Maalim Seif Sharif Hamad atangaza kuihama CUF na kujiunga na ACT-Wazalendo

Unajiuliza wapinzani wanafikiri nini?

1. Maana kama Lowassa alipata wafuasi wengi lakini hakuweza leo hii Maalim Seif mwenye wafuasi wengi Zanzibar tena upande wa Pemba pekee ambao hawafiki hata Milioni 1, kujiunga na ACT Wazalendo inasaidia upinzani?

2. Siku chache zilizopita walizindua azimio la Zanzibar sasa hivi wameshaanza kufarakana, kwa upande wa Chadema in Blood CHADEMA Media Chadema Tanzania JE wamefurahishwa na uamuzi wa Maalim Seif?

3. Uchaguzi unapokufikia wapinzani waligawana CHADEMA na CUF hivi sasa wanakwenda kugawana CHADEMA, CUF na ACT wazalendo. Tena ACT wasiopatana na CUF. JE hii sio faida kwa Chama Cha Mapinduzi Ndani ya Bunge?

Hapo ndio utagundua nchii hii hatupo tayari kwa vyama vingi Baba wa Taifa alilazimisha maana wapinzani hawajui wanachokitaka wala wanapokwenda.
 
Huyu profesa alishapoteza mvuto kitambo sana, alipaswa awe mpole atafute suluhu na mwenzake lkn yeye akajifanya mjanja sasa chamoto atakiona. Cuf Zanzibar haina majengo, ofisi zote ni za kupanga au kujitolea kwa wenye nyumba ambao karibia wote wanamsapoti Maalim Seif hivyo Professor anakabidhiwa Cuf ikiwa tupu kazi kwake, na hao wabunge walionao wengi mwakani watasepa na kujiunga na Maalim Seif, ruzuku aliyokua akiipigania itaota mbawa labda amuombe Dr. Magu ampe japo ubalozi atokomee huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom