Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,696
119,329
Wanabodi,

Hili mada ya swali kuhusu tabia ya kususa, kisiasa, huu mtindo wa kuzira au kususa susa, kususia kila jambo usilokubaliana nalo, sio tabia za kike hizi?, au sio tabia za kitoto?!. Mtu unasusia jambo fulani la kisiasa, ili upate nini?. Kususia jambo lolote la kisiasa bila kupiga hesabu ya what do you want to achieve na kususa huko, sio political suicide?.

The Motive Behind Kususa.
Jee ni nini the motive behind kususa jambo fulani, una susa ili uachieve nini, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata kile walichokusudia?!. Kususa jambo fulani bila malengo, sio tuu ni utoto, bali ni ujinga, kwa sababu ni sawa na kumsusia ngedere shamba la mahindi!, utayavuna mabua!.

Kususa Kwa Watoto, ni Attention Seeking, Kunatokana na Kudeka!.
Nakumbuka nikiwa mtoto, kususa ni kuonyesha protest ili kupata attention, kisha ubembelezwe!. The motive behind kususa kwingi kwa watoto ni ama ku create attention au kutaka kudeka. Mtoto anaesusa ama kuzira, hutaka kubembelezwa, na akibembelezwa, anaishia kudeka!.

Kwenye kususa huku kwa watoto, kuna kususa kwa protest kuna kususa kwa attention seeking, kudeka. Jee hawa wasusasi wa siasa, ni protest au wanataka kutudekea?, Kama ni protest, wana protest nini?, na kama ni kudeka, wanataka kumdekea nani?.

Kuna Tabia za Kike na Tabia za Kiume
Kwa hapa naomba kwanza kuomba radhi wanawake wote, ni mama zetu, bibi zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, wake zetu, wachumba wetu, wapenzi wetu na binti zetu, samahanini sana, ukizaliwa mwanamke uanamke wako sio tuu ni yale maumbile ya kike, bali hormones, tabia, mwenendo na thinking. Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume zaidi ya sex organs ni emotions and reactions katika situations mbalimbali, ndio maana wewe mwanaume ukifiwa hata na baba yako mzazi, unapigiwa simu unaelezwa, na mwanamke, unauliza kwanza yuko wapi, kama yuko sokoni, utasubiri arudi nyumbani. Baadhi ya tabia kama kulia kwa sauti na kujigalagaza, kuwa na tabia za umbeya, uoga, etc, kunaelezwa ni tabia za kike, hata mtoto wa kiume akililia lia, anaambia usililie lie kama mwanamke. Baadhi ya tabia za kulia lia katika siasa, ni tabia za kike, wanaume wao wamefundishwa kupambana na sio kulia lia!.

Kususa, Kuzira, Kugoma ni Tabia za Kike!.
Hizi za kususa, kuzira na kugoma ni tabia za kike, zimekuwa zikiendelezwa sana na wanawake, kwa lengo la attention seeking kama watoto, ili wabembelezwe, au kukomoa, ili kuadhibu. Mfano mke, au mpenzi wako wa kike, akigundua kuwa kuna mwenzake, na yeye amesaidiwa katika kumhudumia mtu wake, yeye anaamua kususa kutoa zile huduma, ili kukukomoa na kukuadhibu kwa hoja kuwa kama kuna mwanamke mwingine anayekutosheleza, mimi unanifuatia nini?. Wanawake wengi hawajijui kuwa wana ladha tofauti tofauti, hivyo mwanaume hata kila siku akipikiwa pilau na kukarangiziwa, kuna siku ana hamu tuu ya kubadili mboga!. Wanawake hususa kwa hasira ili kuadhibu na kukomoa usirudie tena!. Hivyo kususa kwao, kuzira kwao na kugoma kwao, kuna kitu they want to achieve.

Au mume ukirudi home umechelewa sana usiku mkubwa karibu na alfajiri, huku umelewa, mke anasusa kukufungulia, mlango eti rudi ukalele huko huko ulikotoka!, akiamini ameishahudumiwa umekula umeshiba!.

Ukimbeleza mke, anakusamehe, unafunguliwa mlango, mke anarudi room na kukupiga biti usimguse!, ukiendelea kubembeleza, kumhaikishia hujahudumiwa popote na yeyote, baadhi ya wanawake wana set conditions,zawadi,dhahabu,gari, nyumba, etc na mambo yanakwisha, unapewa huduma na life goes back to normal, ila pia wewe mwanaume inakubidi kushukuru kwa kumpiga tuu na hata na kizawadi cha kikanga, kitenge, au ki auting, hivyo kwa sisi wanaume wa Kiafrika wenye tabia za Kiafrika, hii tabia ya kuchepuka, kususiwa na kusamehewa, ni kitu cha kawaida sana, wengi wa wasusaji, huwa wanasusa kutokana na hasira, lakini hasira zikipoa, kususa huwa kunaisha. Sasa ikitokea wewe mtoa huduma za ndani sio bingwa, mume wako, mchumba wako au mpenzi wako kakutana na bingwa, halafu wewe unajifanya kususa!, ndio nitolee!. Hivyo kabla ya kuamua kususa, jitathimini unasusa ili kuachieve nini, japo susa nyingi ni za hazira tuu, hasira zikipoa, kususa kunakwisha.

Kufuatia Kususa Kufanywa Zaidi na Wanawake na Watoto, Jee Kususa Kisiasa Ni Tabia Za Kike?, ni Tabia za Kitoto?.
Kufuatia kususa susa kufanywa zaidi na wanawake na watoto, jee huku kususa kisiasa sio tabia za kike?!. Tabia za kiume ni kukabili, kupambana, kufight to the end hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu!. Jee hawa wasusaji wa kisiasa, tuwaite wana tabia za kike au za kitoto?.

Tofauti ya Mgomo na Kususa. Tutofautishe Mgomo, Kususa na Kuzira.
Mgomo ni kugomea kitu kwa malengo mahsusi na hufanyika kama hatua ya mwisho baada ya juhudi nyingine zote za mazungumzo kushindikana. Kususa a kuzira ni kugoma kwa hasira, bila mazungumzo yoyote na no conditions set. Migomo ni kama mgomo wa wafanyakazi, inayoitwa industrial action, na hufanyika baada ya majadiliano kushindikana. Migomo hii ni kulazimisha jambo fulani lifanyike, na wasiposikilizwa, mgomo huo utaleta madhara. Mgomo hutanguliwa na conditions set, na ultimatum set, na wasiposikilizwa, wakigomo, mgomo huo unaleta madhara fulani, hivyo hutumika kama shinikizo, ili kuzuia wasigome na kusitokee madhara. Jee kususa huku kisiasa kutokushiriki uchaguzi ni mgomo, kuna conditions set, ukigoma, unamgomea nani, unaigomea NEC, nchi, au Watanzania?. What are the conditions set?.

Kususa Kisiasa, Lengo Lake ni Nini?. Jee Kususa, Huku, Kumewahi Kuzaa Matunda?!.
Kuna msemo wa Kiwahili usemao, "ukisusa wenzio twala", jee kuwasusia ngendere shamba la mahindi, kutasaidia au watu walisusa tuu ili wabembelezwe?, na wasipobembelezwa, jee kususa huku kuna faida kwao?!. Ili kususa kuwe ni mgomo, inabidi mgomo huu uwe na malengo, na kama wasiposikilizwa, then kutaleta madhara fulani, ukisusia jambo ambalo halitaleta madhara yoyote, na hakuna mazungumzo yoyote, hakuna conditions, ukigomea kushiriki uchaguzi, huku wengine wanashiriki, ndio unakuwa unagomea nini?!. Ingekuwa ukigoma uchaguzi unasimamishwa, then kugoma huko ndio kungekuwa na manufaa, lakini wewe unagoma, wenzio wala, mwisho wa siku wewe mgomaji ndio the biggest looser!.

Tume ya Uchaguzi ni Tume Huru au Sio Huru?.
Kiukweli kabisa sio tuu Watanzania hatupatiwi elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi, bali hata wanasiasa wenyewe, hawajishughulishi kujua the electoral process, hivyo matatizo mengi ya uchaguzi, hayasababishwa ni kitu kinachoitwa tume bali ni wahusika tuu kushindwa kufuata sheria, taratibu na kanuni. Ukiisoma sheria yetu ya uchaguzi na kuangalia the electoral process yetu, utakubaliana na mimi kuwa NEC ni Tume huru ya Uchaguzi, na kama sheria, taratibu na kanuni zitazingatiwa, then NEC inaweza kuendesha a free and fare election.

Jee Hoja ya Msingi ni Tume ya Uchaguzi au Sheria ya Uchaguzi?.
Hoja kuwa Tume ya Uchaguzi NEC sio tume huru kwa sababu tuu watendaji wakuu wote kuanzia mwenyekiti, mkurugenzi na ma kamishna, wanateuliwa na rais, haina mashiko kwa sababu hata mahakama, ni rais anateua jaji mkuu, msajili wa mahakama na majaji wote na bado zinatoa haki. To be honest from the bottom of my heart, kwangu the composition ya NEC sio hoja, tunaweza kuwa na tume inclusive kama ZEC kwa kujumuisha wawakilishi wa vyama vikuu vya siasa, na bado yakafanyika madudu ya ajabu kama kilichotokea Zanzibar ile 2015!.. Hoja kwangu ni sheria ya uchaguzi.

Kwangu NEC Sio Hoja, Hoja ni Sheria Mbovu za Uchaguzi.Kwa maoni yangu, tatizo kuu la kwanza ni sheria mbovu ya uchaguzi. Kwa vile subject matter ya uzi huu ni kususa, naomba wanaotaka kujua matatizo ya sheria yetu ya uchaguzi, wanatembelee hapa
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. - JamiiForums

Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!. - JamiiForums

Uwanja wa Siasa Hauko Sawia Hivyo Kuleta Ushindani Usio Sawia.
Siasa unaitwa mchezo wa siasa, the political game, sasa uwanja wa mchezo huu kwa Tanzania, hauko sawia, yaani the political playing ground in Tanzania, is not level, umelalia upande mmoja na sio kwetu pekee, bali kote, tena mchezo wenyewe huu ni mchezo mchafu kwa nchi za wenzetu zilizostaarabika na ni mchezo wa hatari sana kwa nchi masikini za ulimwengu wa tatu!, "politics is a dirty game and a dangerous game".

Siasa zetu ni kama kugombea kisu cha makali kuwili, mshindani mmoja ameshika kwenye mpini hala mwingine kwenye makali kuwili, kuanza kuvutana kuangalia nani atashinda!.

Mfano kwenye urais, mgombea mmoja anaingia na vingora, anatumia state machinery, polisi wake, jeshi lake, NEC yake, anasindikizwa na media team paid by the state, na kutumia state cars zilizofungwa number za kiraia, and using state resources, kushindana na mgombea mwingine mwenye nothing!.

Nchi za wenzetu za Scandnavia, hata kama na a seating president, ukigombea re election, unakuwa scraped zile state privileges zako zote, unabakishiwa ulinzi tuu, na wagombea wote wanakuwa treated equally, ndio maana tukiwaambia watu humu CCM itatawala milele, mtuelewe!.

My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki uchaguzi sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.

1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.

2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.

3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.

4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.

5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.

Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 26 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuyarejesha majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.

Hongereni sana CCM kwa ushindi mtamu.
Poleni sana Chadema/Ukawa kwa kupoteza majimbo, wabunge na madiwani.

Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!'

Nawatakia Furahi Day ya Ijumaa Njema.

Wasalaam.

Paskali

Rejea za kuhusu Kususa.
Baada ya uchaguzi wa 2010, Chadema ilisusia matokeo na kujidai kuwa hawamtambui JK, ila bunge tuu lilipoanza, niliibua mjadala huu
Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda

Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

Uchaguzi wa 2015 Ukawa wakadai Lowassa ndie mshindi, hivyo wakajifanya kususa, na kutomtambua Magufuli, mimi niliwapa ushauri ufuatao
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake - JamiiForums

Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!. - JamiiForums

Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz - JamiiForums

Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! - JamiiForums
 
pasco,
so mkuu ulitaka washiriki tu huo uchaguzi hata kama wao wanaona malalamiko yao hayasikilizwi??? haya tufanye kususa hakusaidii kwahio wakienda kwenye uchaguzi ambao wanaona hawajatendewa haki ndo watapata faida??? au kwasababu limefanywa na wapinzan labda??
 
Pasco CCM na wewe wamekununua?
Naamini atajibu aliyeulizwa, mi nataka kuchangia kitu hapa.

Binafsi sifahamu kwa sasa CUF wanasimamia nini. Hiki chama kilikuwa sehemu ya Serikali, mapungufu ya ZEC na ya mahakama kama yapo wamepoteza miaka mitano bila kuyarekebisha.

Sifurahishwi na kunyimwa haki lakini ukifikiria kwa upande wa pili ni kama mwenye hiyo haki haihitaji.

Nafasi waliyoipata CUF Zanzibar kama ingepatikana kwa CHADEMA bara hali ingekuwa tofauti sana. Kuna kitu hakipo sawa
 
pasco,


Jibu la swali lako nafikiri jibu unalo wewe mwenyewe na umeshaliandika kwamba kususa ni tabia ya mtoto hasa pale anapotaka attention sasa Wapinzani au wanaoitwa Wapinzani wasiposusa ina maana hakuna attention na kama hamna attention, basi no money, ila wakati huu wameingia choo cha kike kwa maana Magu hana huwo muda, yeye akili yake yote ipo kwenye kuindustrialize TZ na ,,atakayetukwamisha tutambomoa" kwa maneno yake mwenyewe Magu na hana muda wa kubembelezana mtu anayetafuta attention!
 
Wanabodi,

Hili ni swali kuhusu tabia, huu mtindo wa kuzira au kususa, sio tabia za kitoto hizi au tabia za kike?!. Jee ni nini the motive behind kususa, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata walichokusudia?!.

Nakumbuka nikiwa mtoto, kususa ni kuonyesha protest ili kupata attention, kisha ubembelezwe!.

Tabia hizi za kitoto, zimekuwa zikiendelezwa na wanawake, ati akigundua amesaidiwa katika kumhudumia mtu wake, na yeye anasusa kutoa zile huduma, eti nenda kapate kule kule!. Au ukirudi umechelewa sana karibu na asubuhi, anasusa kukufungulia, mlango eti kalele huko huko!.
Baadaye ukimbeleza yanakishwa na life return to normal, ambapo baada ya muda, utapatiwa tena huduma nje, na utachelewa tena kurudi, utasusiwa utanuniwa, utasamehewa and life goes on!.

Kufuatia kususa susa kufanywa zaidi na wanawake, jee huku kususa kisiasa sio tabia za kike?!. Tabia za kiume ni kukabili, kupambana, kufight to the end hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu!.

Sasa huku kususa kisiasa, lengo lake ni nini?. Huko kususa, kumewahi kuzaa matunda?!. Kuna msema wa ukisusa wenzio twala, jee kuwasusia ngendere shamba la mahindi, kutasaidia au watu walisusa ili tuu wabembelezwe, na wasipobembelezwa, jee kususa huku kuna faida kwao?!.

Nawatakia Ijumaa Njema.

Pasco
Pasco wa JF chukuwa maneno yangu kwa sasa Ukawa (cuf,chadema nk)..ni matawi ya CCM...watu muhimu,wazungumzaji wakuu ni mali ya CCM,hamna kuzira hii ni mipango mizito na sasa wameingia 18,nikikumbuka siku Kinana alivyosema Ukawa imebaki ukiwa baada ya Dr.Slaa na Prof.Lipumba kuondoka...hii ilikuwa siku Dr.Magufuli anaenda kuchukuwa fomu NEC...inahitaji uwe na uwezo mkubwa ili uelewe haya.
 
Pasco CCM na wewe wamekununua?
Mkuu The Big Boss, naomba nikuhakikishie katika maisha yangu yote, japo nina kadi ya chama cha siasa, sijawahi kuutumia uanachama wa chama changu cha siasa kwa kutanguliza mbele maslahi ya chama.

Paskali, anatanguliza mbele maslahi ya taifa, hanunuliki na yeyote kwa lolote kwa sababu hana price tag.

Mimi ni priceless, sio kwa chama changu CCM , wala Chadema, wala Ukawa, wala Lowassa wala Magufuli, au yeyote, hana uwezo wa kuninunua, kwa sababu I'm not for sale, na sina any price tag!.

Naomba uniamini hili ni swali tuu, nimeuliza hawa wanaosusa, wamesusa ili wapate nini?!.

Ni swali tuu.

Paskali
 
Back
Top Bottom