Swali kwa watangaza NIA.

Swali kwa watangaza NIA.

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Nimeona swali langu liwafikie kwa njia hii maana nashindwa kufika mnakotangazia nia ama nikifika sipewi nafasi kwakuwa mimi siyo mwandishi wa habari. Swali langu ni hili:

''je una mikakati gani ya kuleta usawa unaokaribiana wa kimaslahi baina ya watumishi wa umma ili walimu na madaktari wapate mishahara mikubwa kuliko watumishi wote kwakuwa ni idara isiyo na marupurupu?"

Hivi juzi DC wa Kinondoni ametangaza kutoa 75% ya mshahara wake kumapa mawakili wawasaidie wanaodhulumiwa viwanja. Hii ni dhahiri kuwa kuna watumishi wananeemeka kiasi kwamba allowance walizonazo mishahara kwao siyo kitu cha muhimu huku watumishi wengine wakitegemea tu mshahara kiduchu hata kwa mwezi hauwatoshi. Nina imani litajibiwa na kutekelezwa.
 
Mkuu,

Watangaza nia watakujibu ----- tuu..

The world is always not equel...
 
mkuu swali la msingi sana hili. na nyongeza yake ni hii ifuatayo: je rais mtarajiwa atafanyaje ili kuhakikisha mishahara kwa watumishi wa umma inatolewa kwa usawa kwa kufuata level ya elimu badala ya aina ya kazi? mathalani kwa nini bodi za mishahara zisitoe mishahara kwa kuangalia level za elimu?kwa mfano mtu mwenye degree alipwe sawa kwenye kada zote....
 
kwani mshahara wa dc ni shilingi ngapi?

mie sijui ila inaonekana hadi mtu anatoa robo tatu ya mshahara wake kusaidia wengine it means hategemei mshahara kuendesha maisha yake na familia yake.
 
Hili swali halijibiki kirahisi labda umpate nguri na kinara wa Maswali na Majibu Stephen Wasira ambaye pia ana uwezo wa kusimamia.
 
Hili swali halijibiki kirahisi labda umpate nguri na kinara wa Maswali na Majibu Stephen Wasira ambaye pia ana uwezo wa kusimamia.

Wassira amechanganyikiwa na mafuriko ya Lowassa hadi anaongea kwa jazba!
 
Back
Top Bottom