VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Labda kuna Tanzania nyingi,ima hapa duniani au sayari nyinginezo! Kama nchi,tuliponyimwa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC),tuliambiwa na kuaminishwa kuwa Tanzania haikushtuka wala kuathiriwa na kunyimwa huko.
Viongozi wetu walituambia kuwa Tanzania yetu sasa inahitaji kujitegemea. Haihitaji misaada wala mikopo,hasa yenye masharti, kujiendesha. Fedha za MCC zikapondwa bila kupendwa. Zikaonekana si lolote na kunyimwa kwetu kunatuimarisha kama taifa.
Hakika,tuliambiwa Tanzania inataka kujitegemea na kujitenga na misaada pamoja na mikopo. Kuna mtiririko na mfululizo usio na likizo wa mikopo na misaada toka nchi za Ulaya,China,Japan na hata India. Ile Tanzania ya kujitegemea iko wapi?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)