Swali kwa walioko kwenye mahusiano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa walioko kwenye mahusiano!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by idea, Sep 29, 2012.

 1. idea

  idea Senior Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 120
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mpo kwenye mahusiano taklibani mwaka mmoja. Mwanzoni mambo yanakuwa mazuri na Mungu anawajalia mnapata mtoto japo ndoa bado. Mara vitimbwi vinaanaza kutoka kwa mmoja wapo lakini mwenzie anakaa kimya tu akiendelea kusoma mazingira. Hatmaye yule aliyeanzisha vitimbwi anaamua kumwambia wazi mwenzie kuwa amemchoka na hataki kumuona tena kwenye uso wake hivyo afunge virago na kuondoka. Mwenzake aliye kuwa kimya muda wote akajibu kuwa laiti ungejua kuwa nami nimekuchoka, natamani kuondoka hata sasa hivi? Je kama wewe ungelikuwa ni mtu yule aliyeanzisha vitimbwi ungejisikiaje?
   
 2. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ajisikieje vipi na hali yeye ndio kalianzisha?..ukitaka kukimbia agana na nyonga kwanza..lol!
  Halaf mbona imekaa kama inakuhusu vile?..hebu tiririka vizuri usaidiwe..unavyoileta kimfanomfano wakati labda inakuhusu hutapata majibu sahihi!!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Mifano yenyewe migumuuu kama parables za Jesus!
  Unapojibu 'laiti ungejua na mie nilivyokuchoka. . . .', unamaanisha ndo bado upo-upo sana ama?
   
 4. data

  data JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,801
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  Vitimbwi gani? dadavua... Na hii ni yako mwenyewe
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kumbe hata wewe umeona eh...!
  Kwa kawaida kama mtu wako kakwambia amekuchoka halafu wewe ukamwambia hata mimi pia nilikuwa nimekuchoka na nilikuwa natamani kuondoka, atakuona kama wewe si mwehu basi akili yako ina walakini... mtu anakufanyia vitimbi ili uondoke, lakini unang'ang'ania tu, kaona humuelewi akaamua kukupa ukweli, halafu eti ndo na wewe unajibu kuwa ulikuwa unasubiri "go ahead" ili uondoke, sasa kama huo sio wehu ni kitu gani..!
  tena huyo anakupenda mwingine akiona kila akikufanyia visa huondoki, anakuwekea sumu ufe ili umuondolee kiwingu.. lugha ya vitendo huioni hata kauli nazo unazifanyia ajizi....! wewe kweli ni king'ang'anizi..

  Kwa faida yako hebu soma huu uzi hapa chini unaweza kukusaidia:

  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/315418-tuache-ung%92ang%92anizi.html
   
 6. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Funguka zaidi kabla ya akina Mtambuzi hawajuvutwa na mama ngina wao ukose ushauri murua. Halafu ushauri mzuri ukiwa umeweka kitu kichwani utafurahi mwenyewe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,216
  Likes Received: 10,579
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu..huo ni upepo utapita.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimpe na hiki kisa cha mwendawazimu mmoja aliyekuwa na tabia zinazofanana na huyo aliyechokwa hapo juu:

  "Florida nchini Marekani mtu mmoja ambaye anaonekana alimchoka mkewe kupindukia na pengine kila visa alivyomfanyia kugonga ukuta, aliamua kufanya kisa ambacho kiliacha gumzo. Mtu huyo baada ya kuona mkewe anajifanya anajua sana kupenda na hivyo kutojali visa vyake aliamua kufanya kisa kikubwa zaidi.

  mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Teddy Akin alimwambia mkewe kwamba amemuuwa mtu ambaye alimuomba lifti na kumzika porini. mume huyo alitoa pochi na kumwonyesha mkewe akimwambia kwamba, baada ya kumuua mtu huyo alichukua pochi yake. ni kweli pochi hiyo ilikuwa ni ya mtu fulani na ilikuwa na vitambulisho vyake na nyaraka nyingine pamoja na pesa. bila shaka alimwambia mkewe kwamba, yeye (mume) kuuwa kwake ni kawaida akiamua.

  Kuona hivyo mke wa jamaa aliripoti kwa Polisi ambao walifika na kumtia mikononi Teddy Akin. hata alipofikishwa polisi bado aliendelea kusisitiza kwamba alimuuwa mwenye pochi ile na kuichukua. hii yote ikiwa ni juhudi yake kumfanya mkewe yule king'ang'anizi ajue na kuamini kuwa anang'ang'ania muuaji.

  alisema bele ya Polisi na mkewe kwamba, alimuuwa mtu huyo kwa kumpiga kiswasawa shingoni na kwamba baada ya kufanya hivyo, mtu huyo kabla hajafa alivutia roho kwa kutisha na kutoa sauti yenye kugumia vibaya. Alisema yote hayo ili kumtisha mkewe aone kwamba, yeye ni muuaji hasa, ili mke huyo afanye uamuzi wa kuondoka amwache huru.

  Lakini kabla kesi hiyo haijapelekwa mahakamani, polisi walibaini kwamba, mtu aliyedaiwa kuuawa na jamaa huyo alikuwa salama na mzima wa afya. mtu huyo alipopewa taarifa kwamba alikuwa ameuawa alishangaa sana. Aliwaambia polisi kwamba, pochi yake ilikuwa imeibwa siku mbili tatu nyuma..............

  Polisi walipomhoji Teddy sababu ya kufanya hivyo alidai kwamba baada ya kuokota pochi ya mtu huyo aliamua kufanya jaribio hilo ili kumtisha mkewe kwamba yeye ni muuaji hatari ili mke huyo aondoke, baada ya mbinu kadhaa kushindwa kufanya kazi. polisi walishindwa kumuelewa, wakamwambia mkondo wa sheria utafuata njia yake................"
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  "Be a change you want to see"

  Hii signature yako ina jibu zuri sana
   
Loading...