Kwenye huu uzi watu wamechangia maoni yao hata hivyo wengi wamekwepa kutoa jibu kama ni uzembe au la.
Nihitimishe hoja yangu kwa kusema mbunge anaetetea kiti chake cha ubunge kushindwa ndani ya Chama wakati wa kura za maoni ni Uzembe.
Nina sababu kadhaa.
1. Wapiga kura wanaopiga kura za maoni ndani ya vyama vya siasa wengi wao kwa asilimia kubwa bado wanasumbuliwa na maadaui wa taifa waliowahi kutajwa na rais wa awamu ya kwanza hayati mwl JK Nyerere hasa umasikini.
2. Democrasia yetu ni Changa ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya Siasa.
3. Rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu hivyo mtu kumpigia kura kiongozi yeyote bila chochote imekuwa ni jambo gumu sana kama kukuta boat imepaki stend ya mabasi.