Ningekuwa dada ningechangia. Ila mi nikigundua wife kazaa na konda na muuza urembo, namwambia kilicho zaliwa ndani ya ndoa ni changu. Nataifisha watoto
Kwa kweli mume atembee tu nje, akizaa regardless kazaa na nani, ni bonge la noma. Sijuhi nita react vipi kwa kweli kwani najaribu kupiga picha inagoma kabisa kuja aisee.
we nae.....kila mtu ana akili yake....mi kwangu kuzaa na baamedi na changudoa haiwezi kulinganishwa na kuzaa na Dr na mhasibu....the risk is not the same....kupima hata daily si tatizo kwangu....:lying:
upo sahihi. Hii kitu imemtokea sista wangu this week. Amegundua mumewe wa ndoa ana watoto wawili nje. Imagine, sista ameumia sana mpaka anatia huruma.
Wanaume plz lindeni ndoa zenu.
Mambo mengi yatachangia katika maamuzi yangu. Mwanaume wa kutembea mpaka anazaa na changudoa na bar maid ina maana huyo ni cassanova na mlevi wa kupindukia - mwanaume wa namna hiyo mke hua anajua tabia ya mumewe. Ndo maana utasikia baadhi ya wanawake wanasema kabisa hadharani kua mm namjua mume wangu ni malaya!
Kama hio tabia ya umalaya tayari ni dhahiri na bado unakaa nae - cha ajabu nini kusikia kazaa na hao wanawake (tena ukute hata kapakaziwa) hakuna haja ya kumuuliza watoto kama bado una nia ya kuishi nae maana utampa sababu ya kuwaleta hapo uwalee. kwa upande wangu tatizo ambalo halina ufumbuzi sioni sababu ya kulifungua iwapo nimeamua kumuacha naondoka zangu, za nini headaches....