Swali kuhusu majina 97 tuhuma za dawa za kulevya

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Wakuu

Binafsi nina wasiwasi kiasi kuhusu yale majina 97 ambayo yalikabidhiwa kwa kamishna mpya wa dawa za kulevya bila kutajwa jina hata moja kama walivyotuzoesha.

Toka ishu hii au mapambano haya yameanza, majina kadhaa yametajwa, lakini si watajwa wote waliofika kuhojiwa kituo cha kati cha polisi. Ila swali langu linakuja kati ya haya majina 65 ya phase ya pili ambayo inasemekana ni WATUHUMIWA WANNE TU ndio walioripoti polisi, hiyo ina maana kwamba watuhumiwa 61 hawajaripoti polisi.

Swali langu ni je:

1. Hayo majina 61 yaliyobaki, yameunganishwa kwenye hayo 97, hivyo phase 3 ina majina mapya 36 tu..??

2. Kama kamishna ndo kapewa mamlaka rasmi kwa kukabidhiwa majina 97, na kma tunaamini hayo 97 ni MAJINA MAPYA KABISA, swali ni je inakuwaje kwa hayo majina 61 ya watu ambao hawakuripoti polisi kuhojiwa..?? Atakabidhiwa kamishna au yeye anaanza kushughulika na hao 97 wapya..??
 
Back
Top Bottom