swali kwa wataalamu wa physics na science kwa ujumla

swali kwa wataalamu wa physics na science kwa ujumla

Mbeky

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
672
Reaction score
520
Hivi wadau ukipiga risasi hewani juu huwa inarudi chini au inapotelea hewani na kama inarudi chini huwa inadondokea pale ulipo au sehemu nyingine na vipi madhara yake ikirudi chini maana nachojua mimi what goes up must come down
 
Mkuu inategemeana ume shoot vertically au at a certain angle. Na je kuna any resistance kama wind, misitu etc. Lakini risasi ituayo ni hatari pia ndio maana inashauriwa kijaribu silaha mahali pasipo na watu. Ungekuwa una idea na projection ningekucholea ma trajectory then tu calculate velocity itakayotua nayo kama iliondoka na speed x m/s na imepigwa ktk angle y na ilikaa hewani muda t
 
Itategemea na projection utakayoitumia,hapo pia itategemea na velocity,trajectory n.k jaribu kusoma topic ya projectile
 
Risasi ukipiga juu inakwenda mpaka inafikia 0m/s hapo ndipo inapogeuka na kurudi chini, huja kwa kulingana na uzito na umbali ilioenda, ni sawa na jiwe ukirusha juu mpaka likafika sehemu linashindwa kwenda juu zaidi kisha linarudi chini kwa spidi kulingana na uzito na umbali lilioenda.

Pia kwa swala la kurudi pale pale inategemea na angle, kama ukiweza kupiga 90 degrees kamili basi itarudi pale pale ulipo
 
Wabongo bana swali la msingi sana unamtuma mtu arudi kusoma "projectile"!
Imagine yule bibi yako au yeyote asiyejua A wala Z angekuuliza swali kama hilohilo ungemfanyaje ili aelewe??
use simple language tu express complex ideas! Ndo maana wasomi wetu wana shida sana..wamejijaza theories na kukariri formulas nyingi ambazo hawawezi kuzi apply maishani! Si walaumu sana kwa sababu Mfumo wa Elimu umewafanya wawe hivyo! (Watch a Movy: "3 i.d.i.o.ts")! Hii imenikumbusha one of my classmate in the History Class alipotakiwa kudefine "DEVELOPMENT" jibu likawa "Development is a development"!Hahaaa, leo naye ni mwalimu: Oooh poor Tz!:bored:
 
Ikipigwa juu lazima itarudi baada ya kuishiwa nguvu ya kushinda nguvu ya uvutano(acceleration due to gravity)
Maana escape velocity ya risasi haiwezi kuifikisha kwenye geostation(mahali ambapo vitu hutulia angani bila kwenda juu ama kurudi chini-hapa ndipo satellite huwekwa)ama zaidi ya geostation(hapa ukirusha kitu chini kinakuja mpaka duniani,ukirusha kitu juu hakirudi chini,kinaenda kimoja.)

Risasi ikirudi haitakuwa na madhara ya kuua mana nguvu yote itakuwa imeisha na kubakiwa na nguvu inayotokana na uzito na gravitation force.

MAJIBU HAYA NI KUPIGA JUU.

Regardless of 90 angle bado kuna uwezekano wa kitu kurushwa hewani kisirudi kama escape velocity(spidi ya kuondokea)
Itaweza kushinda nguvu ya uvutano na air resistance mpaka kufikia geostation,Japo kivitendo hakuna kitu kilichowahi kurushwa kikafika geostation bila msaada wa engine kama wafanyavyo NASA-USA,URUSI,IRAN,NORTH KOREA,CHINA NA S.KOREA
 
Wabongo bana swali la msingi sana unamtuma mtu arudi kusoma "projectile"!
Imagine yule bibi yako au yeyote asiyejua A wala Z angekuuliza swali kama hilohilo ungemfanyaje ili aelewe??
use simple language tu express complex ideas! Ndo maana wasomi wetu wana shida sana..wamejijaza theories na kukariri formulas nyingi ambazo hawawezi kuzi apply maishani! Si walaumu sana kwa sababu Mfumo wa Elimu umewafanya wawe hivyo! (Watch a Movy: "3 i.d.i.o.ts")! Hii imenikumbusha one of my classmate in the History Class alipotakiwa kudefine "DEVELOPMENT" jibu likawa "Development is a development"!Hahaaa, leo naye ni mwalimu: Oooh poor Tz!:bored:

Sasa wewe na ambaye kamwambia mwenzie akasome projectile mna tofauti gani? Kwanza hujajibu swali na pili umetoa mfano wa History. Usihukum na ww hutahukumiwa.
 
Hivi wadau ukipiga risasi hewani juu huwa inarudi chini au inapotelea hewani na kama inarudi chini huwa inadondokea pale ulipo au sehemu nyingine na vipi madhara yake ikirudi chini maana nachojua mimi what goes up must come down

Just to ans your question, a bullet fired up will give up to Wind resistance and Earth's Gravity which pulls everything down and begin falling. Its just like what Mshinga said. You've reminded me of a show called 'Mythbusters' ilikua inaoneshwa discovery channel, walikua wanatest if its possible for a falling bullet to kill maana there was a reported case of some1 killed by it! They were very thorough and established that while it may injure you killing you is highly unlikely. Search "mythbusters-falling bullets' or somethng on YouTube utapata loads of good things!!
 
Last edited by a moderator:
Risasi ikirudi haitakuwa na madhara ya kuua mana nguvu yote itakuwa imeisha na kubakiwa na nguvu inayotokana na uzito na gravitation force.

Asante sana madau kwa ufafanuzi huo maana kila siku nilikua najiuliza hivi hizi risasi zinzopigwa hewani huko libya au nchi zingine za kiarabu wakati wanashangilia ushindi wa jambo lolote mbona hazileti madhara kwa watu zikirudi chini. Leo umenipa maalifa mapya.
Kweli hakuna kisichowezekana au kupatikana JF asante
 
Nawashukuru wote kwa majibu yenu mazuri, Nami nimeondoa ujinga katika hili, God bless you all God bless JF
 
Hii umenikumbusha yale masuala ya projectile form 5 kwenye physics

topic nilikuwa siipendi aisee daah... Afadhali chuon sikusoma mechanical.... Kulikuwa na swali necta walikua wanalipenda la simple harmonic motion eti assume dunia imetobolew tundu katikati na hilo tundu limetokea upande wa pili zen unarusha mpira katika hilo tundu...... Zen unaambiwa kalikuleti nini sijui..... Daa ilikuwa kero sana. Aheri ya Kirchhoffs laws of electrical circuit zilikuwa tamu na zinasovika
 
Mkuu inategemeana ume shoot vertically au at a certain angle. Na je kuna any resistance kama wind, misitu etc. Lakini risasi ituayo ni hatari pia ndio maana inashauriwa kijaribu silaha mahali pasipo na watu. Ungekuwa una idea na projection ningekucholea ma trajectory then tu calculate velocity itakayotua nayo kama iliondoka na speed x m/s na imepigwa ktk angle y na ilikaa hewani muda t
Umenikumbusha PROJECTILE MOTION mkuu
 
Hakuna risasi inayoenda straight line(except in vaccuum). Ndio maana hata sights(vilengeo) vinawekwa juu ya mtutu wakat risasi inapita ndani ya mtutu kuelekea kwenye lengo(ndio usishangae).

So never risasi hata iweje haiwezi rudi pale imetoka iwe 90degree ama vyovyote. Zaidi nenda hapa www.idahohuntingcourse.com nenda kwenye topic 3(firearms and their ammo) utaelewa zaidi
 
Hivi wadau ukipiga risasi hewani juu huwa inarudi chini au inapotelea hewani na kama inarudi chini huwa inadondokea pale ulipo au sehemu nyingine na vipi madhara yake ikirudi chini maana nachojua mimi what goes up must come down
Ikipigwa kwa mstari ulionyooka( vertically) kwenda juu itarudi na kuleta kibondo au pigo( impact ambayo ni Ft=mv2 -mv1 ambapo mvi ni zero kwenye point ya juu kabisa) kubwa kutegemeana na kimo ambako risasi itaishia mwendo wa kwenda juu. ikiishia juu zaidi, kibondo kitakuwa kikubwa zaidi kuliko ikiishia chini. sababu ni kuwa spidi yenye mwelekeo( velocity) ya kurudi chini inaongezeka jinsi muda na kimo kinavyoongezeka hivyo v2 inakuwa kubwa kama kimo au h ni kubwa. Ft au badiliko la momentum au impact kubwa ndiyo inaweza kusababisha kifo. Risasi isiponyooka kwenda juu ndiyo inaleta projectile motion ambayo mwendo wake wa kwenda chini unapunguza ule mwendo kasi wa mvutano wa dunia (g) hivyo mv2 kwa kimo sawa na mwendo uliyonyooka inapungua. Mwendo wa kushuka vertical una impact kubwa kuliko wa kushuka kwenye slope kama ni free fall sababu kwenye slope zile v zina gawanywa pande tambarale(horizontal component) pande chini au juu(vertical) hapo sasa trigonometry et.c. anyway maelezo ya juu yanatosha. Haya yote usipotilia maanani mkwamisho wa hewa.
 
Kwahiyo mdau nobo unasema ka itapigwa vizuri au mstari ulionyooka inaweza kurudi na kusababusha kifo ebu meelezo kidogo katika hilo na ka unaushaidi wowowte wa tukio la kifo baada ya risasi kupigwa juu, please husiweke hesabu katika majibu yako oleve Math nina mswaki (F) mi ni kilaza wa hesabu kabsaa
 
Lakini ukumbuke hizo risasi zikipigwa juu hapa Tanzania zikirudi zinaua au kujeruhi hasa katika mikutano ya Kisiasa ya vyama pinzani au mapambano baina ya polisi na watuhumiwa wa uhalifu!:noidea:

Back
Top Bottom