Swali kwa CHADEMA: Lowassa aliwaeleza nini hadi mkamkubali?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Lowassa sasa yuko CHADEMA. Ni mwanachama halali. Lowassa amehamia huko akitokea CCM yetu. Iliripotiwa kuwa Lowassa alijieleza mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA kiasi cha kukubaliwa kujiunga nao na baadaye kuwa mgombea wao wa Urais mwaka jana.

Ilielezwa kuwa Lowassa alijieleza vya kutosha juu ya makandokando yake ya ufisadi anaoshutumiwa nao. Ikasemwa kuwa Lowassa alijieleza kwa hatua kuhusu kashfa anazohusishwa nazo,ikiwemo kashfa ya Richmond. Hatimaye akakubaliwa. Akajiunga nao.

Sasa maswali,Lowassa alieleza nini hasa? Alimtaja nani? Alisema kwanini hutajwa yeye? Mlithibitishaje maelezo yake,yaani ukweli wa alichokisema?

Nakala kwa:
Tumaini Makene
freeman mbowe
Ben Saanane
Yericko Nyerere
mpk
Salary Slip na wengineo

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)
 
Na alichokisema ndicho kinasababisha CCM wanuogopa na kumuota kila kukicha
 
Kwa Jinsi ninavyoichukia CCM hata nilisikia Yohana Mbatizaji kafufuka na anafanya shuhuli zake za ubatizo pale lumumba, wallah siendi.........wapo wengi kama mimi Nchi hii, hata kama Lowasa alikuwa na shida zake lkn kwa yy kuhamia tu CDM watu wakasahau yote ya nyuma na ss wanajenga Chama.
 
Mkuu mbona hamtuambii huko alikokuwa alifanya ufisadi gani hadi kulazimika kujieleza CHADEMA? Cha ajabu kwenye uchaguzi kashinda mkatumia dola na Tume ya Lubuva kumpoka ushindi. Cha kutisha ni pale CC ya CCM inakuwa na agenda ya Lowasa kati ya agenda muhimu.

Nadhani una kila sababu na nondo za kujibu hoja yako ila unatuzuga. Haya bwana; ebu tumbueni jipu la sukari tupate haki yetu ya kifungua kinywa.
 
Alisema, muhusika ni mamlaka iliyokua juu yake! Kuwa kwenye baraza la mawaziri alitaka kutoupitisha mkataba, baada ya mapumziko na kurudi kikaoni akaelezwa kuwa maagizo yametoka kwa mamlaka ya juu kuwa mkataba upitishwe!

Ndio maana wale wote waliokuwa kwenye baraza la mawaziri hakuna hata mmoja aliyewahi kumsema lowassa juu ya richmond kwasababu wanaujua ukweli. Pia hii inatoa maana ya kwanin tume ya Mwakyembe ilificha baadhi ya sehemu ya report yao kwa madai kuwa serikali ingetikisika!

Pia haikuingia akilini kwanini tume itoke nchini mpaka ughaibuni kuchunguza na kukamilisha report bila hata kumhoji wakati alikuwa hapa hapa Dar es salaam. Pia akasema yuko tayari kufikishwa mahakamani ili mbivu na mbichi zijulikane.

Mpaka leo serikali imesua, inafahamu fika ikimpeleka mahakamani hata kiapo cha usiri wa baraza la mawazi wanachokula mawaziri utatenguliwa na mahakama na mawaziri wa wakati huo wataitwa kuhojiwa mahakamani, hapo ndio kasheshe!

Kwa vigezo vyote hivyo upinzani uliridhika!
 
Tuhuma za ufisadi wa EL zina umri mkubwa kuliko neno fisadi. Inadaiwa '95 alienguliwa kwenye urais kwa sababu hakuwa safi (fisadi). Na hata baada ya hapo tuhuma za ufisadi ziliendelea kumwandama. Kubenea alipoandika EL hasafishiki haikuwa jambo dogo. Sidhani kama alijieleza lolote la maana bali zilikutana pande mbili zilizokuwa zikiitaka Ikulu kwa udi na uvumba wakakubaliana EL agombee urais ili kila upande utimize malengo yake.
 
Lowassa sasa yuko CHADEMA. Ni mwanachama halali. Lowassa amehamia huko akitokea CCM yetu. Iliripotiwa kuwa Lowassa alijieleza mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA kiasi cha kukubaliwa kujiunga nao na baadaye kuwa mgombea wao wa Urais mwaka jana.

Ilielezwa kuwa Lowassa alijieleza vya kutosha juu ya makandokando yake ya ufisadi anaoshutumiwa nao. Ikasemwa kuwa Lowassa alijieleza kwa hatua kuhusu kashfa anazohusishwa nazo,ikiwemo kashfa ya Richmond. Hatimaye akakubaliwa. Akajiunga nao.

Sasa maswali,Lowassa alieleza nini hasa? Alimtaja nani? Alisema kwanini hutajwa yeye? Mlithibitishaje maelezo yake,yaani ukweli wa alichokisema?

Nakala kwa:
Tumaini Makene

freeman mbowe

Ben Saanane

Yericko Nyerere

mpk

Salary Slip na wengineo

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)

Tafuta hela hela kwa mchagga ni kila kitu
 
Tuhuma za ufisadi wa EL zina umri mkubwa kuliko neno fisadi. Inadaiwa '95 alienguliwa kwenye urais kwa sababu hakuwa safi (fisadi). Na hata baada ya hapo tuhuma za ufisadi ziliendelea kumwandama.


kuna mambo mengine hata kuandika lazima ujifikirie hasa mtu kama wewe toka 95 mtu analiibia taifa kaachwa kaja awamu ya kikwete kapewa uwazir mkuu hivi kweli unafikiria wewe? unataka kutuambia kuna baadhi ya raia wa nchi hii ni ruksa kuiba? basi serikali yote haifai kwa kufuga wezi had leo hii mtu analitia taifa hasara kapewa na uwazir mkuu si ajabu bas viongoz wote wa taifa hili ni wezi kwa maelezo yako!!!! hii nchi ya ajabu sana.
 
Back
Top Bottom