Swali kwa ASP Msangi........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa ASP Msangi........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bisek, Jul 10, 2012.

 1. B

  Bisek Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumeshuhudia mateso makali na ya kinyama aliyofanyiwa Dr Ulimboka, alitekwa akapigwa kwanza ndani ya gari na baadaye katika Msitu wa Pande, ambako ndiko alikokutwa asubuhi akiwa hoi bin taaban. Madaktari wenzake wanasema kavunjwa mbavu, mikono na taya. Pia kang’olewa meno mawili ya mbele na kunyofolewa kucha.

  Sasa viongozi wanasema hawahusiki na tukio hilo lakini “waathirika” wanasema wanamjua mhusika. Hakuna anayemtaja mbele za watu mhusika huyo ni nani, lakini kwenye vijiwe, kila mtu anataja kuwa serikali inahusika na kwamba wahusika ni Kijitonyama.

  Ukiuliza Kijitonyama ni nani, wanasema ni wenyewe hao hao serikali. Kiongozi wa nchi kasema serikali haihusiki lakini yaelekea raia hawamwamini na hawaiamini serikali kuwa haihusiki. Lakini mng’oaji meno, mvunjaji mbavu, mikono na mataya atakuwa nani na kwa nini?

  Na kwa nini mtu mwenyewe anayevunjwa mikono, mbavu na taya ni yule tu mwenye ugomvi na serikali? Kama ni kweli waliompiga Dk. Ulimboka, wakamvunja taya, mikono, mbavu na wakamnyofoa kucha walikuwa wakimhoji eti “nani wanakutumia kuongoza migomo,” je, ni nani hao wapigaji?


  Source: ************************** wavuti - wavuti
   
 2. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,208
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  sasa hapo ndo umemuuliza ACP Msangi au!?!?!?
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi na mimi naomba kuuliza je Polisi wamefikia wapi katika kuwashika wahusika au watuhumiwa kwa kuanzia na yule ofisa aliye kuwa ana ongea na Dr Ulimboka na Dr Deo siku ya tukio, halafu kuwashika watu aliokuwa anawasiliana nao huyo ofisa kwa kutumia call log? au hatuhabarishwi hizo habari kwa kuwa wahusika ni wao wenyewe? kwani ingekuwa sio wenyewe mida hii tungeisha tolewa Picha za Ofisa wa ikulu feki, na hao watuhumiwa wenzake.
   
 4. s

  sawabho JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Binafsi nahofia pale wezi wa kuku na wale wanaokata nyavu za madirisha usiku watakapoonyeshwa kuwa ndio wahusika wa huu mkasa !!!
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aulizwe pia kama kile kikosi chake cha kuiba kwenye malori ya Mizigo "SHUSHA SHUSHA" kama bado kipo na kimeshamuungizia Shs ngapi hadi sasa?
   
 6. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ulichomuuliza Ahmed Msangi ACP ni kipi? Anyaway hata hivo mie nimekuwa nikijiuliza baada ya Dr Deo (achana na Abeid) kuona mwenzie Dr Ulimboka kachukuliwa mzobe mzobe katika hali ya shari,,as we're told alichukua hatua gani tokea hiyo saa 3 usiku hadi alipokuja okotwa asbh?
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hivi wewe ndio unaingia huku mara ya kwanza au ndio unasoma hii taarifa kwa mara ya kwanza? Deo kazungumza mara nyingi kwenye vyombo vy habari kuwa alienda polisi muda ule ule na wakamtafuta vituo vingi vya polisi bila mafanikio mpaka walivyopigiwa simu asubuhi kweli unashangaza.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi baba mwenye familia akimchapa mwanae afu mwanae akamshtaki baba yake kwa mama alafu baba aliyetoa kipigo aseme anaunda kamati yeye akiwa mwenyekiti wa hiyo kamati wachunguze kwanini mtoto alipigwa kweli huyo atapata haki kweli
   
 9. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mie mwenyewe ndio nimeshangaa!! Kichwa cha habari na story wala haviendani.
   
 10. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,208
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Negative
   
 11. C

  Cecy Emmanuel Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Deo alienda police kutoa taarifa usiku ule ule ila jeshi la police halikumpa ushirikiano kama ungesikiliza mahojiano kati ya Dr. Deo kwenye clouds ndio ungejua kwa asilimia 100 police wanahusika...
   
Loading...