro cdm ikituhumu ccm. Hivi pale Arusha ni chama gani kinacho hitaji huruma??! Ndugu mwana sheria hivi nini ilikuwa motive behind ya kurusha bomu na kuwapiga raia risasi pale soweto??
Kuna la Morogoro na kitu chenye ncha kali, kuna mauaji ya pale igunga, kuna wa arusha mwana chadema aliye katwa na "chain saw"?............. Mifano ni mingi sana na motive behind mauaji hayo yote ilikuwa ni nini/tukio????. Ukiniuliza comment yangu juu ya matukio hayo niliobserve figisufigisu kwenye ushughulikiaji wa kesi hizo kisheria na kwingine hapakuwa na kesi kabisaaa!, matukio mengine wahanga walio salimika wali taja aliye wadhuru lkn bado m/watuhumiwa hakuchkuliwa hatua as so long as ccm/selekali ya ccm ilikuwa ina nufaika kwa namna moja au nyengine na tukio hilo. Mwisho kabisa niseme tu, ukifanya kosa lolote ambalo ccm /selekali ina nufaika kwa namna moja au nyengine, wewe ujue kuwa upo salama kabisa kwani nyuma yako kuna walipo juu ya sheria.
 
kama ndo wanasheria tulionao mnaandika hivi, I'm sure tuna safari ndefu ya kufika nchi ya ahadi!!!

Wewe ni kapuku na hujitambui na hii status JF kwamba wewe senior expert haikufai. Ni bora eneo ambalo huna taaluma nalo bora ukae kimya. Wanaoelewa jinai na sheria ya jinai wamemuelewa mtoa mada.
 
Mtu akisoma andiko lako kwa makini inaonekana kama unaizungumzia ccm kama taasisi ambayo inaweza kuratibu mauaji kuanzia ngazi za juu( pengine makao makuu ya chama inahusika)kwa dhana hiyo mtu anaweza kujiuliza swali unalo uliza wewe, kwamba ccm wamuue Alphonce kwa sababu gani? Na hakua tishio kwao
Ungeuliza swali lako kwamba kwa nini walinzi wa ccm (Green Guard) wamuue alphonce Mawazo? Maana inasemekana ameuawawa na walinzi wa chama (kwa hili la wauaji tusubiri uchunguzi wa polisi)
Hawa walinzi.wa chama wanaweza kutumiwa na kiongozi yeyote wa chama pengine kwny kata kwa maslahi yake pengine hata bila kuwashirikisha uongozi wa wilaya au mkoa kama ni jambo/mgogoro binafsina mpinzani wake, kwa hiyo kusema kwamba hawahusiki na kumtaja marehemu kama mtata ambayo inaweza kuwa imechangia kifo chake ni kutoa hukumu, tusubiri uchunguzi wa mamlaka husika tutajua.
 
unajua ukisema kuwa wewe ni mwanwsheria tu watu wataanza kukujaji na ku-critic definitions zako ndipo wanapogundua kuwa unashindwa kuthibitisha uanasheria wako kwa hiyo hawataangalia hoja zako pia. Mwanasheria pia angeweza kutoa mifano mingine kama vile mauaji ya Daudi Mwangosi na kwa nini; nani aliyemteka nw kumtesa dr Ulimboka au Kibanda na kwa nini. Kwa niji hatuoni muendelezo au hitimisho la kesi hizo? Wewe si mwanasheria! Do not be too academic without a touch of down to earth references and example! Hata hivyo kwani ni lazima ujitambulishe kama mwanasheria ili kuvutia wasomaji?
Ubongo wako na wa jecha hakuna tofauti
 
pumbavu! kumbe mlianza CHADEMA mkawadunda wezenu hadi mkawajeruhi,sasa na wao wakajipanga wakalipa kisasi bahati mbaya kimezaa umauti ya kamanda wenu Mawazo

sasa mtajifunza kwa wote CCM na CHADEMA vurugu na maugomvi hayana tija

Ss ccm walienda kwny kikao cha chadema kufanya nn!!? We mwnyw ukiwa chumban na mwandan wako alf mtuakaja kuwachungulia na ukabahatika kumkamata cdhan kama utamuacha hvhv. Alf hyo mauti ya bahat mbaya ya kupigana na mapanga na mashoka ya kichwa imeanzag mwaka gan?
 
Kama usingejiita Mwanasheria, ningesoma hoja zako na kuendelea na shughuli zangu! Lkn kujiita wewe Mwanasheria ambaye huna hata uwezo wa kutafakari jambo jepesi tu alilosema Lema ni upuuzi usiovumilika. Ulichoandika ni sawa na kuifanya Fani ya sheria ionekana haina maana yoyote.
Ni wapi katika andiko la Lema amesema Polisi ndio wameua? Mwanasheria gani usiejua hata mantiki ya alichokisema Lema? U mjinga kabisa! Naamini huna uwezo hata wa kushinda kesi yoyote! Namhurumia alietoa pesa zake kukusomesha!
Ni afadhali kukaa kimya ili watu waendelee kudhani u mjinga kuliko kuzungumza na ukawathibitishia kweli u mjinga!

Bado tuna safari ndefu sana kama vyuo vyetu siku hizi vinazalisha wanasheria wa aina hii!
 
Kama ulvosema mkuu, wengi humu hueneza chuki zisizokuwa na maana, Mawazo alishiriki kumtesa na kumuumiza vibaya kijana mmoja aliekuwa nae kwenye kikao cha ndan, walimhisi anawarekod ndio wakaanza kumpiga kumbe nje wapo wenzake wengi wakaingia ndan, fujo zkaaanza alivoona imekuwa balaa ndo akachukua bodaboda kukimbia wao wakachukua gar mfukuzia ndo kumshambulia...hvo bas niseme hil Mawazo kawaiwa tu angewashinda yy bdo mngemjaza hapa kama.shujaaa...Geita yote majimbo yapo CCM.sasa mchango wake yy chadema kama.mwenyekt n upi ? Au kumjaza ujinga na kumuita kamanda ^hata ruzuku hapat.ndo ujembe?

Tatizo kubwa la watetezi wa ccm nikujitia upofu wa akili, macho na masikio

Tulimsikia makamba January akijinasibu kwa kinywa chake kwamba wao (ccm) wamekusanya matokeo na wamejumlisha watashinda kwa kishindo na wamefikia 67% nknknk.

Ukawa walikuwa na center zao pia lakin hatukumsikia kiongozi yeyote akipika data kama makamba na kutangaza madudu.

Je

Ni vipi ukawa wakaandamwa nakutiwa ndani ilhali makamba anatamba majukwaani kwa kuvunja sheria ile ile anayowatuhumu ukawa mzee wangu kova? Au sheria ziliundwa kudhibiti upinzan tuu na watawala haziwahusu?

2. Unauhakika 100% hayo majimbo ccm alishinda kihaki bila mizengwe yoyote?

3. Kama namba-2 hapo juu sahihi vipi polisi kuvuruga makusanyo ya kura kwa analysis nk na yale ya wa human wright, lakin kova na polisi wake wakiyaacha ya ccm kupitia makamba yatengeneza njia ya tume kuhalalisha walichokitengeza ccm kuwa ndio matokeo halisi?
 
Mimi sio mwanasheria na sina hakika kama nastahili kuitwa Great Thinker,labda normal thinker.Pamoja na hayo,
1.Utawezaje kuanza kupeleleza kisa kama hiki kwa kuanza na Motive badala ya Scenerio?
Sio kwamba scenerio au mazingira ya kifo ndio yatakujengea hoja ya motive?
2.Inasemwa ugomvi na wauaji ulinza kwenye kikao cha ndani(cha CHADEMA) ambapo waligundua kuna mamluki anawarekodi na walipoanza kumwadhibu ndio kundi kubwa la vijana wakawavamia na kwamba Mawazo alijaribu kujiokoa kwa kukimbia na pikipiki lakini walimfukuza kwa gari na kumkatakata hadi kupoteza uhai?
3.Wanasheria kama wewe wanadhani mtu wa kuingia kwenye mkutano wa ndani na kuanza kurekodi atakuwa na visa nje ya siasa? Na kama alikuwa anatafuta taarifa za kisiasa,atakuwa ametumwa na chama gani kama sio CCM ambao ndio washindani?
 
Namimi nikuulize kabla sijakujibu, je? mawazo hajauwawa? nakama ameuwawa nani aliemuuwa? pili, mwangosi aliuwawa na police alikuwa alikosa nini? tatu, je? muuza magazeti alieuwawa morogolo alikuwa na ushawishi gani? nne dk ulimboka aling'olewa meno alikosa nini? tano mkuu wa wilaya ya geita alisema atafurahi akiona maiti ya mawazo kwa mjibu wa lema je? aliimuuzi nini?
Mkuu kwa kweli inasikitisha sana Dr Ulimboka alienda mbali na kumtaja Ramadhani Ighondu!, sina hakika kama polisi ili mhoji zaidi ya kuibuka na kichaa ambaye naye ilikuja kuthibitika kuwa hakuhusika, ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa aliye kamatwa alitumika kusahaulisha watu. Pale soweto arusha nani aliye kamatwa?
 
قيطببباباطابتبطمبنبتبيطزبطتببتبتل
 
mwanasheriaaaaaaa!!!
mhhh hii ni hasara kwa taifa.
hebu rudia som.upya alichondika lema utajua msingi wa yy kusema vile.hapa ndo huwa nnasema.kwa kiasi kikubwa elimu yetu ya sasa km nchi haiondoi adui ujinga vichwani mwa watu.
hivi kweli unapinga madai ya uwezekano wa uhusika wa habari za siasa hapa?.
 
Hata angeshinda kesi yake kulikuwa na threat gani kwa CCM iliyoshinda viti zaidi ya nusu ya viti vyote majimboni kwenye uchaguzi huu??????

hebu muwe mnafikiri huku mkiwa na vichwa vilivyo huru.am unadhani kuchanganya maneno y kiingereza ndo kuonesha uzito wa uliloongea.
unadhani kweli hakuna tisho kupoteza jimbo moja.umefikiri juu ya hali ya mgombea anaenyang'anywa jimbo baada ya kushindwa?unadhani kwake si tatizo na hasara.unajuaje juu ya asili ya gharama alizotumia kwe chaguzi
 
Tatizo kubwa la watetezi wa ccm nikujitia upofu wa akili, macho na masikio

Tulimsikia makamba January akijinasibu kwa kinywa chake kwamba wao (ccm) wamekusanya matokeo na wamejumlisha watashinda kwa kishindo na wamefikia 67% nknknk.

Ukawa walikuwa na center zao pia lakin hatukumsikia kiongozi yeyote akipika data kama makamba na kutangaza madudu.

Je

Ni vipi ukawa wakaandamwa nakutiwa ndani ilhali makamba anatamba majukwaani kwa kuvunja sheria ile ile anayowatuhumu ukawa mzee wangu kova? Au sheria ziliundwa kudhibiti upinzan tuu na watawala haziwahusu?

2. Unauhakika 100% hayo majimbo ccm alishinda kihaki bila mizengwe yoyote?

3. Kama namba-2 hapo juu sahihi vipi polisi kuvuruga makusanyo ya kura kwa analysis nk na yale ya wa human wright, lakin kova na polisi wake wakiyaacha ya ccm kupitia makamba yatengeneza njia ya tume kuhalalisha walichokitengeza ccm kuwa ndio matokeo halisi?

Waangaliz wa kimataifa wametia sain zao kukubal uchaguz ulikuwa huru na haki, makamba alisem mpaka kufkia muda ule walikuwa na ushind wa majimbo 176 na ukwel n kuwa tumezidisha hyo idad... weng wenu hamkumjua lowasa vizur, lowasa hakiwah ishinda CCm na historia imemhukumu, lowasa angekuwa asset leo tungeona wabunge zaid ya Nusa wa Upinzan bungen lakn wapi...endeleeea kucheza ngoma ya mamvi tuljua yule n msanii hana madhaara na tumeudhihirishia ulmwengu ktl hlo, alitaka hack matokeoa atangZwe yeye walaah tungemfundisha adabu, ona wapo wap waliompa kura lowasa? Kaitisha maandamano lakN hakuna anaetokea hiyo n maaana tosha kuwa kura zake hazkutosha
 
Mkuu kwa kweli inasikitisha sana Dr Ulimboka alienda mbali na kumtaja Ramadhani Ighondu!, sina hakika kama polisi ili mhoji zaidi ya kuibuka na kichaa ambaye naye ilikuja kuthibitika kuwa hakuhusika, ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa aliye kamatwa alitumika kusahaulisha watu. Pale soweto arusha nani aliye kamatwa?
Sote ni wa kupita na atakayebahatika sana miaka 70+, na Alphonce Mawazo kafa si kwa ajili ya shibe ya familia yake, kabila lake, dini yake wala chama chake bali kwa ajili ya watanzania wote wanaoteseka na umasikini katika nchi iliyojaa neema na utajiri.
Na hao watakaokamilisha maisha yao hapa duniani huku wakiandamwa na majinamizi ya akina Dr. Ulimboka, Mwangosi, Mawazo nk hakika hizo laana zitavikuta hata vizazi vya tano vya uzao wao.
Alphonce Mawazo kanigusa sana ikiwa tu nikijaribu kujisahaulisha habari za Mohamed Mtoi.
Sijui kama Dr Magufuli aliyatoa moyoni lakini alipokuwa Muhimbili alisema wale wanaosababisha wagonjwa kuteseka 'watalipwa na Mungu', sasa sijui atasemaje kwa waliochukua roho ya Mawazo!

Amani ya Bwana iwe nanyi wadau,

Kwanza kabisa napenda kuanza kutoa pole kwa wale wote walioguswa na kifo na ndugu Alphonce Mawazo. Kifo chochote sio jambo la kawaida kwa hiyo hata iweje lazima pole itolewe hasa kwa wale walioguswa kwa dhati na kifo hiki.

Nikiwa natafakari kifo hiki kumekuwa na maneno mbalimbali yamekuwa yakiendelea humu mitandaaoni kwa watu kurushiana maneno hasa wakihusishana na kifo hiki. Watu hawa kwa kifupi ni wafuasi wa CHADEMA wakisema kuwa CCM wanahusika na kifo hiko, wengine wanadai kuwa ni polisi na huyu si mwingine bali ni mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini ambaye ameenda mbali zaidi hadi kuwataja polisi kuwa wanahusika na kifo hicho.

Nikiwa mwanasheria na mdau wa mambo ya kisheria hapa napenda nishirikiane na wenzangu jambo hili, nalo ni kama nilivyoandika kwenye kichwa cha thread husika kuwa CCM WAMUUE MAWAZO KWA SABABU ZIPI HASA?

Hili swali linaweza kuonekana la ajabu kwa watu ambao sio critical thinkers ila kwa critical thinkers ni swali la msingi na la muhimu sana kwa sababu hata upande kwa upelelezi unapoanza kuchunguza tukio ili kumuhusisha mtuhumiwa na mauaji kwanza wanaanzaga kuangalia MOTIVE YAANI KWA LUGHA NYINGINE INTENTION.

Kwa wale msioelewa maana ya motive ni nia au dhamira ya mtenda kosa. Sasa kwenye hili tukio ili kuwahusisha CCM napenda kuuliza kuwa Je kuna sababu zipi hasa kwa CCM kumuua ndugu Mawazo ili tu kuweza kutengeneza au kupata motive yao?

Sijaandika ili kuwatetea CCM ila as long as taarifa za kipelelezi hazijatoka napenda tujiulize kwa pamoja kuna sababu gani za msingi kwa CCM kama chama kupanga au kutekeleza mauaji ya ndugu Mawazo?

Nimefikiria sana hata sijaweza pata hata moja kwa sababu hata kwa Geita mawazo hakuwa threat kwa chama kwa kusema kuwa hali ya upinzani kwenye uchaguzi huu kwa Geita imeonyesha kuwa haikuwa nzuri yaani hata ushawishi wao haujaonekana kwa sababu robo tatu ya mkoa tena kama sio wote kwenye uchaguzi uliomalizika imeenda CCM sasa kulikuwa na threat gani kwa CCM hadi waseme wamuue ndugu mawazo? kwa sababu ili iweze kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo lazima narudia ni lazima ili motive ipatikane tuweze kujiridhisha kiwango cha threat ambacho ndugu mawazo alikiweka kwa CCM. Kama hakijapatikana basi hapo hatuwezi kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo.

Jambo la pili ni kuhusiana na Polisi kwa sababu ndugu LEMA amejaribu kuwahusisha polisi, swali lilelile napenda kuli impose hapa Je, ndugu Mawazo alikuwa na threat gani kwa polisi hadi polisi wahusike na mauaji yake? Hadi sasa swali hili halijaweza kujibiwa popote pale.

Napenda kumaliza kwa kusema ingawa haturuhusiwi kuongelea upande negative wa marehemu ila hapa lazima tuseme kitu. Marehemu alikuwa anajulikana vizuri sana kuwa ni mtu mtata sana hasa kitabia na hulka na hata kuna thread humu ndani alizokuwa akimsema vibaya kwa vitisho ndugu Zitto Kabwe zinaonekana humu ndani. Naomba tusiondoe nadharia hii kwenye kifo cha marehemu kuwa inawezekana marehemu alikuwa kwenye ugomvi na wauaji wake na kwenye huo ugomvi ndo yakatokea yaliyotokea. Na pia inawezekana yeye ndo alikuwa mgomvi kwa sababau hadi sasa hivi hatujaweza kuelezwa kuwa marehemu alikuwa na nani na kitu gani kilitokea hadi kusababisha mauti yake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.

Kabla ya kuja na hii thread ulijiridhisha juu ya ufahamu wako kuhusu Siasa za Geita? For how long have You known A.C Mawazo? Umefuatilia juu ya Taarifa za tukio la kuuawa kwake ipasavyo? Umeelewa mazingira ya Tukio lenyewe?
 
Waangaliz wa kimataifa wametia sain zao kukubal uchaguz ulikuwa huru na haki, makamba alisem mpaka kufkia muda ule walikuwa na ushind wa majimbo 176 na ukwel n kuwa tumezidisha hyo idad... weng wenu hamkumjua lowasa vizur, lowasa hakiwah ishinda CCm na historia imemhukumu, lowasa angekuwa asset leo tungeona wabunge zaid ya Nusa wa Upinzan bungen lakn wapi...endeleeea kucheza ngoma ya mamvi tuljua yule n msanii hana madhaara na tumeudhihirishia ulmwengu ktl hlo, alitaka hack matokeoa atangZwe yeye walaah tungemfundisha adabu, ona wapo wap waliompa kura lowasa? Kaitisha maandamano lakN hakuna anaetokea hiyo n maaana tosha kuwa kura zake hazkutosha

Waangalizi wa Kimataifa? Unaweza niwekea Vigezo vyao walivyovitumia kwenye Uangalizi? Je! Vilikidhi Uhalisia wa Zoezi zima la Uchaguzi? Pathetic!
 
Back
Top Bottom