Swali la Ijumaa: Hivi huu "utaifa" ni wa CHADEMA tu?

Swali la Ijumaa: Hivi huu "utaifa" ni wa CHADEMA tu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,253
Reaction score
44,595
Hivi huu unaoitwa "utaifa" kwanini hatusemi na CCM wauoneshe? CHADEMA imekuwa ikipigania Bungeni na nje ya Bunge kwa Rais Kikwete kuunda Tume ya Kimahakama (Judicial Inquiry Commission) ili kuchunguza mauaji yanayotokea mikononi mwa vyombo vya dola au yenye utata; lakini hadi leo Kikwete hajafanya hivyo? Je siyo maslahi ya taifa kwa yeye kufanya hivyo? Kwanini hatujasikia mwana CCM hata mmoja akiunga mkono hili au hili ni la "CHADEMA" lakini ujio wa OBama ni la "Kitaifa"? Huu "utaifa" ni nini hasa?

CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa POlisi wananyanyasa na Jeshi la POlisi linatumia nguvu mno kwenye mikusanyiko ya amani na limesababisha mauaji; wakataka IGP Mwema, Chagonja na Kamuhanda wawajibishwe; Kikwete akaamua kuwatunukia nishani za "utumishi uliotukuka"? Halafu watu wanasema CHADEMA ioneshe utaifa! Hivi kwanini Kikwete yeye haoneshi huo "utaifa"? Kwanini huu "utaifa" uwe wa CHADEMA kushabikia mambo ya serikali na CCM lakini wao CCM hawatakiwi kushabikia mambo ya upinzani na ukisikia mwana CCM anafanya hivyo anakuwa labelled kuwa ni "mpinzani" kwanini hao CCM hawaoneshi huo "utaifa"?

Huu "utaifa" Unaosifiwa kwa CHADEMA kwanini hatuudai kwa CCM ili na wao wauoneshe au haya mambo yote ambayo CHADEMA inapigania na kusimamia ni ya CHADEMA tu na siyo ya kitaifa? ila yale yanayofanywa na Ikulu ndiyo ya kitaifa? Au wao CCM na serikali yake wanakubaliwa tu kuwa wanayosema wao na kufanya ni ya "kitaifa" na ya wengine ni ya "kikabila, kidini na kikanda"?

Nauliza tu:

NB: Ukijisikia kuniita majina yoyote ya kejeli usijizuie I can handle punches.
 
Kweli kuna mambo mengine yanafanywa na hili chama letu yanaacha maswali mengi sana! Any way sijui mpaka sasa kama "turn the other cheek" or "send him to the cemetery " ipi ni njia sahihi kwa haya majitu.
 
huyu ndiyo mwanakijiji leo anarusha jiwe huku kesho kule...
 
daaaah Mwanakijiji ...!
binafsi silipendi neno amani, utulivu na utaifa hasa linapotumiwa na magarasa wa ccm, nasema hivyo kwakua maneno hayo yamekuwa yakitumika kupumbaza, kuviza akili na kuogopesha WATANZANIA.
Kila criticism dhidi yao haraka watakwambia unahatarisha amani na umoja wetu wa kitaifa...ni maneno yanayotumiwa kipuuzi kwa malengo ya kipuuzii.
Hawawezi kuiunda hiyo tume kwakua wao ndio waliolipua lile bomu, jamani huo ndio ukweli na wanajua kuwa chama chao kilihusika. Kikwete hataunda unless polisi wamuhakikishie wamesambaratisha ushahidi wote na ndio maana Arusha wanapambana kukamata kila mpiga picha na kila mtu wanaehisi anaweza kutoa ushahidi murua utakaowaingiza matatani wauaji wanaolindwa na dola.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , unataka CCM waunge mkono uundwaji wa tume ya kimahakama na wakati wanajua wazi ikiwepo tume huru na namna hiyo ,Wanaofanya mauaji ya raia sasa watajulikana, watashughulikiwa na kudhibitiwa, nao hawa CCM kwa sasa mbinu zao zote katika siasa zimeshashindikana na wamebakiza hii ya ...............Pekee! Sasa unataka wajikaange wenyewe kwa kukubali tume huru ya(kimahakama) uchunguzi? Hawatokubali mpaka watakapoona sasa maji yamefika shingoni.
 
Last edited by a moderator:
MWANAKIjiji uko sahihi kwa mtazamo wako, lakini si lazima chadema walipe baya kwa baya, kikubwa chadema kama chama kikuu cha upinzani kinapaswa kuwa makini kusimamia yale yote ambayo wanaya anzisha, kuhakikisha wanaishi kwayo.
wikiend njema
 
Last edited by a moderator:
Naungana na wewe M/Kijiji. Kuna haja ya kutafakari kwa kina jambo hili la ''Utaifa''. Napata wazo kuwa serikali ya CCM ni kwa ajili ya maendeleo ya 'utaifa' wa kiccm, na 'utaifa' wa CDM ni kwa ajili ya maendeleo na demokrasia ya Watanzania.
 
Betlehem lakini CDM wakigomea mambo ya CCM wanaambiwa hawana utaifa na hivyo wanalazimika kuyafanya ili wasifiwe wameonesha utaifa? Inaingia akilini kweli?
 
CDM waliowengi hawapendi kukosolewa na ukiwakosoa kwa nia ya kujenga basi utaitwa majina ya kila aina, katika uwanja wa siasa kuna makundi ma3 kwa uelewa wangu, la kwanza wanachama wa vyama la pili wasio na vyama(wanasubiri kupiga kula kwa chama chenye msimamo) la Tatu wasiotaka kusikia siasa(na hufanya mambo yao tu) ni upofu kujidanganya kuwa wanachama wako watakuingiza Ikulu, hapo sijataja wizi wa kura wa maccm,rufaa za hovyo,mizengwe nk. CDM kubalini kukosolewa!

"To know the enemy is half the victory"
 
Mbowe alipokwenda Ikulu ujio wa Obama ilikuwa ni utaifa huo huo.......lakini CCM wanaichukulia ni positive kwao! kwa mwelevu sio tatizo kwa mbowe kwenda kwenye shighuri waliyoaanda CCM, ila tujiulizeee, viongozi wetu wanajua wanachokitaka wenzetu wanapokuja hapa? ua wanafurahia kupiga nao picha tu? ...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji
Kwa Ma pro CCM kwao kila kinachofanywa na CDM ni sio utaifa na kila kinachofanywa ama kuagizwa na CCM ni utaifa.
Hivi ndivyo walivyosadikishwa na waka sadiki.
Kwa sasa wanapinga Judiciary Commetee Kwa Sababu tu ni wazo la CDM
Lakini Siku JK akikubali kuunda hiyo tume basi mi Pro CCM itamiminika humu kumpongeza kwa kuonesha utaifa.
Si unakumbuka Suala la Katiba Mpya.

My Take

Siku JK akiamka na Wazimu akasema kuanzia leo kutembea na nguo marufuku na mnatakiwa kutembea uchi, nakuhakikishia mi Pro CCM itakuja Speed hapa Kuanzisha Thread Kumpongeza.

Tukiwafananishaga na Misukule wanasema tunawaonea.
 
Last edited by a moderator:
Aliyetuloga anaelekea kushinda maana nionavyo ni mfumo wa kutugombambanisha wenyewe kwa wenyewe mwisho wa siku kila mtu abaki na mkanganyiko wake ilihali wao wanazidi kusonga mbele..
 
CCM ilishachana na utaifa toka enzi za uongozi wa Baba wa Taifa MWL NYERERE, sasa hivi wao kwa chama kwanza , ufisadi ulindwe na chadema isambaratishwe kwa nguvu zote. Huu ndiyo utatu mtimilifu kwa CCM , kwahiyo Mzee Mwanakijiji kuishinikiza CCM ifanye utaifa ni sawa na kusubiria Embe kudondoka kutoka kwenye mti wa Mfenesi
 
Last edited by a moderator:
CCM ilishachana na utaifa toka enzi za uongozi wa Baba wa Taifa MWL NYERERE, sasa hivi wao kwa chama kwanza , ufisadi ulindwe na chadema isambaratishwe kwa nguvu zote. Huu ndiyo utatu mtimilifu kwa CCM , kwahiyo Mzee Mwanakijiji kuishinikiza CCM ifanye utaifa ni sawa na kusubiria Embe kudondoka kutoka kwenye mti wa Mfenesi

Mbona CDM wanaambiwa kuyupa mafenesi kwenge mwembe ni sawa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mzee mwenzangu azimio la Zanzibar lilimaliza kazi ,tangu hapo hakuna wa kwenda kinyume na Azimio hilo na linatekelezwa kwa hari mpya nguvu na speed iliyotukuka. Kwenda kinyume ni kukiuka mashart
 
huyu ndiyo mwanakijiji leo anarusha jiwe huku kesho kule...

zamani nlijua yeye ni msemaji wa CDM kumbe nae mganga njaa. Naona kamkomalia mbowe mpaka mishipa inamtoka akihaha na mithread yake anayoianzisha kuhusu mbowe.
 
Anayejua masharti ya azimio la Zanzibar atuwekee hapa. Naona imekuwa siri kama mikataba ya China.
 
Jamani, hivi sherehe za uhuru, muuangano na sherehe za mashujaa; hizi sio utaifa? Mbona CDM uwa hawashiriki? na sijawahi kuona wanaCDM wakihoji!

Labda watu humu wanadhani dhifa ya serikali inatofauti sana na hizi sherehe zingine za hapa nchini, ukweli ni kwamba hakuna tofauti, kwani dhifa ya serikali ni kwa ajili ya kutengeneza mahusiano miongoni mwa viongozi wakiwa wanapata chochote mezani, that's it.

Na wala msidanganyike kuwa kutakuwa na fursa ya mazungumzo ya faragha baina ya Mbowe na Obama zaidi tu ya JK kumtambulisha Obama kwa Mbowe.

Sipendi kuona watu wanapotosha wakiwa kwenye jukwaa hili, sikupenda kujibu chochote ila sipendi vile vile kuona upotoshaji.

Kusema dhifa ya serikali ni UTAIFA ilhali hata namna ilivyo andaliwa tu ilikuwa sio halali. Kitendo cha mchujo wa viongozi tu kimeondoa hadhi ya neno UTAIFA.
 
Back
Top Bottom