Mbona ndoa raha sana tu !!
sema tatizo ni kwamba, mabaya ya ndoa yanavumishwa na wasio wanandoa. Yaani mtu asie dereva anaelezea jinsi ya kuendesha gari !!
Ukiwa kwenye maisha ya NDOA inatakiwa ujue kwenye Nafsi ya mwenzawako kuna maSHUJAA waWILI yuko shujaa Mzurina shujaa mBAYA sasa mnapokuwa mnaishi ni uamuzi wako kumuamsha 1 wa mashujaa hao! atakaeamka ndo atakuletea matokeo ya NDOA yako!
Faida za ndoa ni chache sana binafsi nipo kwenye ndoa mwaka wa tano! Ndoa ipo kiimani na kidin zaidi kama utaratibu wa maisha ndoa ndo chimbuko la kizazi bila ndoa tutapata kizazi kisicho na maadili! Wakatoliki ndoa ni sakramenti tena takatifu kuishi bila kuchafua hekalu la roho mtakatifu(mwili) ila mtume paul anawaasa wanadamu kwamba maisha ya useja/utawa humfrahisha mungu ila km mtu hayawezi maisha hayo ni bora aoe au kuolewa kulikoni kuwaka tamaa! Mungu aliona si vema adamu aishi peke yake bila msaidizi(mwanamke) alimpa kila kitu lkn akaona hakuna kiumbe kinachomfanana na adam mke mwema au mume mwema ni campany tosha sana. ndoa inajenga heshima ndan ya jamii pia inakushape kitabia huwezi kula ovyo kila sehemu huwezi kulala kokote km muhuni! On the contrary ndoa inaöngeza majukumu hasa mkipata watoto. Watoto watahitaji pa kulala chakula elimu malezi nk unapanua undugu nao wanaongeza changamoto! Si lazma kuoa au kuolewa ndoa ni taasisi ngumu sana inabidi uwe na uvumilivu mkubwa na upendo wa dhati na mungu akupe mwenzi mnaendana
Ndoa ni nzuri hasa ukiolewa/kuoa na unaempenda. Nataka nikuambie kuna raha wakati wote . Mimi ni mwanandoa so ninachokwambia ninakiishi. Kama imetokea umesoma thread kadhaa zinazozungumzia ndoa vibaya bas naweza kusema imetokea bahati mbaya tu , ni one side story. Ingawa ni kweli kabisa zipo baadhi ya ndoa ni chungu na hata ukiziona kama hujaingia kwenye ndoa hutaitamani ndoa hata kidogo kumbuka kuangalia upande wa pili wa shilling. Zipo ndoa zingine nazo ukiziona utajilaumu na kusema umechelewa wapi kuingia kwenye ndoa kama ndoa zipo hivi. Kama nilivyosema ndoa ili iwe nzuri inahitaji sana uangalifu kabla hujaamua kuiingia. Nasema haya kwa sababu ndoa ni muunganiko wa watu 2 wenye nia na lengo moja sasa ikiwa hamko pamoja kimtazamo lazima ndoa iwe ndoano.
Ningekuwa sijaoa nisingeoa tena, kwani mie ni mkatoloki nilioa dada mmmoja wa magorofani Ilala mwaka 1999, mama kumbe ni kicheche hadi leo! nimekanya, nimesema, nimepiga karibu kuua umalaya upo pale pale!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.