Mimi kama mke wa ndoa baada ya utambulisho ningempa mume mkono na kumwambia Glad to know you kisha nauchuna kimya kama siyo mimi vile.
Umeona eeh hakuna haja yakugombana na mdada wa watu kisa gubegube.
Kumkomesha kabisa au? Unaweza ukasababisha asiondoe hata gari!
Simkomeshi jamani si yupo na GF wake sasa mimi mgeni nitasema nini,na tukifika home naweza nisimuulize vilevile.
Ukifanya hivyo hakika atatokwa jasho na aweza hata kusababisha ajali msifike nyumbani...! Mental torture hiyo..!
Simkomeshi jamani si yupo na GF wake sasa mimi mgeni nitasema nini,na tukifika home naweza nisimuulize vilevile.
Easier said than done...!
Uko sahihi, wanaume wengi hutoa visababu kwa wake zao wanapohitaji huduma. Kwa michepuko wapole kweli. Ukimfumania kama hivyo atafanya kila utakachomwambia!
Ningeuambia mchepuko ushuke kisha naondoka na wife.
Hahahaha!! Sasa ajali ya nini wakati yupo na kitulizo chake, kwanza mimi naona bado tu ananithamini kanipa hela ya tax kwenda na kurud, hakuniacha nipalamie daladala, still loving me no means of fighting, yaani naweza nisimuulize vile vile hata tukifika nyumbani.
natulia tu mimi si nimepewa lift bwana
Rahisi sana kusema mtani. Reality ni tofauti kidogo...!
honey faith pokea like yangu kuanzisha timbwili barabarani haifai utaonekana busara chache na kudhalilika zaidi kwa sababu watu watajua mume wako asivyokuthamini lakini pia kasha kudhalilisha kwa mchepuko ni kutulia tu hadi home ndiyo unacheza utakavyo uwanja wa nyumbani tena lazima pachimbike.ningetulia tuli hadi nifike nyumbani ndio ningejua huo mziki niucheze style gani