Swali: Kuna Njaa au Hakuna Njaa Tanzania???.

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Upande 01: Kuna Njaa Tanzania.
Upande 02: Hakuna Njaa Tanzania.

Serikali: Hakuna Njaa Tanzania.
Vyama vya Upinzani: Kuna Njaa Tanzania.

Viongozi wa Dini: Kuna Ukame na Njaa Tanzania, tumwombe Mwenyezi Mungu atuepushie mbali na hili.

Baadhi ya Wananchi: Kuna Njaa Tanzania.
Baadhi ya Wananchi: Hakuna Njaa Tanzania.

Wasomi na Wanataaluma kama Ma Dr na Prof. kwenye vyuo vyetu vikubwa wako kimyaaaa. Au wanatengeneza proposal wakafanye research kabisa kama kuna njaa Tanzania ama la!!!!.

Tunakumbuka sijui usemi usemao Mwenye shibe hamjui mwenye njaa????.

Kuna Njaa au Hakuna Njaa Tanzania???.
 
Debe la mahindi 20000 sasa kufikia mwezi wa tatu litakuwa 40000
 
Njaa ni matokeo ya kutokupatikana kwa mavuno ya mazao ya chakula kwa sababu ya majanga yanayotokana na hali ya hewa mfano mafuriko yanapoharibu mashamba au ukame unaosababishwa na ukosefu wa mvua.
Hili la pili haswa ndiyo limekumba baadhi ya maeneo hapa nchini. Ukame ni hatua ya kwanza na inafuatiwa na njaa endapo utaendelea kwa kipindi kirefu.
Hivyo basi kutokana na kwamba majira ya mvua yanatofautiana hapa nchini zipo sehemu ambazo tayari ukame umeshakuwepo kwa muda mrefu kiasi cha kuleta njaa na pia kuna sehemu zingine ukame ndiyo umeanza hivyo sehemu hizi kuhofiwa kuishia kwenye njaa.
Wanaopinga wanaishi kwa matumaini badala ya uhalisia.
 
Back
Top Bottom