CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,827
- 1,858
Hata Mataifa yaliyoendelea tumesikia mara kadhaa viongozi wakitumiwa kwa rushwa, matumizi mabaya ya ofisi, kudorora kwa uchumi. n.k. Kwa hiyo mkuu serikali yoyoye inayoongozwa na Binadamu ina mapungufu yake. Hauwezi kuwahukumu wanaoipenda CCM kwa kuangalia matatizo ambayo ni ya kawaida kwa binadamu. Hii ni hoja mfu kuliko zote nilizowahi kuona humu Jf. Eti unauliza swali wanaoihusudu CCM wakati wewe ukiulizwa unakihusudu chama kipi na kwa nini , sidhani kama una jibu kwa vile hakuna hata kimoja zaidi ya CCM kilichothubutu kuongoza serikali hata kwa sekunde tukaona kama viongozi wake wakuwa kama IDD AMIN aliyekuwa akimpenda mke wa mtu anachukua bila hata uoga, kama viongozi wake hawataishia kusaliti ndoa zao na kwenda DUBAI sasa tena mchana kweupe na kusahau kuwa wako kwa ajili ya kuwatumikia watanzania, kama viongozi wake hawatakuwa wa vurugu na kero kibao kwa watanzania.
Mkuu waache watanzania wajivunie chama chao, chama chenye kuwaleta pamoja badala ya kuwagawa kwa mtindo wa umajimbo, ukabila na udini.
Unaweza kuona hayo ni matatizo yaliyosababishwa na CCM kama ambavyo walibya walivyolewa amani, utajiri na kumuona Ghadaffi hafai tena kwa musukumo wa wabaya wa LIBYA, leo hii wanatamani bila mafanikio afufuke mzee wa watu angalau awaonjeshe analau ule utamu waliokuwa nao enzi za uhai wake.
Mi kweli watatizo yapo nchi nyingi je umesikia nchi hizo mafisadi na wabadhirifu wanaombwa waache wizi wa mali ya umma? Ambapo Rais anadai anayo orodha ya wezi wa mali ya umma huku hachukui hatua yoyote badala yake ni kupanga tu safari za nje ya nchi?