Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Hebu fikiria umesoma hadi umemaliza Elimu ya chuo
Ukakutana na jamaa mmoja ambae mnaanzisha uhusiano
Baada ya kuanzisha mahusiano na huyu jamaa ulifanikiwa kupata ajira na maisha yenu ya mahusiano yaliendelea vyema sana
Lakini baada ya miezi 6 ulipata maradhi ambayo yalipelekea kukuweka kitandani kwa mwaka mzima na huyu jamaa alikuwa bega kwa bega na wewe na alitumia kila uwezo wake kukutibu na ilifikia hadi alikupeleka South Africa kwaajili ya matibabu,baada ya huo mwaka ulipona
Lakini kutokana na ugonjwa uliokuwa nao ilikubidi ukae nyumbani kwa mwaka mwingine ili urudishe afya yako iliyokuwa imeporomoka kwa sababu ya ugonjwa
Baada ya huo mwaka wa kurudisha afya jamaa yako akakuomba usianze kutafuta kazi kwanza ili mpate muda wa kukaa pamoja na zaidi sana mfanye mipango ya kufunga ndoa,ukakubali
Mlifanikiwa kufunga ndoa na kwa muda wote wa huo mwaka na nusu mlikaa kwa amani na furaha na hakuna ulichokuwa unakihitaji kutoka kwa mumeo ambacho alikuwa na uwezo nacho ulikikosa,kwa kifupi uliifurahia ndoa sana tena sana
Baada ya muda huo ulimuambia kuwa ni wakati wa wewe kujishughulisha
Hapo ndipo anakuomba kuwa huna haja ya kutafuta kazi kwani kila unachokihitaji unakipata
Je ingekuwa ni wewe ndio mke wa huyo jamaa ungeamua nini na kwanini?
Karibu .................!!