Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,485
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitasubiri wanachama watakaoachwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.
Kutokana na tamaa ya kuingiza watu wengi kwenye Bunge, vyama vya upinzani vimekuwa na tabia ya kuwapokea wanachama wa CCM wanaoshindwa kwenye kura za maoni na baadaye kuwapa nafasi ya kugombea ubunge, lakini Dk Slaa anasema safari hii hawatakuwa tayari kufanya hivyo.
"Tulishasema kwamba kwa ngazi zozote hata ngazi za udiwani au ubunge hatusubiri mabaki, makapi yatakayotokea CCM ndiyo yaje kwetu," alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?
Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?
Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
Hii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!
Pitia hapa,
Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,

Mkuu,Demokrasia ya kiAfrika inajengwa kwa kuhama vyama. Mfano Kenya, Nigeria, Malawi n.k
usijidanganye kuwa chadema ina malengo ya kweli ya kumkomboa mtanzania. chadema inachoangalia ni masilahi. huoni wanavyofurahia kupokea wale wanaokatwa/kuogopa kukatwa huko ccm? inasemekana mpaka sasa mbowe keshavuta bil 10 kutoka kwa lowasa, tatizo linakuja kwa slaa aliyemtangaza pale mwembeyanga kuwa lowasa ni miongoni mwa wale mafisadi wakuu 11 katika nchi hii. je slaa atakula matapishi yake? hicho ndo kikwazo. vinginevyo dili limekamilia.
Mwanakijiji
Alikuwa anapiga madongo kweli Lowasa alipokuwa anagombea CCM. Sasa the ball is in your court. Sijui utatoka na calculus ya aina gani.
Hoja yako ni ya msingi.
Hata hivyo, katika siasa sio lazima iwe hivyo wakati wote.
Kwa kutaja wachache tu;Dr. Slaa alikatwa CCM enzi hizo na akatimkia CHADEMA. Hivi sasa huko ameshakuwa lulu.
Inawezekana pia hata kwa wengine ikawa hivyo hivyo, jambo la msingi ni kuangalia nia ya dhati awe "mhamiaji halali" si
"mhamiaji haramu..."
Aah.. mimi tena; mbona nilishasema kwenye ile makala nyingine. Ila kuna upande mwingine unahitaji kutafakari. Je, akitaka kujiunga kama mwanachama wa kawaida naonaje? Na akiwa mwanachama wa kawaida akachangia mno katika kuiondoa CCM madarakani niseme nini?
Kwa zaidi ya miaka 7 sasa viongozi wa CHADEMA wametuaminisha kuwa wanapigana na ufisadi na wakaenda mbele zaidi kwa kutaja majina ya watu wanaowaita ni mafisadi, Lowassa mmojawapo. Leo hii tunaposikia kuwa Lowassa yuko mbioni kwenda CHADEMA na Chama kinakaa kimya bila kukubali au kukanusha hizo taarifa ni dalili ya giza!
Na haingii akilini kuwa miaka yote hiyo CHADEMA hawakuwa wamejiandaa kuhusu mgombea urais!
Mkuu,
Sio demokrasia za Africa pekee hata Ulaya.
Tumeona chaguzi nyingi za Uingereza ambapo mbunge wa chama anahama na kwenda kugombea chama kingine na kushinda.
Hii mara nyingi inatokea ambapo anayehama anatoka kwenye chama kikubwa na kwenda chama kidogo.
Viongozi wa CHADEMA walitoa kauli ya 'makapi' kwa sababu nadhani waliamini CHADEMA kwa sasa ina uwezo wa kupata wagombea wazuri bila kutegemea mgombea kutoka nje.
Hoja yako ni ya msingi.
Hata hivyo, katika siasa sio lazima iwe hivyo wakati wote.
Kwa kutaja wachache tu;Dr. Slaa alikatwa CCM enzi hizo na akatimkia CHADEMA. Hivi sasa huko ameshakuwa lulu.
Inawezekana pia hata kwa wengine ikawa hivyo hivyo, jambo la msingi ni kuangalia nia ya dhati awe "mhamiaji halali" si
"mhamiaji haramu..."
Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?