Swali: Kwanini wanamuziki wengi wanaimba nyimbo za mapenzi zaidi?


MTV MBONGO

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Messages
1,024
Likes
799
Points
280
MTV MBONGO

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2016
1,024 799 280
Msanii ni kioo cha jamii, nakubali. lakini, kwanini kioo hiki kinaangaza mapenzi zaidi? mbona mada za kuimbwa ni nyingi? elimu, ajira, amani n.k kuna nini ktk mapenzi? tena unakuta misong mingine ya mapenzi matusi kibao. KULIKONI!
 
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Messages
2,189
Likes
1,978
Points
280
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2013
2,189 1,978 280
Mapenzi yametawala dunia. Yanagusa kila mwanadamu bila kujali umri, jinsia, cheo au hali yake kiuchumi. Yaani Tajiri na masikini, wapiga kura na wapigiwa kura n.k. watakimbizana wee lakini mwisho wa mbio zao watagota kwenye mapenzi. Na mapenzi yana uwanja mpana zaidi ambako waimbaji pote duniani wanapata mashairi bila kikomo. Na kwa vile muziki siku hizi ni biashara tofauti na zamani ndiyo maana unaona watu wengi wanaimba sana kuhusu mapenzi kwa sababu mapenzi yanamgusa kila mmoja na kwa maana hiyo huko kuna biashara inalipa.

Binafsi ukiniuliza napenda nyimbo zipi kati ya nyimbo za mapenzi na zile zinazohusu siasa nitakwambia napenda zaidi za mapenzi. Na hisia za mtu hazivutwi kwa kamba au mnyororo.
 

Forum statistics

Threads 1,235,802
Members 474,742
Posts 29,236,346