Tumeshuhudia mateso makali na ya kinyama aliyofanyiwa Dr Ulimboka, alitekwa akapigwa kwanza ndani ya gari na baadaye katika Msitu wa Pande, ambako ndiko alikokutwa asubuhi akiwa hoi bin taaban. Madaktari wenzake wanasema kavunjwa mbavu, mikono na taya. Pia kangolewa meno mawili ya mbele na kunyofolewa kucha.
Sasa viongozi wanasema hawahusiki na tukio hilo lakini waathirika wanasema wanamjua mhusika. Hakuna anayemtaja mbele za watu mhusika huyo ni nani, lakini kwenye vijiwe, kila mtu anataja kuwa serikali inahusika na kwamba wahusika ni Kijitonyama.
Ukiuliza Kijitonyama ni nani, wanasema ni wenyewe hao hao serikali. Kiongozi wa nchi kasema serikali haihusiki lakini yaelekea raia hawamwamini na hawaiamini serikali kuwa haihusiki. Lakini mngoaji meno, mvunjaji mbavu, mikono na mataya atakuwa nani na kwa nini?
Na kwa nini mtu mwenyewe anayevunjwa mikono, mbavu na taya ni yule tu mwenye ugomvi na serikali? Kama ni kweli waliompiga Dk. Ulimboka, wakamvunja taya, mikono, mbavu na wakamnyofoa kucha walikuwa wakimhoji eti nani wanakutumia kuongoza migomo, je, ni nani hao wapigaji?
Source: ************************** wavuti - wavuti
Ulichomuuliza Ahmed Msangi ACP ni kipi? Anyaway hata hivo mie nimekuwa nikijiuliza baada ya Dr Deo (achana na Abeid) kuona mwenzie Dr Ulimboka kachukuliwa mzobe mzobe katika hali ya shari,,as we're told alichukua hatua gani tokea hiyo saa 3 usiku hadi alipokuja okotwa asbh?
sasa hapo ndo umemuuliza ACP Msangi au!?!?!?
Mie mwenyewe ndio nimeshangaa!! Kichwa cha habari na story wala haviendani.sasa hapo ndo umemuuliza ACP Msangi au!?!?!?
NegativeHivi baba mwenye familia akimchapa mwanae afu mwanae akamshtaki baba yake kwa mama alafu baba aliyetoa kipigo aseme anaunda kamati yeye akiwa mwenyekiti wa hiyo kamati wachunguze kwanini mtoto alipigwa kweli huyo atapata haki kweli
Ulichomuuliza Ahmed Msangi ACP ni kipi? Anyaway hata hivo mie nimekuwa nikijiuliza baada ya Dr Deo (achana na Abeid) kuona mwenzie Dr Ulimboka kachukuliwa mzobe mzobe katika hali ya shari,,as we're told alichukua hatua gani tokea hiyo saa 3 usiku hadi alipokuja okotwa asbh?