Swali kwa Samwel Sitta na S. Wassira

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,210
Baada ya kuwa nje ya system kwa muda wa siku 100 sasa ninahakika mnashuhudia jinsi rais wa awamu ya 5 wa HAPA KAZI TU anavyojifanyia mambo tofauti kabisa na yale aliyokuwa akiyafanya yule wa mtandao wenu wa awamu ya 4. Na hapo bado hatujajua atakayekuja katika awamu ya 6 atakuja kwa staili gani.

Hivi mpaka sasa bado mnaamini ktk misimamo yenu ya hovyo ya katiba ya Chenge iliyopuuza maoni ya wananchi? Au sasa mmekuwa kama shabiki wa bao, mnaliona zaidi kuliko wachezaji? Hiyo 50% kwa 50% kwa akina mama katika uongozi ikowapi? Katiba hii si sawa na ile mliyoichonga? Mlijiaminisha kuwemo katika kuipitisha katiba pendekezwa mkijifanya nyie ndio serikali, sasa mko wapi?

Mmeshuhudia Wateule wataalam wanavyoweza kuondolewa na wanasiasa bila kufuata utaratibu unaoeleweka. Je akija raisi Mpuuzi, asiye mzalendo, fisadi, mwizi si anaweza kutujazia wezi tena katika serikali?

Akija wa kung'ang'ania madarka kama sinema ya ZEC sisi wananchi tufanyeje ? Kilicho wafanya muondoe kipengele cha maadili katika katiba ni nini hasa?

Samweli Sitta uliambiwa mfumo wa uteuzi ubadilike, wewe ukapinga. Uliacha umeteua bodi ya mamlaka ya bandari, leo imetumbuliwa wewe unaanza kupiga kelele, sindio hayo tuliyokuwa tukisemea wewe unatukejeri?

Nataka hili liwe fundisho kwa viongozi mliomadarakani sasa, mkae mkijua na kufanya maamuzi kwa mtazamo wa mbele sio kuangalia usawa wa pua tu. Leo ni nyie ni viongozi, kesho wapiga kura kama sisi. Badilikeni tutengeneze katiba inayoeleweka na kuleta heshima kwa Taifa.

Wapiga kelele wengine ambao nahakika walikuwa wakitetea wasiokijua ni: Saidi Mkuba, Aden Lage, Mchimbi, Asumpta Mshama, Amina Chilolo, Ana Kilango, Blandes, Tizeba, Kapuya, Anna Abdala, Gaudensi Kabaka, AG Werema, na wengine wengi. Tafadhali badilikeni njooni UKAWA tudai katiba sahihi.
 
umeandika vizuri mwanzo ila kwenye umaliziaji umeingia chaka.....waambie waende ACT WAZALENDO aU waanzishe chama chao
 
Unawapandisha B.P. Wengi wao wana majipu ya madudu waliyofanya awamu iliyopita. Huyo s 6 pale bandarini tusubiri tutasikia
 
Umekosea sana kumwita sitta aje ukawa, umenifanya nikudharau na wewe mwenyewe, toka lini sitta anaaminika?
 
Umekosea sana kumwita sitta aje ukawa, umenifanya nikudharau na wewe mwenyewe, toka lini sitta anaaminika?
Kwenye Biblia, katika mafunzo ya Yesu Kristu, au Nabii Issa, yategemea wewe ni muumini wa dhehebu gani; wanafunzi hawakumuelewa Yesu kwa kumruhusu kahaba kumkaribia, kumbusu miguu yake na kuiosha kwa machozi na kuipangusa kwa nywele zake. Yesu alipoona hivyo aliwatolea mfano wa watu wawili waliosamehewa madeni, mmoja alisamehewa deni dogo na mwingine akasamehewa deni kubwa, akawauliza kati ya hao nani ataona katendewa vyema zaidi, wanafunzi wakasema aliyesamehewa kikubwa. Pia akawaambia mwenye AFYA hamuhitaji daktari.

Kamwe, usiangaike na wanaokuelewa haraka na wenye msimamo kama wako. Daima pambana na wenye matazamo tofauti, nao wakikuelewa watakuwa wapambanaji hata zaidi ya wale ulionao. Ukiweza badilisha kada mmoja, tena aliyekubuhu kutoka CCM kuja UKAWA unakuwa umefanya jambo jema saaaana.

Mfano; Kitendo cha kumbadilisha Lowasa, Sumaye, Kingunge, Mgeja, Msidai, Olemedeye, Esta Bulaya, James Lemebeli, Mahanga, Masha n.k kiliidhoofisha sana CCM.

Hawa nao niliowataja, wakivuka mstari wakaja, inamaana somo linakuwa limeeleweka zaidi na watasidia zaidi katika mapambano.

Kama unafahamu vizuri Biblia inasema Mtume Paul ambaye ndiye Saul, alikuwa mfarisayo mkatili sana kwa wafuasi ya Yesu Kristu, lakini alibadilika nakuwa mpambanaji na mtetezi na msambazaji mkubwa wa dini ya Kikikrisu.

Ukiweza kutongoza mwana CCM mmoja kwa mwaka na kumlete UKAWA baada ya mika mitano utakuwa umevuta kura 5, nao hao uliowavuta watavuta wengine.

Nadhani sasa umenielewa kwanini najaribu kushawisi vinara wapinga katiba mpya wabadilike waje upande wa watetezi wa rasimu ya katiba ya jaji Warioba, mimi ninao wafahamu ni UKAWA.
 
umezunguka sana, porojo nyingi, maneno mengi kumbe mwisho wa yote ni kwamba ulikua unamwita sitta ahamie UKAWA?, by the way "lowasa kuhamia ukawa haibadilishi ukweli kuwa mzee ni fisadi" vivyo hivyo "sitta kuhamia ukawa haibadilishi ukweli kuwa aliichakachua katba ya wananchi" tatzo mlilonalo wanaukawa ni kuamini kuwa kila aliyeupande wenu ni MSAFI, siku mkijilekebisha ndipo tutakapo wakabidhi nchi, over!!!!!
 
Back
Top Bottom