Swali kwa Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa Dr. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngonini, Aug 7, 2011.

1. N

Ngonini JF-Expert Member

#1
Aug 7, 2011
Joined: Sep 1, 2010
Messages: 2,024
Likes Received: 8
Trophy Points: 135
Dr Slaa, kulikuwa na kasumba iliyozoeleka huko nyuma kuwa jimbo likichukuliwa na upinzani, huwa kuna visasi vinavyofanywa na serikali ya chama tawala vya kutotekelezwa kwa mipango ya maendeleo katika jimbo hilo kwa makusudi ili kuwakomoa wananchi wale. Kwa mfano kuna tetesi kuwa mgao wa umeme Arusha mjini ni mkali kuliko sehemu zingine na watu wanahisi ni kwa sababu ya kuchagua chadema. Je chadema wamejiandaaje kupambana na tatizo hili la serikali ya chama tawala ambalo kwa kiasi kikubwa hutumiwa ili kuzoofisha upinzani?

Sisi wengine tunajua ni wajibu wa serikali kupeleka maendeleo sehemu zote za nchi pasipo upendeleo wa aina yoyote kwa kuwa wanalipa kodi, lakini inapokuja kwenye majimbo ya wapinzani huwa kuna tatizo la serikali kuwasusia wananchi wale.

Pia kwa uelewa wangu, jimbo linaloongozwa na mbunge wa upinzani linatakiwa lifanye vizuri kimaendeleo kwa sababu kutakuwa na matumizi mazuri ya fedha za maendeleo kwa kuwa kuna usimamizi mzuri.

2. MAGAMBA MATATU

MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

#2
Aug 7, 2011
Joined: Jul 2, 2011
Messages: 617
Likes Received: 220
Trophy Points: 60
Hili swali si la kumuuliza Dr Slaa hata mie naweza kukujibu,,umeisha sema ni wajibu waserikali kupeleka maendeleo sehemu zote, na kama inashindwa na kuamua kupeleka sehemu ambako wenyewe wanaongoza hiyo ni dhahili kuwa hii serikali ni ya kibaguzi sana,, ndoo maana hata Ana Kilango
alisema kuwa Ngeleja amewapelekea watu wa Sengelema umeme na amewaacha watu wa Same,, pili taizo la umeme hapa TZ ccm kuliweza ni ndoto tena za panya akiwa ziwani kwani viongozi siyo wabunifu wa maendeleo zaidi ni wabunifu wa kuwaibia WATZ,nawasilisha mkuu!!!!

3. Jilanga

Jilanga JF-Expert Member

#3
Aug 7, 2011
Joined: Feb 13, 2011
Messages: 254
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Naomba kumsaidia Mzee wangu Dr Slaa! Ukiangalia bila kufanya upembuzi yakinifu utahisi hii hoja/kasumba ni ya msingi mathalani tukiangalia Jimbo la Nyamagana-Mwanza matatizo yamekuwa mengi mno baada ya upinzani kumpokonya Mh. Mashe! Lakini si kweli kwani matatizo ya kusuasua kwa maendeleo yanakabili majimbo yote japo Wabunge wa ccm yanayapamba kwa mgongo wa chupa wakidhani wanaimarisha ngome ya chama tawala huku wakikizika bila ya wao kuona haya! Mi nasema heri kuwa na maadui wengi kuliko marafiki wanafiki kama ilivyo kwa baadhi ya MP's wa Ccm!

4. p

politiki JF-Expert Member

#4
Aug 7, 2011
Joined: Sep 2, 2010
Messages: 2,356
Likes Received: 154
Trophy Points: 160
swali lako linamuhusu zaidi ngeleja kuliko slaa kwani swala la ku deliver umeme kwa wananchi linasimamiwa na serikali zaidi kuliko chama cha siasa na kama unachokisema kama ni kweli basi ccm ndio itahathiirika zaidi na mgao huo kuliko chadema kwa maana chadema hawaendeshi Tanesco bali ni ccm. kuhusu upatikanaji wa umeme kulingana na kuichagua au kuitoichagua ccm labda nukuulize vijijini ambapo hakuna umeme kabisa hata wa mgao huko si ndio waliko chagua ccm kwa asilimia 90% nao pia wanakomolewa kwa kuchagua chadema siyo ???

5. b

bulunga JF-Expert Member

#5
Aug 7, 2011
Joined: Oct 24, 2010
Messages: 290
Likes Received: 8
Trophy Points: 35
Kwa hili nitamtetea Ngeleja, huyo mama hamnazo, anasahau wakati wa Cleopa Msuya bara bara umeme vilipelekwa huko milimani, hakuna aliye hoji, aeleze vigezo ambavyo Sengerema haina lakini Same vipo kiasi wao Sengerema wasipelekewe umeme, nilimuona alipokuwa anatoa hoja hiyo kwenye TV huku akiwa amefura na mate kumtoka, Kwa taarifa yake sidhani Same nayopigia kelele ina qualify comparatively na Sengerema

6. KIMBURU

KIMBURU JF-Expert Member

#6
Aug 7, 2011
Joined: Jan 12, 2011
Messages: 210
Likes Received: 10
Trophy Points: 35
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya makali ya mgao wa umeme na kuchagua mbunge wa upinzani coz mimi nipo hapa Iringa mjini ambapo mbunge ni Rev Peter Msigwa kwa wiki ya pili sasa; na toka nifike nimeshuhudia umeme ukikatika mara zisizozidi nne tu. So hoja yako haina mashiko mkuu na usimsumbue rais wetu wa moyoni.

7. Kobello

Kobello JF-Expert Member

#7
Aug 7, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 5,690
Likes Received: 658
Trophy Points: 280
Kwani,kwenye serikali ya halmashauri ya jiji la arusha ni chama gani kina wajumbe wengi?...Nadhani Arusha mjini ni jimbo la CCM,wao ndiyo wenye madiwani wengi na meya wa jiji.
Kwa hiyo,swali linakuwa kama halina nguvu sana.Sorry.

8. s

samoramsouth Senior Member

#8
Aug 7, 2011
Joined: Jan 16, 2011
Messages: 184
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Mm nipo kawe ka halima mdee umeme upo kila siku mara chache sana unakatika. Hoja inaendelea kukosa mashiko.

9. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#9
Aug 7, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,107
Likes Received: 22,163
Trophy Points: 280
Kwa nini ukanda wa Pwani wote (Kaskazini mpaka Kusini na visiwa vyake), Kigoma, Tabora iliachwa bila maendeleo yoyote kwa miaka mingi? Jee, tukisema kulikuwa na ubaguzi wa kidini wa makusudi stakeout? sehemu hizo zinajulikana kwa waislaam kushamiri.

10. N

NasDaz JF-Expert Member

#10
Aug 7, 2011
Joined: May 6, 2009
Messages: 11,308
Likes Received: 1,655
Trophy Points: 280
Hii ni hoja dhaifu miongoni mwa hoja dhaifu fikirika tuanzopenda kuzitoa Watanzania! Why arusha na isiwe Moshi ambako for couple of years now ipo chini ya CHADEMA?!! Why Arusha na isiwe Kigoma ambako CCM haina amani mkoani humo kwa miaka yote ya kuingia kwa upinzani?! Why Arusha na isiwe Pemba ambako CCM haijawahi kupata kiti ukiachilia uchaguzi ule wa kura za maruwani?! Why Arusha na isiwe Ubungo, Mbeya au Iringa?! What's so special in Arusha ukilinganisha na majimbo mengine ambayo yamewahi kuwa chini ya upinzani kwa vipindi mbalimbali kama vile TMK ambako kuna mengi kiuchumi hata kama wilaya yenyewe watu wake wengi ni maskini?! Acheni hisia mfu na mawazo ya kufikirika!!

11. N

Ngonini JF-Expert Member

#11
Aug 8, 2011
Joined: Sep 1, 2010
Messages: 2,024
Likes Received: 8
Trophy Points: 135
Hoja hapa ni kwa jinsi gani chadema wataweza kuwaelimisha wananchi wa majimbo yao wasiwe na hofu ya kukosa maendeleo kisa wamechagua upinzani? Hofu hii ipo na miongoni mwa wananchi na mfano mzuri ni jimbo la Bariadi magharibi ambalo lilikuwa upinzani kwa muda mrefu lakini baadaye wananchi walianza kuingiwa na hofu hii na baadaye upinzani ulianza kupoteza credibility na kurejea tena mikononi mwa ccm na kweli baada ya ccm kuchukua kulianza tena kuonekana project kubwa kubwa kama za barabara.

Mimi naamini cdm wanahitaji kuwaelimisha wananchi wajue kuwa wanayo haki ya kuandamana kudai haki ya matumizi ya kodi zao kama hawataona Maendeleo yoyote bila kujali chama gani walikichagua. Wananchi wakijua haki hii serikali itawajibika na kazi ya wapinzani itakonekana machoni mwa wananchi.

Swali langu kimsingi lilitaka kujua kama cdm wanamkakati wa kuwaelimisha wananchi wake kuhusiana na dhana ya maendeleo kuletwa na ccm badala ya serikali na ni haki yao ambayo wanaweza kuidai hata kwa maandamano bila kujali itikadi ya vyama vyao.

12. myhem

myhem JF-Expert Member

#12
Aug 8, 2011
Joined: Nov 1, 2010
Messages: 932
Likes Received: 8
Trophy Points: 35
Mbona hata Singida,Rukwa,Mara zote ziko nyuma kimaendeleo? Au huko nako wamejaa waislamu? Kwa taarifa yako hata Kigoma ukiondoa Ujiji maeneo mengine yamejaa wakristu.

Kitu kimoja nilichojifunza kuhusu watu wa pwani ni kwamba wengi wao hawapendi kufanya kazi ngumu ndo maana wanakimbilia mjini kufanya biashara.Kwa kifupi ni wavivu sana na hiyo imepelekea kufanya mikoa mingi iliyopo ukanda wa pwani kuwa nyuma sana kimaendeleo.Nadhani sasa hata CCM isifanye kosa lingine la kuchagua mgombea urais kutoka pwani kani imedhihirika kuwa ni mzigo kwa taifa.

Mwisho nakushauri uwe unajenga hoja zaidi kuliko kuleta mipasho humu jamvini!

13. Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

#13
Aug 8, 2011
Joined: Nov 25, 2010
Messages: 31,817
Likes Received: 36,921
Trophy Points: 280
Nani alimbagua nani?

14. SaidAlly

SaidAlly JF-Expert Member

#14
Aug 8, 2011
Joined: Jan 22, 2011
Messages: 1,806
Likes Received: 648
Trophy Points: 280

Nawe pia hoja yako ni ya kufikirika vilevile. Unasema ''Acheni mawazo ya kufikirika'' tuambie tofauti ya Mawazo na Kufikiri.

15. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#15
Aug 8, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,107
Likes Received: 22,163
Trophy Points: 280

Wavivu wa kujenga barabara, mashule, viwanja vya ndege, bandari, umeme, maji. Nimekuelewa na wala sikushangai!

16. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#16
Aug 8, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,107
Likes Received: 22,163
Trophy Points: 280
Nyerere na aliokuwa akiwatumikia waliwabagua Waislaam.

Loading...